Gwaride la FFU wa Ngoma Africa band jijini Frankfurt siku ya jumamosi ilopita katika onesho la Afrika-karibik festival mjini frankfurt,Ujerumani, palikua hapatoshi ! Pata shika kubwa ilitokea baada ya washabiki kukolewa na muziki wakapandisha mzuka na kukwea jukwaani ! walinzi walizidiwa nguvu kabisa. FFU kamanda Ras Makunja akiwa katika kazi ya ziada, kibarua kipevu cha kugawa "supu ya mawe" na washabiki nao anajipendelea jukwaani. Usikose kuwasikiliza ffu at www.ngoma-africa.com
Kamanda Ras Makunja akiongoza gwaride Frankfurt
Mashabiki wakiwa wamepagawa na gwaride la FFU Ughaibuni jijini Frankfurt
Mdau hana hamu kwa uzito wa gwaride
Mashabiki wavamia jukwaa
FFU aka watoto wa mbwa,ngoma africa kazi mnaiweza tena mnatisha,lakini habari nyeti tunasikia kwamba kamanda umewekewa kali na washabiki kuwa
ReplyDeletesiku utakayosema heti muziki basi..ndio mwisho wa kuishi..pole sana kwa
kali hiyo
hole wako kamanda kama usingetokea pale ,kama ulivyokua unadai oh! nafunga swaumu kaburini ungekwenda na watoto wa mbwa nao wangekufuata
ReplyDeleteHongera wanaNgoma Africa band,juhudi zenu zinaonekana na nyinyi ndiyo mabalozi wetu huko ugaibuni kimuziki,ni vizuri na heshima kuu kuona wsanii wetu walio nje wakiwajibika na kujitahidi kutuletea habari mara kwa mara,za muziki na maendeleo yao.Wasanii wetu wengine pia mjitahidi kuwa mnatupa habari kama hawa "FFU"msijisahau sana huko majuu.
ReplyDeleteJuma Mdoe,Korogwe.
Mbona watazamaji wanaingia bure? Kuna pesa wanazolipwa lakini hawa?
ReplyDelete