Ankal Nakusalimu! 

Pole na vakesheni karibu tena Bongo. Sasa Ankali kuna ka jambo kananisumbua muda sasa. Nimeona leo nitafute ufumbuzi na msaada. naomba niwekee hii na wadau wahusika wanisaidie.

Ankali mimi ni kijana (Mwanaume) mwenye umri wa miaka 28, Nashukuru Mungu amenibariki kwani nina kila kitu maishani ambacho kinafanya leo hii niseme nina maisha mazuri. Nina elimu ya chuo na nafanya kazi nzuri kabisa. 

Ila nina shida moja. Sijapata mtu ambaye ananipenda na kuonyesha mapenzi ya dhati. Hilo tu ndio limekosekana kwangu ili kuniletea raha kamili ya maisha. 

Ambaye nilikuwa naye awali alionyesha kunijali mwanzoni na nilimpenda sana ila baada ya muda hakuonyesha kujali tena.Nimekuwa nikijaribu kumpenda na kumpatia kila kitu anachohitaji maishani pamoja na uhuru wa kujitawala mwenyewe lakini nilichovuna sicho nilichokitegemea toka kwake. 

So nikaamua kukaa mwenyewe kwa muda sasa. Nachotaka kusema hapa nahitaji msichana ambaye anaweza kuwa mke wangu kwa siku zijazo kama tukiendana kitabia. 

Niko serious kwa hili, nahitaji mtu mwenye elimu ya sekondari na kuendelea mtu mwenye upeo wa kuona mbele, mtu mwenye kujishughulisha na mtu mwenye kunijali na kunipenda kwa dhati kutokea moyoni mwake.

 Najua wapo watu wa aina hiyo labda imekuwa bahati mbaya kwangu sijaonana nao live. 

Please kama unajihisi waweza kuwa mmoja wapo Nitumie e-mail kupitia (fan.elli@yahoo.com ) then tutapeana information zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Kila la kheri broo!! However I don't think kama hii ni sehemu sahihi ya kutafuta mke, mtu ambaye unategemea kutumia the rest of ur life na yeye. Just think about it broo.
    Kuna sehemu unaweza ukakutana na mademu ambapo utaanzisha casual relationship, mfano kwenye party, shule wakati ukiwa shuleni, kazini, kwenye conference etc. Kwenye internet no, bar no
    Gudluck son

    ReplyDelete
  2. Pole sana kijana. Kutafuta mchumba ni kazi kubwa sana. Sijui dini yako ni ipi lakini nitakuambia kitu kimoja. Kwa usoefu wangu kama unataka mke hakuna kitu mapenzi. Isipokuwa kuna kitu kinaitwa umefika wakati uwe na mke na mwanamke nae amefika wakati kuwa na mume. Kilichobaki ni kuwa wewe kama mume utimize wajibu wako, na utakaemuoa nae kama mke atimize wajibu wake. Kuoa ushauri niliopewa mimi ni kuwa unatia mkono kizani. Na wewe nakupa ushauri huo huo. Kilichobaki usipoteze wakati na utakayekutana nae na akikwambia hana mume wala mchumba basi ndie huyo huyo oa.

    ReplyDelete
  3. Taratibu za upatikanaji za wachumba ziko katika njia mbalimbali kufuatana na chaguo lako linavyokugusa.Kama wewe ni mkristo ni vyema kujiunga kwenye kwaya kanisani na pia kushiriki matukio mbalimbali ya kidini ambayo yanawakutanisha warembo wengi wenye nia kama yako,kama unaangalia wenye elimu basi library ni mahala pazuri sana juu ya haja yako na mengine mengi ambayo yanaleta mikusanyiko ya watu.Cha msingi ni kuwa mkweli endapo utakutana na yule ambae umemwona kuwa ni chaguo lako.Nakutakia mafanikio mema.

    ReplyDelete
  4. mi niko tayari lakini nina miaka 35, unaweza kinioa kweli kama tukiendana au nitapoteza muda wangu tu

    ReplyDelete
  5. POLE SANA KAKA UNAJISUMBUA SANA KUANDIKA HUMU KWA KWELI..DAWA NI KUMUOMBA MUNGU AKUPATIE MKE MWEMA NA SIO TU HILO AKUPE HEKIMA YA KUANGALIA TU MWANAMKE NA KUJUA YUPI NI YUPI NAAMINI WAPO WATU WA NAMNA HIYO AKIKUTANA NA MTU NA KUONGEA NAYE MARA KADHAA ANAWEZA KUJUA TABIA YAKE MWANZO MWISHO HATA KAMA HUYO MTU ANAJIFANYISHA,HIYO NI HEKIMA NA SIO KILA MTU ANAYO BALI NI KARAMA TOKA KWA MUNGU,MIMI SIJIFII ILA MIMI NINAYO HIYO KARAMA NA WANAWAKE ZANGU WOTE TOKA HUKO NYUMA NILIKUA NAWEZA KUJUA TABIA ZAO KWA SIKU CHACHE TU NINAO KAA NAO.NAJUA KWAKO NI VIGUMU SANA KUJUA KAMA HUYU NI MKE MWEMA AU LA...KAMA HUNA KARAMA KAMA YANGU BASI PIGA GOTI MUNGU AKUONGOZE KWA MWANAMKE MZURI....NA HAPA NAANZA KUKUOMBEA MUNGU AKASAIDIE SANA MAANA NIMESHAKUTANA NA RAFIKI ZANGU WENGI NAO WANALIA KAMA WEWE,ILA MUNGU WETU NI MWEMA ATAKUJALIA SAWA NA HITAJI LA MOYO WAKO.

