Wakazi mamia waliohudhuria onyesho la Parapanda katika tamasha kubwa la Utamaduni la Sweden jijini Gothenburg, ambapo shangwe na chereko zilimeza uwanja huo wakati wasanii hawa alipokuwa wakiunga kazi moja baada ya nyingine.
Onesho hilo limefanyika leo jioni saa 11.30 hadi saa 12.00 juu ya alama mbele ya umati ambao uliomba kurudiwa kwa onyesho lakini kwa kweli isingewezekana kwani kuna vikundi zaidi ya 10 vinasubiri! Hili lilikuwa ni onyesho la kutambulisha onyesho kubwa la NATIGONE litakalofunguliwa rasmi hapa tarehe 8 Oktoba
Shabo Makota akicharaza gitaa
Eva Nyambe, Frank Samatwa na Amani Lukuli wakilishambulia jukwaa
Daudi Joseph akicharaza Jembe ngoma yenye asili ya Afrika Magharibi.
Eva Nyambe na wenzie wakishambulia jukwaa
Eva Nyambe akipagawisha watasha
Fujo Makaranga mtalamu wa kupiga ngoma ambaye naye yuko Sweden kikazi akimpongeza Daud Joseph wa Parapanda baada ya kazi nzuri jukwaani. Nyuma yake ni Binti wa Kiswidi ;Cameila ambaye "amewatoa" vijana wengi wa Tanzania katika fani ya ngoma na hasa za ubunifu. Anayeangalia ni Mkurugeni wa Gothernburg City Theatre Ronnie hallgren
Ronnie akimpongeza Kiongozi wa Parapanda na Mwongozaji Mwenza katika tamthiliya ya Antigone bwana Mgunga Mwa Mnyenyelwa.


Hongera sana PARAPANDA ART THEATRE hakika mmeiwakilisha Nchi yetu vizuri. Sisi wazawa hatutambui mchango wenu lakini wageni wameona pia wametambua umuhimu wenu kazeni buti ipo siku isiyokuwa na jina nanyi mtafaidi matunda ya kazi na uvumilivu wenu. Achaneni kabisa na viongozi wetu wala rushwa wasiotambua mchango wenu katika taifa hii.
ReplyDelete