Bill Gates: mwanzilishi mwenza na afisa mtendaji mkuu wa Microsoft
Mark Zuckerberg, mwanzilishi mwenza, rais na afisa mtendaji mkuu wa Facebook
Steve Jobs: mwanzilishi mwenza na afisa mtendaji mkuu wa Apple.
Kupata chanzo na listi ya vipoba 15 wasiopiga pamba za nguvu
Haya wenye hela zao hawahangaiki na nguo Ankal mna msimanga na Fulanazzz kumbe umekaa kibopa bopa halafu kuna wale ndugu zangu wa jirani na Kigoma bora alale chini lakini apige pamba za nguvu na uturi wa bei ghali mno!
ReplyDeleteSitaki Kusema sana, ila uchunguzi wangu nimegundua wengi wenye hela wapo busy kujiweka sawa kila siku. Hawajali nini kavaa kwani kichwani mwake anahesabu mabillioni. Wengi tumekuwa na mawazo kuwa anayependeza na kutanashati basi mambo yake mazuri.
ReplyDeleteNimekaa USWAZI, Jirani kagonga Yai basi anazo, ukitaka kuudhi watu wewe tupa maganda ya mayai nje tu uone watu wanakupenda, watakuona unazo na wengine watakuchukia. Hii hali ya USWAZI nyumba za kupanga.
Sio kwamba yai ni kitu kikubwa au gharama sana NO, ila ni Idea ya tu kwamba Yai na USWAZI ni vitu viwili haviendani kwa sana, sasa ikitokezea mtu akagonga basi anazo. sasa tazama kalipata vipi yai?
[SHOW OFF]
Ndio maana tunakuwa busy kutafuta nguo za gharama ili tujionyeshe. Mawazo yetu kuridhisha watu ndio tunaridhika na sisi. Mtu akikwambia mambo yako si mabaya basi moyo wako unafurahi unajiona jamii inakupenda inakuona mtu wa maana.
Matajiri wao washajijua kuwa matajiri, kwanza akitakacho anapata ana miliki kampuni inawafanyakazi si chini 10000 na anawalipa wote, thamani yake ya utajiri ni mabillioni, sasa hana haja ya kujionyesha kwa kutumia nguo au vifaa, jamii inamjua tayari. Yaani Simu yako inatengenezwa na kampuni yake sasa utamweleza nini.
Wengi tunafeli hapo, tunatumia mapesa mengi kujionyesha kwenye jamii, sometimes tunakopa ili kutimiza tuyatakayo, matokeo yake unanunua suti za gharama ili uende kwenye sherehe au uko tayari kulipa laki 3 kwa kumuona SHAGGY AU JAY-Z wakati kwako friji linamwaga maji chini, jiko limeharibika, ukuta una UFA, Maji yamekatwa (Unaibia) tu, yote jamii ikuone na wewe ulikuwepo.
Matokeo yake tunabaki kwenye Umasikini kila siku, Tazama mfano mdogo, Kila mtu sio wote anataka Iphone or Ipad, ukimuuliza nini tofauti na ile laptop yake ya nyumbani hajui, anakwmabia ndio technology ilotoka mpya, na Smartphone anakwambia inamuwezesha kuwa close na rafiki zake all the time, rafiki ambao yupo nao kila siku.
Sasa tazama gharama zake ni zaidi ya au karibu na mshahara wake, matokeo yake IPad inakuwa show tu, sasa jiulize Una laptop, computer, smartphone, Ipad zote unaweza kufanya kazi moja, zote za nini?
Ndio matajiri wanatajjirika kavaa jeans lakini anakuuzia kitu usichokuwa na haja nacho, anakwambia unakihitaji sana hiki na wewe unajikuta upo kwenye mikono yake.
NI MAWAZO YANGU TU.
Bora hao wengine wanabadilisha, lakini jamaa wa Apple mmhh.. utadhani hilo vazi ni uniform. Maana kila siku!
ReplyDeleteAnonymous namba pili wewe ni BONGE la kichwa mkuu....tatizo watanzania tuna norrow mind ndo kinachotuponza na kutaka maisha ya juu...unakuta mtu ana mshahara mdogo but anataka kufanya vitu zaidi ya uwezo wake...
ReplyDeleteNa mimi nilikuwa na mawazo kama wadau wote mliotoa maoni yenu hapo juu mpaka nilipojua ukweli: Mimi na wewe tunaona pamba hizo ni za kawaida kwani mpaka tuone majina ndio tuone ya bei mbaya. Hizo pamba zinaonekana simple na si kama hawana muda wala hawapendi kujionyesha; Hizo pamba ni za ukweli na bei yake hugusi!!!! Si pamba utazozikuta madukani kama zangu na zako.
ReplyDeleteUmemsahau Richard Branson, yule tajiri wa kutupwa Mwingereza ambae hajawahi kuvaa suti wala tai tangu azaliwe. Huyu jamaa huwa anapiga masweta na mashati ya kawaida tu.
ReplyDeleteKila mtu na uchawi wake au ugonjwa wake. Ugonjwa wao unaujua? wote hao ni College Dropouts, too smart than their professors!!!!
ReplyDelete