Aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak  (pichani) amekana mashtaka ya rushwa na kuamuru kuuliwa kwa waandamanaji, siku ya mwanzo ya kesi yake iliyofanyika mjini Cairo.
Waandishi walisema, alipelekwa akiwa kwenye kitanda cha hospitali na kuwekwa ndani ya kizimba mahakamani humo, jambo lililowashtusha wengi waliokuwa nje.
Bw Mubarak mwenye umri wa miaka 83 anashtakiwa na watoto wake wawili wa kiume, ambao pia walikana mashtaka yanayowakabili, na pia aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Habib al-Adly na waliokuwa maafisa wengine sita.
Hukumu ya kuamuru mauaji ya waandamanaji ni adhabu ya kifo.
Takriban askari na polisi 3,000 wamezambazwa kuhakikisha kuna utulivu katika chuo cha mafunzo cha polisi ambapo kesi hiyo inasikilizwa.

Awali ilikuwa isikilizwe kwenye kituo cha mkutano cha Cairo lakini mamlaka husika zikahamisha eneo na kuunda mahakama ya muda ndani ya chuo hicho kutokana na suala la usalama.
Inakadiriwa watu 600 walitazama kesi hiyo ndani na nje ya mahakama, na mamilioni ya wengine wengi wakitazama kupitia televisheni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...