Hongera kwa kazi kaka!

Nimatumaini yangu kwamba ni mzima. Ningependa kuomba msaada wako tafadhali. Jana jioni majira ya saa moja hivi nilivunjiwa kioo cha gari,pale CAROLZ BAKERY(njia ya chini mbezi kama unaelekea white sands) nakuibiwa Laptop na vitu vingine vingi vilivyokuwepo ndani ya ile laptop bag yangu,zikiwemo pesa,camera,hard disc drive etc..and unfortunately too kulikuwa na wallet yangu ambayo naweka business documents na ATM cards.

Hawa jamaa wamekomba vyote na wakachukua ATM cards (CRDB) na kwenda kuchukua hela zote kwenye account yangu,na wakatumia branch yangu,asubuhi ya leo!

sasa kama kwa bahati nzuri watasoma hii tunachowaomba nikutusaidia na Files zilizomo kwenye hiyo laptop kupitia email address,noequk@yahoo.co.uk plus kwenye hiyo hard disc kwasababu ni kazi za watu na kazi zangu za shule zote!kwaujumla ni kila kitu kwangu. Nakwayeyote atakayeokota any documents pliz contact me through

0719-905009 / 0784 903039 au viwasilishe kituo chochote cha polisi au ofisi za EASB mikocheni.

Asante kaka

Moses.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Mdau pole sana kwa yaliyokukuta na hebu tupe ufafanuzi kidogo, hizo hela kwenye account yako walizichukua vipi? I mean password ya account yako waliipata wapi? Pole sana.

    ReplyDelete
  2. Pole sana mdau. sio vibaya kuuliza wamekomba pesa zote kwenye account yako- PIN number ya kadi yako waliijuaje?

    ReplyDelete
  3. Pole sana Mdau!
    Ila kwa mwendo huu, vibaka hawataacha kuvunja magari. Kama wakivunja wanapata vyote hivyo + Kukomba pesa kwenye account!!

    ReplyDelete
  4. Aise pole sana..Ulikuwa kwenye foleni..Hiyo password wanaweza kufanya PEMUTATION NA COMBINATION plus PROBABILITIES,FACTORIALS etc lakini wakikosea mara tatu si kadi inakuwa blocked au?

    USHAURI:Siku nyingine ukiwa na 'files' muhimu kama hizo jaribu kwenda kwenye email account yako andika blank email,attach na usitume au jitumie mwenyewe..Nayo inasaidia katika hali kama hii..hata kama umesafiri nje ya nchi ukakwapuliwa Laptop,flash/hard disc..

    David V

    ReplyDelete
  5. pole sana kaka.....lakini kwanini hatujifunzi???kila siku tunaibiwa vitu ndani ya gari,kwanini hatuachi hii tabia ya kuacha laptop na vitu vingine ndani ya magari???

    ReplyDelete
  6. Nenda Kariakoo kuna kijana mmoja huwa anamawasiano na wezi wa Dar na yeye atakufanyia mpango uipate hiyo laptop, lakini itabidi ununue tena.

    ReplyDelete
  7. mdau pole sana,nenda kwa mganga ukawavimbishe vitambi hawa nyani.

    ReplyDelete
  8. Ndugu pole, ila samahani we kweli una akili? mpaka unaacha wallet kwenye gari? Ulikuwa wapi? Najua hayanihusu ulikuwa wapi ila kaka come on man! Vitu vingine tunajitakia especially hapo bongo, halafu wamewezaje kutoa hela kwenye ATM? PIN # ulliandika kwenye wallet pembeni ama?
    All in all, pole ndugu.

    ReplyDelete
  9. Pole sana ndugu yangu. Unasema wamekomba pesa zote, ni kupitia ATM au wamekula njama na mfanyakazi wa benki wakachukulia dirishani? Kama ni kwenye ATM, PIN yako waliijuaje? Kama ni dirishani basi ni rahisi sana maana teller inabidi ajulikane aliyewapa pesa ukifuatilia benki. Kama ni kwenet ATM, ATM huwa zina CCTV camera kwahiyo unaweza kuwatambua wahusika kupitia benki ukijua ni ATM ya wapi walikochukulia hizo pesa. Pole sana.

    ReplyDelete
  10. AISEE pole sana mkuu ila hata kama wamefanya factorial,probabilities na madudu yote ok at last wakapatia password inamaana ATM zetu za CRDB hawana limit ya pesa kwa siku mpaka wakung'ute zote! makubwa.

