Basi la Country Express baada ya ajali Jumapili jioni


Zaidi ya abiria 18 walikuwa wakisafiri kwa basi la kampuni ya Country Express lenye namba za usajili T 806 AVM wamejeruhiwa vibaya na kunusurika kifo baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na Lori katika eneo la kijiji cha Mnimbila, wilaya ya Lindi vijijini,  mkoani Lindi.

Ajali hiyo imetokea jioni ya leo Jumapili na  majeruhi wote wa ajali hiyo hali zao ni mbaya na wameondolewa katika hospitali ya mkoa wa Lindi na kupelekwa Hospital ya Rufaa ya Nyangao kwa matibabu zaidi. 
Picha na habari na mdau Abdulaziz Video

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Poleni sana Wahanga wote.

    Ilaq Kaka hao waandishi nyie WAKONGWE muwe mnawafundisha. Hio sio USO KWA USO bali ni kwamba WAMEPIGANA PASI.

    Usos kwa uso ingekuwa ni pande mbili za mbele kwa kila gari.
    Waandishi muwe makini jamani.

    ReplyDelete
  2. Hope insurance itafanya kazi yake,jamaa wote waliokuwa ndani ya basi wanahaki ya kushitaki kulipwa matibabu na mafao yao yote toka walipopata ajali mpaka watakapo pona .
    Wabongo hawajui haki zao ,kama ni nchi nyingine abiria wote wanafungua kesi na wakiwa na wanasheria ,tena wanasheria ktk kesi hizi huwa bure.
    Hii itakomesha uzembe wa madereva(kufungiwa leseni) na wenye mabasi kuwa waangalifu na service za magari yao na ubora wa madereva wano waajiri.

    ReplyDelete
  3. Blaza, ankali, hii sio ajali ya uso kwa uso. Hii ni kwamba basi limekwanguana na lori ubavuni

    ReplyDelete
  4. Hizi ajali hadi lini jamani?

    ReplyDelete
  5. Hivi kuna waziri anayeshughulikia wanausalama wawajibike?
    Sheria za barabarani ni muhimu kwa usalama wa wananchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...