Waziri wa Elimu Dkt Jumanne Shukuru Kawambwa (kushoto) akifuatilia maelezo jana kutoka kwa Afisa Elimu Mkuu wa Wizara ya Elimu Jane Kamwera(kulia) kuhusu malalamiko ya baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne kulalamikia udanganyifu wanaofanyiwa na Wamiliki wa Vyuo Vya ualimu binafsi kuwa wanaweza kujiunga na Diploma ya Ualimu kwa sifa za Kidato cha Nne tu. Waziri huyo alipata maelezo hayo kwenye banda la Wizara hiyo wakati alipotembelea maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma
 Waziri wa Elimu Dkt. Jumanne Shukuru Kawambwa (kushoto) akiangalia jana maandishi maalum ya watu wenye ulemavu wa kutoona kutoka kwa Afisa Elimu Mwandamizi Msaidizi wa kitengo cha Elimu Maalum Wizara ya Elimu Amani Katembo(kulia) wakati alipotembelea  banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma
 Waziri wa Elimu Dkt. Jumanne Shukuru Kawambwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Dodoma mara baada ya kutembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane mjini Dodoma

Waziri wa Elimu Dkt Jumanne Shukuru Kawambwa (kushoto) akipata maelezo jana kutoka kwa Afisa Elimu Mwandamizi Msaidizi , Kitengo cha Elimu Maalum , Wizara ya Elimu Amani Katembo (kulia) juu ya matumizi ya mashine yakuchapa ya watu wenye ulemavu wa macho (typewriter ) wakati alipotembelea  banda la Wizara hiyo 
Na Tiganya Vincent, Dodoma

Waziri wa Elimu Dkt Jumanne Shukuru Kawambwa alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne imeandaa Mpango wa Elimu Juu unaolenga kuboresha mapungufu yaliyojitokeza huko nyuma katika utoaji wa Elimu ya Juu hapa nchini.

Dkt. Kawambwa ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Elimu kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayofanyika kitaifa mjini Dodoma.

Alisema katika Mpango huo Serikali inalenga kuboresha miundombinu ya ufundishaji na ujenzi wa hosteli nyingi kwa ajili ya kutatua tatizo la malazi kwa ajili ya wanachuo.

Dkt. Kawambwa alisema kuwa hatua hiyo pia inalenga kuwaendeleza wahadhiri kuanzia kwa ajili ya kusomesha katika Shahada za uzamili na uzamifu ili kupunguza tatizo la upungufu wa wahadhiri katika taalamu mbalimbali ambao watasaidia kuwaandaa vijana kuwa wataalamu katika fani mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa nchi.

Alisema kuwa ili kufanikisha zoezi hilo ya Chuo Kikuu kimoja hapa nchini kinaweza kuchaguliwa kuwa Kituo maalum cha kuwaanda na kuwafundisha wahadhari kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kujenga msingi wa kuwa na viwango vya Elimu sawa kwa wahadhiri wa vyuo vikuu vyote hapa nchini katika sekta ya ufundishaji na hivyo kuwa na wataalamu waliopikwa vizuri.

Dkt. Kawambwa alisema kuwa baada ya kukamilka kwa maandalizi ya mpango huo vyuo vikuu 38 vinavyotoa elimu ya Juu hapa nchini vitakuwa na fursa ya kuelimisha walimu wao katika Chuo Kikuu ambacho kitakuwa kimechaguliwa kwa ajili ya kufundushia wahadhari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...