Kamati kuu ya CHADEMA iliyokutana mjini Dodoma inasemekana imewatimua madiwani wake watano wa Arsuaha mjini kwa tuhuma za kushirikiana na chama tawala CCM.

Madiwani hao ni Naibu Meya na Diwani wa Kimandolu, Estomih Mallah, Diwani wa Elirai, John Bayo, Diwani wa Themi, Ruben Ngowi, Diwani wa Sekei, Crispin Tarimo, Diwani wa Kaloleni, Charles Mpanda na Diwani wa Viti Maalumu, Rehema Mohamed.

Habari zilizotufikia zinasema Madiwani hao wamefukuzwa saa sita usiku wa kuamkia leo , baada ya kuitunishia misuli Kamati Kuu hiyo ya CHADEMA kwa kukataa kuhojiwa mmoja baada ya mwingine na badala yake wakataka wahojiwe kwa pamoja, la sivyo liwalo na liwe.

“Wamefukuzwa kwa kuonekana wamekula dili na CCM na kukubali mwafaka hali ambayo uongozi wa Chadema uliwashushia tuhuma madiwake wake hao kwamba wamelamba rushwa”, kimesema chanzo chetu cha habari ndani ya kikao hicho.

Madiwani hao wamekana katakata shutuma
hizo na kuomba ushahidi wa kuthibitisha hilo.

