Kada wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Ndugu PETER KAMFUMU ameongoza kura za maoni zilizopigwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora kwa ajili ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Igunga lililoachwa wazi na Rostam Azizi (pichani)aliyejiuzulu.

Taarifa iliyotua hivi punde katika mtandao huu kutoka radio Uhuru Fm inadai kuwa Ndugu KAMFUMU ambaye pia ni Kamishna wa Nishati katika Wizara ya Nishati na Madini amepata kura 588 kati ya kura 928 zilizopigwa na Wajumbe wa Mkutano huo katika uchaguzi uliofanyika jana Mjini Igunga.

Katibu wa CCM Wilaya ya Igunga Ndugu NEEMA ADAM ameiambia Uhuru FM kwa njia ya Simu kuwa jumla ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Kumi na Tatu wamepigiwa kura za maoni katika mkutano huo.

Wanachama wengine waliopigiwa kura ni pamoja na Ndugu JAFARI ALI OMAR kura 163, SHAMSI FEROUZ IBRAHIMU kura 36, Ndugu HAMIS MAPINDA kura 36, Ndugu NGASA NIKOLAUS kura 18, Ndugu SELF HAMIS kura 13 na Ndugu SHIRE MASHAURI kura 16.
Wengine ni Ndugu HAMAD SAFARI kura 5, Ndugu MKOBA SHABAN kura 5 Ndugu DANIEL MBOJE kura 4, Ndugu ADAM KAMANI kura Tatu na Ndugu AMINA FUNDIKILA kura Saba.
Kulingana na Katibu huyo wa CCM Wilaya ya Igunga majina hayo yote yatapelekwa ngazi ya Mkoa ambayo nayo itayapitia na kisha kuyapeleka katika Kamati Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kwa maamuzi zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Peter Kamfumu ndiye atakayekuwa mbunge wetu Igunga whether cdm wanataka aua hawataki. Read,copy and paste that. MwanaIgunga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...