    ReplyDelete
  6. Hapo dogo 'utawamaliza'Ni kama umemwaga Petroli kwenye moto...Lakini kuwa mwangalifu sana na njia hii uliyotumia.
    David V

    ReplyDelete
  7. Sasa mtu wa kukupenda kwa dhati hata picha yako tu hajawahi kuiona kweli hili linawezekana? Good lucky.

    ReplyDelete
  8. Kwa tabia yako ya kujisifu kuwa una kila kitu kinachohitajika maishani,kazi, na Elimu nzuri - ambayo huenda haina hata mchango wowote kwenye jamii bali umebakia tu kulalia makaratasi ni wazi kuwa hustahili kupata mke mwenye sifa ulizozitaja - mchapakzi, anayeona mbele n.k., bali Kinachowezekana ni kupata mke mwenye tabia na mitazamo kama yako. Kingine ni kwamba inaonekana wewe unataka tu kupendwa lakini wewe hupendi, na kinachoonekana ni kwamba wewe ulishawahi kupata mtu aliyekupenda lakini ulishindwa kumjali na kumpenda. Upendo unatengenezwa, unapaliliwa, unatunzwa, unathaminiwa na kuendelezwa. Lakini wewe unataka mambo kirahisirahisi ndio maana haukwenda mbali na yule mke wa kwanza- kama mlikuwa mnazini lakini hamkuoana huo ni uzinzi! Jirekebishe kwanza ndio ufikirie kuoa maana unataka kurudia mtihani ambao ulishaufeli vibaya mno. Napita tu.

    ReplyDelete
  9. Kaza buti tu mimi nilitumia njia hiihii nikapata mke mwema sana na mwenye upendo na kunijali.Huko makanisani kuna wasanii utajuta,jambo hilo ni kuomba Mungu tu atakusaidia kukuonyesha atakayekuwa mke wa kweli unayemhitaji.

    ReplyDelete
  10. Haya ndiyo matatizo yanayotokana na sisi waafrika kujikataa na kuanza kuuvaa uzungu. Njia zetu za asili za kupata wenza tumezitupilia mbali na kujiingiza kwenye njia za kizungu. Ukweli ni kwamba, watu waliooana kwa kukutanishwa na wazazi/walezi, ndoa zao huwa zina mafanikio zaidi kuliko wale tuliojitafutia wenyewe. Lakini kwa kuwa "elimu" inatuambia kwamba tamaduni za kiafrika zimepitwa na wakati, na wote inabidi tuwe wazungu; sasa haya ndiyo madhara yake.

    ReplyDelete
  11. nakushauri ujiunge na facebook pia, inaweza kukuwia rahisi

    ReplyDelete
  12. UNAHITAJI MAOMBI!!

    ReplyDelete
  13. ukweli nikwamba mimi nimekupenda tena sana na ninamapenzi ya dhati ya kutafuta mchumba kama wewe wa ulaya. i love uu.

    ReplyDelete
  14. Nenda kwenye social websites kama vile facebook, person.com. Badoo, tagged.com, twitter, etc., Kuna warembo kibao wanatafuta kuolewa.

    ReplyDelete
  15. Weka na picha yako kaka

    ReplyDelete
  16. Jifunze kupenda na kuheshimu wanawake, anza kujifunza wanawake wanapenda nini na ni jinsi gani unaweza kuwa na relationship nzuri. Haya mafunzo yako kwenye vitabu, Google, na kila mahali, pia uliza wenzio. watu wengi huwa tunajitumbukiza kwenye mahusiano na kuona ni magumu ni kwa sababu, hatuna elimu ya relationship na kujua tofauti ya mwanamke na mwanaume ktk mahusiano. Na pia ni vizuri kujifahamu wewe mwenyewe ni mtu wa aina gani na ujipende, kwani ukiwa na mtu mwingine ni vigumu kuanza kumjua mtu mwingine na kumpenda kama haujaanza kwako.
    Umesema umeenda shule (elimu ya kupata kazi), jua mapenzi nayo yanataka shule kabla ya kuyafanyia kazi. All the best mate

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...