    ReplyDelete
  11. na mimi ninaungana na wadau hapo juu 1-kama uliandika PIN # yako kwenye ATM card, ni matatizo yako. 2-Kama umeacha hard drive na wallet kwenye gari, vile vile ni uzembe wako 3-kuhusu laptop kidogo inaeleweka, watu wengi huacha kwenye motokaa zao 4-next time, back up ypur documents and leave your hard drive home, ATM pin # yako ni siri yako - usiandike popote, unatakiwa kuibumbuka, na ukipoteza vitu kwa uzembe wako usimsumbue ankal Michuzi

    ReplyDelete
  12. pole sana kaka.ila kupitia atm najua kuna limitation ya kuchukua hela.labda kama ulikuwa na less than 1 million kwenye account hapo ntakuelewa.
    2.kaka sasa labda ulikuwa unafanya ubishoo maana wewe mwenyewe unaweza ukawa uliwatega makusudi maana hata kama ni gari basi weka sehemu ambayo mtu akichungulia hawezi kuviona.we unaacha mpaka wallet rafiki yangu unategemea nn?siku nyingine hard disk acha nyumbani au kwa ofisi na hakikisha inakuwa na back-ups za document muhimu.
    3.Mi mwenyewe huwa nina kabegi kangu muda wote hata kama nikishuka kwenye gari naweka vitu vile vya muhimu then nashuka navyo maana sio kuibiwa tu hata gari yaweza unguzwa au kuibiwa pia.
    4.Nadhani hii itakuwa mfano kwa watu wengine wenye tabia hii.huwezi acha hadi wallet kwenye gari wallet inakaa mfukoni bana!!

    David Muni**
    manchester!!

    ReplyDelete
  13. kwanza polee,lakin kaka moses ndio maana tunatakiwa tusome driving theory na practical bana maana tunaambiwa document muhimu usiache kwenye gari hata kidogo,tena hasa kwa hapo dar jaman kila siku story ni hizo,na hawa vibaka nao jaman wamezidi inatia uchungu poleee kakangu,sasa na hiyo kadi vp kuhusu pin wamejuaje!!!

    ReplyDelete
  14. Wataalam wanasema" follow the money" kwa kifupi nenda bank angalia records za withdrawals, muda na sehemu, request videos from that exact time, picha za jamaa lazima zitakuwepo, print, peleka polisi,tv stations na magazeti, tangaza reward kwa mtu atakayetambua sura kwenye picha, mchezo umeisha!

    ReplyDelete
  15. Mhh style hii ya kukombwa mpaka wallet kama umeibiwa na changu vile. Maana machangu wa Bongo ndio zao nini wallet kuna dada aliibiwa mpaka mtoto mchanga na changu aliyeokotwa na kaka yake, bahati mtoto alitangazwa kwa vyombo vya habari akapatikana sijui Mvomero.

    Maana haingii akilini kuacha wallet yenye pesa na kila kitu ndani ya gari, wewe umekombwa vichocoroni ulipokuwa unajivinjari. Nawajua watu waliokuwa wanaenda mpaka madanguroni saa za kazi.

    ReplyDelete
  16. Mdau hapo juu na wee unachekesha eti print peleka polisi kwani wewe unaishi TZ kweli ????? ukipeleka polisi watawasaka kweli ila ujue umewapa mradi na polisi ya kwetu mimi nilishangaa ukipeleka kesi wewe ndo unakuwa mradi wao na anayeshtakiwa vilevile hivi wewe unaishi bongo kweli?

    ReplyDelete
  17. aisee hata mimi bado hainingii akilini hilo swala la wallet!!we sema labda ulikuwa na totoz ukawa unamrudisha kwake kushuka ndo ukaacha vitu afu ukachelewa kurudi wanaume ukakuta wamevikomba!!vitu vyote hivyo kweli sijui maana hata hela unaacha kwenye gari sasa ukikanyaga nyanya njiani inakuwaje?
    sema vizuri usaidiwe bana moses!!

    david Muni**
    manchester

    ReplyDelete
  18. Anony, wa 12:41, katika option ambazo zipo, nilizoweka hapo juu za picha ndio nimeona zinaweza kumsaidia, Kama una other ideas please ziweke hapa, and no mi siko TZ kwa miaka 13 sasa, but the fact remains if dude wants to know who stole his stuff, he needs to do what I said, now Kama police is f**ked up that's not my problem, au sio bwana.

    ReplyDelete
  19. Ni kweli kabisa jamaa atakuwa amekombwa na changu aliyekuwa naye kwenye gari, si unajua mambo ya malove akajisahau
    Pole utapata vitu vingine. Hilo ni fundisho kwa midume inayotaka kufanya mambooz ndani ya gari

    Rubafu

    ReplyDelete
  20. Asanteni wote kwa maoni yenu!nimeshapata hizo picha ila sura haionekani,amechukulia kwenye ATM.Hiyo pin amecheza tu na numbers.hiyo sehemu kuna walinzi,tena wawili,mmoja walimtuma ndani,mwingine alikua anaongea na watu anasema hakuwaona,sasa kuchukua mkate tu mara moja na begi plus everything wakati kunawalinzi??anyway,kama jambo halijakukuta huwezi kuelewa.

    kaka hapo juu tafadhali naomba niambie huyo kaka yuko kariaako sehemu gani??nitainunua tu sina jinsi,nitashukuru kama nitapata feedback toka kwako tafadhali.

