ANKALNAKUMBUKA WAKATI TUNAPATA UHURU WA TANGANYIKA NILIKUWA MWANZA NA  KATIKA MAAJABU YALIYOJITOKEZA  NI KUZUKA KWA MAELFU YA JAMII YA PANZI KULE TANGA WANAITWA BARARE WALIOKUWA NARANGI ZA  BENDERA YA
 TANGANYIKA NA NAMBA 9, KWA KUMBU KUMBU YA UTOTO NILIOKUWA NAYO, WADUDU HAO WALIDUMU TAKRIBANI WIKI AU WIKI MOJA  KABLA YA KUTOWEKA. NAOMBA KUWAULIZA WADAU KAMA WANAKUMBUKA TUKIO HILI
 LA MAAJABU LILILOTOKEA KARIBU TANGANYIKA YOTE NA KAMA KUNA ALIYHIFADHI PICHA YA WADUDU HAWA WALIOTUSHANGAZA SANA NA KUSABABISHA GUMZO MITAANI  NA TAFSIRI ZA KILA AINA JUU YA TUKIO HILO KIPINDI HICHO, KUISHI KWINGI KUONA MENGI!

MDAU UMANGANI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Ndugu yangu Utoto ulikusumbua sana, we na wenzio mliona nzige maana walikuwa na rangi za kijani na njano mchanganyiko, sasa kwa kuwa mlikuwa excited na uhuru mkaona mambo ya ajabu pole sana

    ReplyDelete
  2. Sijawahi kusikia panzi waliokuwa na rangi hizo za bendera - hiyo ilikuwa ni illusion tu.

    Kama alivyoongea mdau hapo juu hao walikuwa nzige na wala hakukuwa na la ajabu lililotokea wakati wa uhuru wa tanganyika.

    ReplyDelete
  3. interesting, nimezaliwa miaka 10 baadaye, sijawahi sikia story hii, nadhani hao walikuwa nzige kama wadau hapo juu.

    ReplyDelete
  4. Hao pandandigwa

    ReplyDelete
  5. Hakuna panzi wa aina hiyo bongo la huko unakoakuita Umangani hata huko Uarabuni uliko pia hakuna hao panzi!!
    Halafu hakuna nchi inaitwa Umangani kila nchi za kirabu zina majina yake.Na wala hakuna kabila Arabuni linaitwa wamanga.

    ReplyDelete
  6. mimi hiyo story nimeisikia, na nimezaliwa miaka kadhaa baada ya uhuru.hao panzi wanaitwa tisa disemba. na niliambiwa wanatokea kipindi hiko tu(desember 9)

    ReplyDelete
  7. hata mie niliezaliwa miaka zaidi ya 20 baadae, nimewahi kusimuliwa hiyo story na wazazi wangu!!sidhani kama walinidanganya

    ReplyDelete
  8. Vijana kuweni na subra, acheni wazee wamjibu ndugu wa umangani. Maana wazee ambao waliokuwa vijana wakati huo ndio walioona kama kulikuwa na kitu kama panzi uhuru au la.

    Watu tuna tabia ya kusahau sana. Miaka mingi ijayo watu watabisha kuwa kwenye miaka ya themanini jamaa hakubadilika kuwa chatu pale Buguruni. Michuzi unakikumbuka kisa hiki cha kweli, maana wakati huo ndiyo ulikuwa unaanza anza kupiga picha.

    Mdau muuliza swali umetuchanganya kidogo. Umesema wakati wa uhuru ulikuwa Mwanza na hao panzi walionekana Tanga na sasa uko umangani, Mnh!

    ReplyDelete
  9. Naona wadau hapa wengi ni watoto wa juzi.
    Kama mambo hamjayaona au kuyasikia bora kwanza kuuliza wazee waliokua na akili zao wakati huo na mahali pasemwapo. Tafadhali msi misslead jamaa kwa pungufu ya fahamu zenu.
    Mimi binafsi NIMEWAONA hao panzi wakati huo wa uhuru. Ni kweli walitokea na tulikuwa tunawakamata na kuwachezea. Walikua wengi sana mwambao wa Tanga. Tuliwaita wadudu wa uhuru.
    Walikuwa na rangi za bendera ya Tanganyika na nambari tisa kwenye mbawa zao. Bahati mbaya sidhani kama kuna aliyekumbuka au hata kuwa na camera ya kuwapiga picha.
    Mdau anaeuliza ni kitu kilichotokea kwa uhakika kabisa.

    ReplyDelete
  10. Mdau mbona umeshupalia kuhusu Umangani!!??? Umangani ni lugha isiyo rasmi ya kusema ni Uarabuni na Wamanga pia ni lugha isiyo rasmi kumaanisha Waarabu. Ni kama kusema Bongo na Wabongo ni lugha zisizon rasmi zinazomaanisha Tanzania na Watanzania.

