![]() |
| Naibu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar Thuwaiba Kisasi |
Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Thuwaiba Kisasi amesema kuwa Biashara ya Magendo ya Karafuu ikiwa haitadhibitiwa kuna uwezekano mkubwa wa kudumaa kwa huduma za jamii.
Akizungumza na Wafanyabiashara na Wakulima wa Zao hilo katika ukumbi wa mikutano wa Umoja ni Nguvu Mkoani Pemba, Kisasi amesema kuwa huduma za Maji Safi na Salama zinahitaji Uchumi bora ili kuimarika.
Amewataka wakulima hao kuichukulia bei mpya ya Karafuu kama Motisha kutoka Serikalini kwa kuuza zao hilo katika Shirika la ZSTC.
Amesema kuwa zao la Karafuu litabakia Bado ni nguzo na Uchumi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa hivyo ni lazima wahakikishe kuwa wanauza zao hilo Serikalini.
Nae Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Pemba Bw Hemed Suleiman Ali amesema kuwa wafanyabiashara na wakulima wa zao hilo wanapaswa kulitumia zao hilo vizuri kwa maslahi yao na Taifa.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...