Kaka Michuzi,
Pole kwa majukumu na hongera kwa kazi nzuri ya kuelemisha na kutuhabarisha. Mimi ni mmoja ya wapenzi wa Blog yako. Kwa leo nina tatizo kidogo naomba ikiwezekana uwahabarishe wadau.
Ni kwamba iwapo kuna yoyote atakayeweza kuwa ameona au atabahatika kuona au kusikia habari za Gari Namba T 962 AZR Toyota sprinter (Chasis No. AE1103037372 na Engine number 5AH871768) au vitambulisho vya Kazi, Card ya Bank, Driving Licence na documents nyinginezo kwa jina la Grace Kabate. Kwa mawasiliano iwapo kuna habari zozote namba 0688-477875 (Stephen) na 0754-64062 (Grace)
Asanteni kwa Ushirikiano wenu


pole sana mdau. swali langu umepotelewa au umeibiwa???? itapendeza kama utaelewesha vizuri hapa ili tukimuona navyo mtu tujuwe njinsi ya kumfesi,haya ni maoni yangu.
ReplyDeletepole sana ndugu. Sasa unasema hilo ni tatizo kidogo? au unayo mengi hayo magari?
ReplyDeleteDUH POLE SANA MDAU ..MIMI PIA NILISHAWAHI KUIBIWA GARI KIPINDI FULANI ILA LILIPATIKANA BAADA YA MUDA KWA TAARIFA ZA RAIA WEMA YANI INAUMA SANA JINSI MTU UNATAFUTA MALI ZAKO KWA BIDII HALAFU WAPUUZI WACHACHE WANAKUHARIBIA KAMA HIVO...HAYA MWENYE TAARIFA ASAIDIE WAPIGANAJI WENZETU
ReplyDeleteMDAU MWENYE UCHUNGU
haya mwenzetu ni kwamba umepotelewa na gari ukiwa na maana ya kwamba hukumbuki ulipo park au umeibiwa?kuwa muwazi upate kusaidiwa maana wengine watajua umesaha ulipopark.
ReplyDeletePOLE SANA MDAU. NILISIKIA STORY ZA KUIBIWA KWA HIYO GARI MAENEO YA SINZA MADUKANI. KWA WENYE MACHUNGU NA MAPENZI MEMA TUSAIDIANE MAANA HAWA JAMAA WANAUDHI SANA
ReplyDeletepolice kazi yao nini???.
ReplyDeleteDada yetu hebu rekebisha hivyo namba ya Voda kwani haiko fulu ..... imemiss some digit/digits flani hv ... pia elezea uliibiwa wapi na saa ngapi tuweze kukusaidia dada yetu ...
ReplyDeletejamani pole dah yaaani uwizi wa magari umezidi itabidi tuwe tunatembea wawili wawili ndani ya gari...pole sana dada labda utangaz magazetini pia !!
ReplyDeleteDADA KANDA YA ZIWA NINI? ETI UNA SHIDA KIDOGO??? UMEPOTELEWA NA GARI?? HEEE!!
ReplyDelete