Awali Madiwani hao walisema wameamua kuingia mwafaka na CCM kwa sababu ya uchu wao wa kutaka maendeleo zaidi katika jiji la Arusha badala ya mitafaruku isiyo mwisho ambayo inayochelewesha maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. TULIOKO MBALI TUMEKUWA TUKISIKIA KWA MSHTUKO YALE YANAYOJIRI HUKO NYUMBANI BAADA YA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA. WENZETU CHAMA KIKUU CHA UPINZANI INAELEKEA LABDA WANATAMANI NCHI IBADILIKE (?) LAKINI STAILI YAO YA KUSHINIKIZA INATISHA! JAZBA, VITISHO, KUSHUTUMANA HATA WENYEWE KWA WENYEWE, UKALI, VURUGU, UVUNJAJI WA AMANI, UKOSEFU WA SUBIRA, KUTOTII SHERIA, KUTOHESHIMIANA WENYEWE KWA WENYEWE, KWA HAKIKA ORODHA NI NDEFU.
    WENYE UMRI KAMA WANGU TUNAIFAHAMU TANZANIA KUWA IMEJAA UOZO NA UVUNDO KATIKA NYANJA NYINGI TENA KWA MIAKA MINGI, LAKINI MAANA YA SIASA NI BUSARA, STAHMALA NA KUWA NA SIMILE KUWEZA KUYABAINI, KUYAKABILI NA HATIMAE KUYASAFISHA. KWA MTAZAMO WANGU, CHAMA KIKUU CHA UPINZANI KIMEKOSA YOTE HAYO.
    WALIOSEMA ROMA HAIKUJENGWA SIKU MOJA WALIKUWA NA MAANA YAO. WENZXETU HAWAELEKEI KUWA NA MTAZAMO HUO. NA MATOKEO YAKE NI HAYA TUNAYOYAONA, SASA WANAANZA KULANA NYAMA WAO KWA WAO! HAWAONI HAYA KUSHUTUMIANA KUWA WAMEKULA RUSHWA PALE WANAPOTOFAUTIIANA MIELEKEO. NINI BASI MAANA YA DEMOKRASI?
    KWA MAONI YANGU KUMSHUTUMU MWANACHAMA NA KIONGOZI WAKO KUWA AMEKULA RUSHWA NI JAMBO OVU ZAIDI KULIKO LOLOTE NDANI YA CHAMA CHA SIASA. NA INAPOFIKIA HATUA HIYO, NIONAVYO, CHAMA KAMA HICHO KIPEWE MUDA TU, SI KITAMBO MTAFARUKU MKUBWA UTAKIKUMBA NA KITACHOFUATIA NI KUSAMBARATIKA.
    NA IKIWA NI KWELI KUWA KUNA CHAMA HUKO NYUMBANI KINATOA RUSHWA KWA AJILI YA KULETA MUAFAKA, BASI HICHO NDIO CHAMA CHA KUKISHANGILIA, MAANA HIYO NDIO ASILI YA MTANZANIA, AMANI, UPENDO NA MAPATANO.
    MIMI SIPENDI HIZO SIASA NJAA ZA NYUMBANI, LAKINI HILO NALIUNGA MKONO. NIKO NA RAFIKI ZANGU HUKU WAZANZIBARI AMBAO BAADHI WALIDAI KUWA MAALIM SEIF HAMAD AMENUNULIWA ILI KUKUBALI MUAFAKA! SASA HIVI WOOOTE KIMYAAAA, KWA NINI? KWA SABABU VURUGU VISIWANI ZBAR ZIMEKWISHA NA RAIA WAMERUDISHA UPENDO ULIOPOTEZWA SABABU ZA TOFAUTI YA VYAMA!
    KWA HIYO IKIWA HUKO UKWENI ARUSHA KUNA CHAMA AU WATU WANAOTOA RUSHWA KWA NIA YA KUPATANISHA WATU, CHAMA AU WATU HAO NAWAPA TANO!! WALILOFANYA, KAMA NI KWELI, NI BAAB KUBWA. NA WENZANGU WA CHAMA KIKUU CHA UPINZANI WAJIULIZE KAMA MFARAKANO UNAOSITISHA MAENDELEO YA JAMII NDIO MBIU YA CHAMA CHAO.
    NAWASILISHA
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  2. CHADEMA hitaki mchezo. Ni sera ya fukuza fukuza mpaka kieleweke. Yyetote anayeonekana anapenda amani ni kufukuzwa! hao madiwani watano ni wahanga wa fukuza fukuza, jaziba, fujo, vita na karaha ambazo ndiyo sera za chama. CHADEMA hoyeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Mchangiaji hapo juu tunashukuru kwa maoni yako na ukweli ni kwamba una kila haki ya kutoa maoni yako ila nadhani unaweza ukawa umesahau kuzingatia maswala flan flan kwenye kutoa hayo maoni. Kwanza unawashutumu hawa jamaa wa CHADEMA kwamba hawana busara na wanafanya vurugu, nadhani hili si ukweli ukumbuke wanachokifanya hapa ni kuionesha umma jinsi gani walivyojipanga kiasi kwamba hawana mambo hayo ya kubebana kama tulivyozoea kwenye vyama vingine. Hawa jamaa ni wa kuwaunga mkono maana hata wewe uliyekuepo ukerewe nadhani unafahamu wenzetu huku mtu akiwa na kashfa lazima aondolewe kwenye chama au kampuni ama serikali na anakaa pembeni, mfano yule jamaa anaitwa Andy Coulson ilibidi aachie ngazi kisa ile ishu ya NoW. Tumechoka kuona nyumbani watu wakibebwa kwenye vyama vingine wakati kila kukicha wanashutumiwa kwenye umma kwamba si watu wazuri wamejaa skendo kibao tubadilike na kua watu tunaopenda kuwajibika kama mtu unamakosa na kashfa bac uwajibishwe sio uhamishiwe kitengo kingine; kwa hili nawaunga mkono CHADEMA. Pili ukumbuke hawa madiwani wametofautiana na CC ya CHADEMA ambayo ndio mamlaka ya juu kwenye chama sasa kama ni hivyo ni vyema wao wenyewe wangejitoa kwenye chama maana ninavyofahamu mimi kila chama duniani kinaongozwa na itikadi zake na kama mwanachama anatofautiana na itikadi za chama chake ni vyema akajiondoa kwenye chama kama vile tulivyoona mwaka 2005 Israel Ariel Sharon wakati ni waziri mkuu alihama Likud akaenda kuanzisha chama kipya Kadima, basi na hawa wangejitoa tu CHADEMA wakaenda kule wanakokubaliana na itikadi zao. Si vizuri kwa chama kuwa na watu ambao hawakubaliani na itikadi za chama, isije ikawa mambo yale yale ya CCJ nadhani hii stori unaifahamu. Mi nawaunga mkono hawa jamaa wa CHADEMA wawe na msimamo huo huo. Sasa ivi tulipofikia tunahitaji watu makini na 'serious' kama hawa, enzi za kubadilishana vitengo na kupeana likizo za malipo zimekwisha, tuache utawala wa sheria ufuatwe na itikadi za chama ndo zinamfanya mtu ama ajiunge au asijiunge na chama flan.
    NAWASILISHA.
    Mbeba boksi, Ukerewe.