    ReplyDelete
  21. Mdau
    Umeleta swala lenye utata mwingi sana tena sana, binafsi nadhani taarifa uliyotoa si kamili na ndiyo maana unawaomba wakurudishie lap top, kama vile unawajua.
    Ukitaka kuendesha gari kuna maadili, ukitaka kuingia nyumba ya ibada kuna maadili, ukitaka kugombea nafasi ya uongozi kuna maadili, ukitaka kufanikiwa katika jambo lako kuna maadili. Wewe huna maadili ni kama ulikuwa ndiyo kwanza una miezi 3 na utaka kukimbia utapinda miguu hata uwekwe juani kwa mwaka mzima!
    Dunia ya leo, wenzako wameacha kutembea na lap top kama begi, lap top inakaa sehemu moja inayoaminika wewe unatembea na flash disk tu tena siku hizi zipo zenye uwezo mkubwa sana. Ikiwa unakwenda kila mahali na lap top huna maadili ya IT, waulize wataalamu wa IT watakwambia juu ya matumizi ya kibwebwezo mpakato.
    Lakini niungane na wengine ambao wanashangaa kuwa hata akaunti yako imeingiliwa kwa vile tu jamaa wamepata ATM card yako, haingii akilini lazima wewe umekosa maadili ya matumizi ya ATM Card. Kwa kifupi ni kuwa wewe ni MSHAMBA unayejifanya umeendelea , pengine sasa ndiyo utakuwa umepata somo kwa vitendo juu ya maadili.
    Kuhusu utaratibu wa Benki kutoa pesa kwa kutumia ATM card soma zile karatasi za mkataba na Benki.

    ReplyDelete
  22. Does not click in my head at all.....you look DISORGENISED....Pole anyway

    ReplyDelete
  23. Eat your own mess peacefully.....hili tukio umepigwa na changu.....lets hope ulisahau kila kitu kwenye gari lakini NYENZO iwe ilikumbukwa..........Definetly gari ulisahau kulifunga pia......Ankal usibane hii ili wengine wazijue threats behind ngono zembe......

    ReplyDelete
  24. Hey Dude!....hopefully you are trying to fool your wife here....ulipaki bakery na ukatoka bila pesa siyo?....what was your intention?....after all that bakery ina ulinzi wa kutosha na paking yake haina uwezo wa ku-accomodate gari nyingi za kuweza kumconfuse askari.....The story is not convising!

    ReplyDelete
  25. Hivi jamani kila siku tunasikia malalamiko kuwa watu wamevunjiwa vioo vya magari wameibiwa, lakini bado tunaacha vitu vyetu vya muhimu kwa magari, inaingia akilini kweli?
    Ukiniambiwa umevunjiwa umeibiwa power window na side mirror ntakupa pole but laptop, wallet, documents sijui nini ntakuweka vibao because uo ni uzembe jamani hata kama uko karibu na gari yako shuka navyo, utapungukiwa nini kwani?

    ReplyDelete
  26. AAAH HII STORY NI UTATA MTUPU HATA MIMI SIELEWI PESA ZIMECHUKULIWAJE BENKI LABDA AELEZE VINGINEVYO YAANI WATU WACHOPOE KADI WAKIMBIE WAENDE BENKI WAKACHUKUWE PESA! AAH HIYO PIN WAMEPATA WAPI! AU ULIANDIKA HUMOHUMO KWENYE WALETI YAKO? HAYO MENGINE SINA MASWALI MAANA KUIBA WATU WANAWEZA HATA KUKUIBA WE MWENYEWE WAKAENDA WAKAKUFUNGIA MAHALI WAKADAI WALIPWE ILI WAKUACHIE KWA HIYO SI KULAUMU ILA PIN AMBAYO UNATAKIWA UKAE NAYO KWENYE UBONGO WAKO, HATA HIVYO POLE KAMA STORI NI YA KWELI MAANA ISIJE IKAWA NI KUCHANGAMSHA BLOGU TUU HAPA

    ReplyDelete
  27. huyo kaibiwa guest house tena uswazi kabisa.duh!!kadi zote za benk ukikosea mara 3 huwa inamezwa wewe sema demu alikuchanganya ukampa password bila kujua akakuzidi ujanja!!!
    hata kwenye magari watu wanatembea na laptop but wanazificha vizuri bana!!
    Huyo mlinzi unaesema alitumwa ndani inawezekana kweli wakati hapo ni bakery.huyo mwingie unadai alikuwa anapigishwa story ina maana hamna watu wengine waliowaona!!!!
    We acha changa la macho hapa tumeishi mjini miaka na miaka!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...