mtafiti mwandamizi wa taasisi ya utafiti wa zao la kahawa (TACRI) Malyatabu Ngh'oma akimuelezea mkuu wa wilaya ya Bukoba samwel kamote namna wakulima wanavyoweza kuongeza ubora wa kahawa wanayoizalisha.
Thadeo Rweyemamu ofisa wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) akimuelezea mkuu wa wilaya ya Bukoba Samwel Kamote namna mfuko huo unavyowanufaisha wastaafu.
mmoja wa watumishi wa taasisi ya utafiti wa zao kahawa (TACRI) iliyoko katika kituo cha utafiti Maruku akimuonyesha akimuelezea mkuu wa wilaya ya Bukoba Samwel Kamote namna kituo hicho kinavyozalisha miche bora ya kahawa inayohilimi magonjwa alipotembelea banda la taasisi hiyo lililopo katika viwanja vya maonyesho ya nanenane.
baadhi ya watumishi wa ranchi za taifa zilizoko mkoani kagera ambazo ni pamoja na ranchi ya Misenyi, kikurula, mabare na kagoma wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao la maonyesho ya nanenane yanatoendelea yanayofika kilele chake leo yaliyokuwa yanafanyika kwenye viwanja vya maonyesho ya kilimo vya Kyakailabwa vilivyoko katika manispaa ya Bukoba.
msanii maarufu mkoani Kagera kwa jina la Rasi akimuonyesha nyani anayemiliki anayefanya vitendo vinavyoenda sambamba na vitendo vifanywanvyo na binadamu, nyani huyo anayevuta hisia za watu wengi yuko kwenye viwanja vya maonyesho ya nanenane yanayofanyika mkoani Kagera sasa anaoneka akijiangalia kwenye kioo.Picha na Audax Mutiganzi,Bukoba







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...