    ReplyDelete
  4. Utashangaa CCM wanapiga kelele za kujivua magamba lakini siku si nyingi mtasikia wamepokea magamba yaliyovuliwa na CHADEMA.

    ReplyDelete
  5. Anony wa kwanza na wa pili jisahihisheni. Nchi hii imekuwa ikiongozwa pasipokufuata sheria ila maslahi binafsi. Tunawaunga mkono CHADEMA kwa silimia mia moja. Na mnavyowaita ni watu wa fujo bado mnajidanganya kwa sababu hatujaona fujo wanazofanya ila ni CCM inayotumia Polisi kuwavuruga ili waonekane wana fujo. Hamtudanganyi na propaganda zenu tumechoka na uovu wa ccm. Hebu angalia nini kimetokea UDA? Utashangaa kwa utawala wa ccm hakuna atakayepatikana na hatia na pesa zilishaliwa.

    ReplyDelete
  6. Jambo la ajbu hata wasomi walioko Nje ya nchi wana mawazo finyu. Anony wa kwanza na wa pili mnasikitisha sana. Mtu anapokosea kwenye chama lazima awajibishwe. Ona CCM walivyochukua muda kuwawajibisha akina nanihii. Sababu tu wana utamaduni wa kulindana. Huu ndio umeliangamiza taifa hili kama hamjui. Mpaka leo hii hakieleweki kama watavua hayo magamba au ni danganya tanzania ili tuendelee kula.

    Ila sishangai kwa sababu baadhi ya wadau wa UK tunawajua wanakotoka hapa bongo na itikadi zao. Hawazungumzi kwa maslahi ya nchi ila wanatumia propaganda kuwadhoofisha chadema ili itikadi zao zitamalaki. Hatukubali kubeba watu wasio na maslahi kwa taifa.

