![]() |
| Marehemu Saidi Hassan Mgoi |
Jumuiya ya watanzania ugiriki inasikitika kutangaza kifo cha mwenzetu SAIDI HASSAN MGOI (Maarufu kwa jina la CHANCE)kilichotokea hospitali ya mjini Piraeus Jumatatu 1/8/2011.
Marehemu kabla ya kuwasili ugiriki alikuwa ni mkaazi wa Tandika Dar.Hivi sasa tupo katika harakati za michango ya kutuwezesha kumsafirisha nyumbani.
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN
Kayu Ligopora
KATIBU



Poleni saaana wadau wa ugiriki kweli nyie ni mfano wa kuigwa katka watz wote waishio nje, unapotokea msiba hampitishi bakuli humu hata siku moja mna mshikamano wa ajabu, Mungu awabariki mzidi kuwa na umoja na mshikamano. wengine muige mfano huu. Dola elfu kumi tu watu wanaleta bakuli humu kweli ni aibu na wakati jamii ya watanzania huko waliko wapo wengi sana hadi unashangaa!
ReplyDeleteNimekuwa nasoma sana vifo vinavyotokea ugenini na ni kweli hawa jamaa wa ugiriki wana mfumo tofauti na wenzao maana hata mara moja sijawahi kuona wakitafuta msaada wa nje na baada ya muda unasikika wameshachangishanaa na wanamsafirisha mwenzao home.Ila natofautiana na mdau anayewalaumu wale walioomba msaada (tenga kumi za US)
ReplyDeleteNawaombea wote wa Ugiriki na wale wa Marekani Mungu awafanikishe katika jitihada zao za kuwarudisha nyumbani marehemu.Mungu awafanikishe Amen
SIO TU UGIRIKI,HATA UBATANI,BURUDA NA NCHI ZENYE WANAJESHI WA UKWELI WANAOJUA MAISHA NI NINI WANAOPISHA BAKULI NI WATOTO WALIOFUNGA MKANDA NA PESA ZA BABA ZAO,WANAOJUA NINI MAANA YA MAISHA LAZIMA AMUSAIDIE MWENZAKE...WE UNAFIKIRI MTOTO WA MAMA AMEFUNGA MKANDA TOKA KIWALANI MPAKA HEATHROW AU JFK HAJUI BEACH WATU WANAFANYAJE WE UNAFIKIRI ATAMUWAZA MWINGINE....HONGERENI WATU WA UMANGANI....NINA MENGI YA KUWACHANA WATOTO WAZURI ILA WACHA NIISHIE HAPA HAPA.
ReplyDeleteila mbona wamesema wapo katika harakati za michango ya kumsafirisha?so hata wao wanapitisha michango
ReplyDelete