Mmoja kati ya washindi wa shindano la Tusker la Tusker All Stars 2011,Peter Msechu akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Nia Njema wakati akiwahamasisha umuhimu wa kuifahamu lugha ya kiingereza.
Msechu akiwa na baadhi ya walimu wa NIa Njema High School.

Na Mwandishi Wetu

MMOJA kati ya washindi wa shindano la Tusker la Tusker All Stars 2011 Mtanzania Peter Msechu amewaasa wanafunzi nchini kutilia mkazo wa kuifahamu lugha ya Kiingereza kwani inasaidia katika kupata mafanikio.

Msechu amesema hayo leo wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nia Njema iliyopo mjini Bagamoyo ambayo aliwahi kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne.

Alisema kufahamu lugha hiyo ni kitu muhimu kwani kumemsaidia kwa kiasi kikubwa kutwaa taji hilo ambalo litamuwezesha kufanya kazi na wasanii mbalimbali wakubwa duniani.

“Napenda niwaambie lugha ya kiingereza ni mkuhimu katika kusaka mafanikio ya kitu…mimi nilipokuwa nasoma hapa niliona kama mwalimu wangu ananionea baada ya kuniadhibu kutokana na kutoifahamu vema, lakini sasa nimeona hawakuwa wakikosea,”Alisema.

Aliongeza kuwa, tangu alipoanza mchakato wa kushiriki shindano hilo kwa mara ya kwanza alikutana na changamoto ya lugha hali iliyomfanya aombe msaada wa kufunzwa zaidi na walimu wake hali iliyomsaidia kuchanja mbuga.

“Asikwambie mtu kiingereza ndiyo kila kitu kwani bila hivyo ningeona aibu kujifunza na kuishia njiani…nawasihi wadogo zangu kuitilia mkazo lugha hii,”Aliongeza.

Aidha, Msechu aliwashuku walimu wa shule hiyo kwani ndiyo chachu ya mafanikio yake kutokana na shule hiyo kutilia mkazo lugha hiyo kama lugha kuu ya mawasiliano shuleni hapo.

Naye mkuu wa shule hiyo, Anthony Nyenshile alimpongeza msanii huyo kwa kukiendeleza kipaji chake sambamba na kujibidiisha hali ambayo imemfikisha hapo alipo.

“Kwa kweli kijana huyu alikuwa mchapakazi na anayependa sana sanaa…tunakupongeza kwa hatua uliyofikia hivyo tunakutakia kila lka heri katika harakati zako za kimuziki,”Alisema.

Msechu, pamoja na wenzake wawili Alfa wa Burundi na Davis wa Uganda walitwaa ushindi wa shindano hilo lililofikia tamati mwishoni mwa wiki iliyopita huko Nairobi, Kenya.

Kwa ushindi huo wasanii hao watapata fursa ya kupanda jukwaani na wasanii mbalimbali wakubwa toka nchini Marekani ambao wanatarajiwa kwenda nchini Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Michuzi niko nje kidogo ya Mada..Usisahau kutupatia matokeo ya Simba na Yanga..!!!

    David V

    ReplyDelete
  2. We nawe unatuchanganyia habari muone watu wengine hata darasani mlikuwa zirooooo.hapa tupo kwenye kumpongeza Msechu hayo ya ya mechi unatuletea ya nini???? Hongera Msechu nakuombea ufanikiwe na lazima utalitwaa taji lazmaaaaaaaaa wewe ndio mshindi wa tusker mwaka huu narudia msechu utalitwaa taji.

    ReplyDelete
  3. hongera sana Msechu, kaza buti kaka watanzania tupo nyuma yako kukusupport.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Msechu,kipaji unacho jambo la msingi ni nidhamu na kuongeza juhudi na mbwembwe katika kulishambulia jukwaa. "usiwe tozi kama Hemed,ametutia aibu sana kwa lugha chafu aliyompa judge Ian,majibu yake yalionyesha darasan zeroooooooooooooooooooooooooooooooo!!!

    ReplyDelete
  5. jamani mbona kama naachwa njia panda hii tasker last week si ilikua bado inaendelea au kwenye Television zetu ni recorded? watanzania wako busy ku-Vote jamani mimi last week niliangalia kweli walikua bado wako kwenye mchakato iweje leo nasikia eti msechu na wenzake wameshinda?
    Ofcourse Nampa shavu sana Msechu na nilifanya juhudi sana ashinde( I mean nilivooote) Kwakweli Hemed Hemed pale sijui walimpeleka kufanya nini he was just there Kufanya ubishoooo wa kipuuzi sijui nani alimwambia Mzuri he was peace of nail in our brains jamani.Muuza sura tuuuu hana lolote. Isitoshe akasema maneno ya kipuuzi kwa judge hata kama ni utani ule ulipitiliza Aangalie mwenzake Msechu alifanya utani ila alikua na adabu. Msechu you go boy! but usibweteke maana nawe umeanza kujiachiaaa unakula manyama sana mwili utashindwa kuperform.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...