    ReplyDelete
  7. Nimemsoma mstari kwa mstari, neno kwa neno mtoa maoni wa kwanza kabisa katika habari hii, kwa maoni yangu wadau wengine hawakumwelewa.
    Tanzania ya leo ni ya utandawazi, na si haki kwa raia kuburuzwa na kulazimishwa kuabudu siasa ili kupata haki zao.
    nadhani ndivyo mtoa maoni alivyokuwa akijaribu kujieleza.
    Hata akasema anaunga mkono juhudi zozote za kuleta mshikamano na maelewano, hata ikibidi ziletwe kwa njia ya rushwa.
    hawa viongozi 5 wa CHADEMA ni kafara kwa kosa la kusimama upande wa wananchi, ila watoa maoni wengine wamedhani kosa lao ni ama kuiunga mkono CCM au kukisaliti chama chao.
    Binafsi nakumbuka hata huko CCM kwenyewe walikuwepo viongozi wasaliti kwa kupinga maamuzi ya chama chao ili kuwanusuru raia, wakaitwa wasaliti, wakatolewa kafara.
    Mmoja wao ni huyu Maalim Seif.
    Ila tatizo la wanasiasa ni kudhani kuwa wameyamiliki maisha ya raia, na kwamba maslahi yao ya kisiasa ni LAZIMA yaje mwanzo hata ikibidi raia wateseke. Mimi siungi mkono hilo.
    Kwani ni raia wangapi walikwenda kupiga kura?
    Hiyo CCM na CHADEMA kwa ujumla walipigiwa kura na asilimia ngapi ya watanzania wote?
    Je ni haki kwamba wale raia ambao si wanachama wa chama chochote cha siasa, au si wana CHADEMA au wana CCM wakadhalilika kwa sababu tu vyama hivyo viwili vina ugomvi wao ambao unatokana, kwa mawazo yangu, na ubinafsi na uchu wa madaraka?
    Hawa vyama vya siasa wanaishi kwa jasho la raia, yaani ruzuku zao zinatokana na kodi wanayokamuliwa raia, je raia wanapata wapi ruzuku?
    Ni asilimia ngapi ya pato la raia linatokana na mashamba, viwanda au makampuni yanayomilikiwa na CCM au CHADEMA?
    Hakuna hata asilimia moja.
    Sasa iweje tena kiongozi wa chama fulani, ambaye kimsingi ni raia pia, anapoamua kuachana na misimamo batili na ya kiharamia ya chama chake, alinganishwe na mafisadi?
    Hivi ni kweli hasa kwamba kuna watanzania wenzangu wanaweza kuiunga mkono CHADEMA kwa uamuzi huu wa kuwafukuza viongozi hawa ETI kwa kisingizio cha kukiuka maagizo ya chama chao? Ina maana hawa uraia wao na haki za raia waliowaongoza havina thamani CHADEMA inapoamua kiwazimu wazimu tu kukomoana na CCM?
    Ina maana kwamba hata wale raia walioipigia kura CHADEMA walitumika kuwa chambo tu na wala maslahi yao hayapewi nafasi hata kidogo linapokuja suala la mvutano wa kivyama?
    AMA KWELI SIASA NI MCHEZO MCHAFU, NI NAKAMA KWA MLALAHOI.
    Natamani kusikia hawa viongozi 5 wana kipi cha kusema, na kabla wafuasi wa CHADEMA au raia wengine hawajakurupuka kuwaita mafisadi au wasaliti ni bora wakasikiliza na kupima hoja zao.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  8. Hivi mnafikiri vurugu na kufuzana ndio kutajenga chama, baadhi walifaidika chini ya CCM na watoto wao ndio wengi walioko huko nje, tena wanasoma kwa gharama za serikali. Mimi nakumbuka nilikuwa na mtoto wa dada ake mheshimiwa mmoja alikuwa wizara ya elimu, akisoma katika shule ya wasichana weupe inaitwa St. Mary of the Woods, mtu mweusi ni yeye peke yake. A private expensive school paid by . huo ni mfano mmoja tu. Walidanganya hata shule walizokuwa wanaenda. Katika macadre waliokuwa wanatawala na ambao walikuwa wanashika nafasi nyingi serikali na mashirika ya umma ni wa aina fulani na wamezitumia hizo fursa kisawasawa na ndio walioimaliza hii nchi. Wengi wabeba maboksi huko nje ni watoto wa akina Mbowe na akina Slaa (Past CCM cadres) (ingawa yeye mwenyewe ni Padri HANA MTOTO???). Mbowe mwenyewe was close to Nyerere in those days. Sasa hao waliofaidi chini ya Nerere wameshajenga na kuendeleza utajiri wao wa elimu na mali walizorisi kutoka kwa wazazi wao ambao wengi ndio walioua mashirika ya umma, ndio hao hao wanabeba mabango kujenga chama kipya cha wazee wao. Msituzingue sisi ingawa CCM mimi haikunifanyia mema wala wazee wangu lakini JINI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKUMALIZA. Mfano huu ni hai CHADEMA mhhhhhhhhh????????????????.

    ReplyDelete
  9. Nyie watu wa ukerewe acheni upuuzi,tuachieni hii nchi yetu. Kama vipi mrudi muone,sio mnapiga kelele tu. Muda mwingine mnakuwa kama wapuuzi fulani hivi. Changes have & shall happen soon.

    ReplyDelete
  10. Baadhi ya wdau wa ukerewe tunawajua wengi wao wanatoka kule kwa wale jamaa waliokubuhu kwa ulalamishi. Kila kitu wanasema wanaonewa. Tunawajua baadhi yenu mna chuki binfsi kwa ajili ya ajenda zenu za siri.

    Huwezi ukasema hao madiwani wamekubali muafaka kwa ajili ya wananchi ni kwa ajili ya maslahi yao. Ni wanafiki wakubwa. Walizuiliwa na nani kutetea wananchi kabla hawajaingia kwenye huo muafaka? Warudishe basi mashamba ya BURKA yaliyouzwa kwa vigogo wakati wananchi waliomba hawakupata. Ubinafsi mkubwa umetawala nji hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...