Mdau akiwa kaambulia lita tano katika kituo kimoja katikati ya jiji jana jioni baada ya wafanya biashara ya mafuta wengi kusitisha huduma baada ya serikali kutangaza bei mpya ya nishati hiyo kwa madai kwamba kwao wafanya biashara imekuja ghafla mno na kwamba kwa vile wana stock ya zamani itakuwa ni hasara kuuza kwa bei ya sasa ambayo ni pungufu. Je, kifanyike nini ili kumaliza hii dhahama?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kwa bei kupanda, wanapandisha hata wakiwa na stock ya zamani, kushusha shughuli!

    ReplyDelete
  2. SERIKALI IMEJENGA URAFIKI WA KIJINGA NA WAFANYABIASHARA KIASI CHA KWAMBA HAWAOGOPI SERIKALI HATA KIDOGO..NAJARIBU KUFIKIRIA INGEKUWA SERIKALI KAMA YA QUEEN HAPA UINGEREZA IMESEMA HIVYO HAKUNA AMBAYE ANGEBISHA LABDA IWE KWELI HELA WATAKAYO UZIA HAYO MAFUTA HAKUNA FAIDA...NAAMINI SERIKALI IMEAMURU WAFANYABIASHARA WASHUSHE BEI YA MAFUTA HALI WAKIELEWA KWAMBA BEI WATAYOUZIA ITAWAPA FAIDA BILA YA WASI WASI ILA KWA SABABU WAFANYA BIASHARA HAWA HAWAIOGOPI SERIKALI YA BWANA JK BASI WANADINDA ILI KUPATA FAIDA KUBWA NA KUWATESA MAMA ZETU NA BABA ZETU NA NDUGU WENGINE.

    ReplyDelete
  3. Ajabu sana hawa wausa wese. Bei inapopanda haraka hukimbilia kuyaficha mafuta na kupandisha bei bila kujali ya kwamba ni stock ya zaman. leo hii wanaona bei imeshuka imekuwa vile na hivi...

    ReplyDelete
  4. waliogoma wafutiwe leseni na biashara hiyo hawaitaki kwa kifupi habari ndio hiyo.hawa ni wahujumu uchumi na sio kingine

    ReplyDelete
  5. Lakini sio sawa kwa serikali kupandisha bei ya mafuta ya taa simply kwa sababu wameshindwa kuwadhibiti wachakachuaji. Yaani unashindwa kudhibiti lakini unatumia njia ya kuwaumiza walala hoi wanaotumia mafuta ya taa kisa nini hawana wakuwatetea

    ReplyDelete
  6. MDAU NO.2 NAMUUNGA MKONO. KUFUTIWA LESENI/FINE NDIO SULUHISHO.KWANINI TAKUKURU ISIPINDWE KIDOGO IONGEZE MABAVU WAKASHUGHULIKIA NA MASUALA HAYO PIA????? WAINGIE SHELI, WANUNUE MAFUTA, KAMA WAKICHAJIWA BEI KINYUME NA TAMKO LA SERIKARI THEN WAKAMATE MUUZAJI NA WACHUKUE LESENI< BLOODY SIMPLE EEHHH??? PERIOD.

    ReplyDelete
  7. mimi nadhani serikali iwa warn ambao wamegoma kuuza mafuta na iwape 24hrs kuuza mafuta kwa bei ya serikali ilyoamuru nakama watapingana na serikali wafungiwe lessen zao zaid ya mwaka lakini waelezwe masharti kabla serikali haijachukua mkondo wake wakishupaza shingo serikali i take action. Hatuwezi kuongozwa na wauza mafuta lazima waheshimu mamlaka ya nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...