Wasanii 7 na Mwongozaji mmoja wa kundi la sanaa za maonyesho wako nchini Sweden kwa ziara ya maonyesho  ya Utambaji wa mashairi na uandaaji wa  tamthiliya ya ANTIGONE. Tamthiliya hii imeandikwa miaka 42 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo, yaani  zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Mwandishi  wake ni  Yule msanii mwandishi nguli wa Kigiriki wa tamthiliya za jukwaani aliyejulikana kwa jina la  Sophocles.

Tamthiliya hii  imetafsiriwa katika lugha  zote kuu za dunia  kasoro Kiswahili na kwa mara ya kwanza itachezwa kwa Kiswahili na Kiswidi.

Maandalizi na maonyesho ya tamthiliya hii yanafanywa na taasisi mbili za sanaa za maonyesho: Parapanda Theatre Lab Trust na Gothernburg City Theatre ya Swiden, .kuanzia  tarehe 2/8/2011 mpaka 14/12/2011. Maandalizi na maonyesho yanafanyika Sweden na Tanzania.


Kwa Habari kamili na picha zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...