Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari leo mchana,kwenye kituo cha Polisi Urafiki,mara baada ya kuwanasa watuhumiwa wa Kurudufu kazi za wasanii mbalimbali,aidha aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Bashir Abdul pamoja na Jofrey Anatori (Wakazi wa Mabibo jijini Dar) .Msama alisema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa maeneo ya Mabibo Mpakani,jijini Dar,wakiwa na mitambao yao pamoja na kazi mbalimbali walizozirudufu zenye thamani ya sh milioni 25.Aidha Msama amefafanua kua mpaka sasa wamekwisha wakamata watuhumiwa wapatao 10,wakiwa na mitambo yao,ambapo mpaka sasa wawili wamepata dhamana na wengine bado wako rumande.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akionesha baadhi ya kazi FEKI zilizorudufiwa na watuhumiwa hao,ambao wanaziuza kazi hizo kwa bei ya hasara kabisa na zisizo na ubora unaotakiwa.Msama ametoa wito kwa Wadau mbalimbali wakiwemo wasanii wenyewe kutoa ushirikiano katika jambo hilo ili kuhakikisha linatokomezwa kabisa kama si kupungua.
Mmoja wa Watuhumiwa akiwa na vifaa vyake vya kurudufia pamoja na kazi feki ambazo alikiwisha zirudufu tayari kwa kuzipeleka sokoni.
Baadhi ya kazi feki zilizokamatwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mabibo Mpakani,jijini Dar na kampuni ya Msama Auction Mart.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naona Msama wanataka kumfunika Mh.SUGU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...