    ReplyDelete
  11. Yes. TISA DISEMBA! Yule mdudu anafanana na Kokontinko aka vunjajungu aka Brucelee aka Mantis. Hao wadudu walikuwepo hadi miaka ya 80 hadi 90 mwanzoni. Mimi nimekulia Morogoro na nimewaona hao jamii ya panzi. Pattern za michoro kwenye mabawa yao ina herufi namba 9 ingawa kwa ujumla ni wa kijani ila yeye ameshiba kuanzia shingoni hadi mkiani. Tusihamishe mada kitoto kwa kubishania Umanga na ujinga mwingine ambao si msingi wa request yake. Msaidieni mdau.

    ReplyDelete
  12. Sasa kumegeukia umanga na Uarabu.
    FYI Wamanga wapo......ni kabila kama vile walivyo Wasukuma au wachagga.
    Kuna makabila mengine katika nchi za kiarabu, na wengine hata matamshi fulani katika lugha yao ya kiarabu zinatofautiana.
    Kuna Washihiri, Wamanga, Zakwan, Ghamid, etc etc.

    Hebu tafuteni elimu kwanza, msiingilie vitu kimkichwa mkichwa tu!

    ReplyDelete
  13. Mdau unaeulizia neno Umangani. Kwa huku Zenji Umangani hasa hasa ni Omani na Wamanga ni waarabu wenye asili ya Oman.

    Wengine wanaitwa waarabu na washihiri (kutoka Shihri, Yemen). Kwa hivyo huyo jamaa hakukosea.

    ReplyDelete
  14. Afadhali mmoja ametuambia kuwa na yeye aliwaona. Mimi nimezaliwa Tanga katika ya miaka ya sabini na nilipata kusikia habari za panzi hao. Jamani msikurupukie mambo msiokuwa na hakika nayo.

    ReplyDelete
  15. Ni kweli watoto wa siku hizi hawana muda wa kuuliza mababu/mabibi zao historia za nyuma. Mimi nakubali kwani niliwaona kipindi hicho na nilikuwa darasa la pili.

    ReplyDelete
  16. Mmmh sijawahi sikia kitu kama hicho. Tatizo letu waafrika hatuna tabia ya kuweka vitu kwenye makabrasha yanayoweza kutumika kama kumbukumbu. Na miaka hiyo angetokea mtu akafanya hilo jambo angeonekana mchawi. Na angepiga picha angesemwa anajidai mzungu. Kwa sababu hakuna mahali tunapoweza kupata kumbukumbu ya vitu kama hivyo, tunajikuta tukibishia wanaotoa ushahidi kwa mdomo. Mimi binafsi siamini kitu kama hicho. Na kama walikuwepo panzi wa rangi hizo wasihusishwe na uhuru bali wachukuliwe kuwa walitokea tu.

    ReplyDelete
  17. .....Ok, kwa kumsaidia mdau kweli panzi hao wapo na mimi mara ya mwisho kuwaona ilikuwa Mbeya,mjini Mbalizi kwenye bonde la mlima Iwambi ambapo nakumbuka walikuwa wakikaa kwenye majani mabichi sana na walikuwa wakiluka asubuhi tu ila mchana hawaonekani. hiyo ilikuwa miaka ya 90 mpaka 97 na nakumbuka nilipoenda tena Mbeya miaka ya 2000 nilikutana na panzi hao so hawa panzi wapo wa aina mbili, coz kuna wanaonuka yaani ukiwashika hawakimbii ila wananuka na ukiwaangalia sana unaweza kusisimka kutokana na jinsi walivyo kwani walikuwa wanalangi nyingi na zinazofanana na bendera kama ilivyosema na wengi wao wanaruka na mara zote wakilala wanapandiana na hata ukiwakuta chini wanakua wanabebana. ASANTE, BY Andrew Chale,mdau libeneke..

    ReplyDelete
  18. Jamani, jamani, jamani,swali lililoulizwa ni ju ya pazi wa uhuru. Vipi mmanga katawala uwanja? ndiyo maana watu tunashindwa mitihani. Mada au swali ni juu ya panzi. Mmanga, mmanga, mmanga. Mwishowe munanikunbusha stori ya mmanga na mchaga walivyosafiri wakapewa kulala chumba kimoja cha hoteli. Mpaka machweo hakuna aliyesinzia. Ngoma drow.

    ReplyDelete
  19. Ninayo picha yake, ni tukio la kweli, wiki iliyopita nilimuoina panzi huyo Mbeya na picha yake ninayo. 0713560998 Daud.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...