Gwaride la FFU  wa Ngoma Africa band jijini  Frankfurt siku ya jumamosi ilopita katika onesho la Afrika-karibik festival mjini frankfurt,Ujerumani, palikua hapatoshi ! Pata shika kubwa ilitokea baada ya washabiki kukolewa na muziki wakapandisha mzuka na kukwea jukwaani ! walinzi walizidiwa nguvu kabisa. FFU kamanda Ras Makunja akiwa katika kazi ya ziada, kibarua kipevu cha kugawa "supu ya mawe" na washabiki nao  anajipendelea jukwaani. Usikose kuwasikiliza ffu at www.ngoma-africa.com
 Kamanda Ras Makunja akiongoza gwaride Frankfurt
 Mashabiki wakiwa wamepagawa na gwaride la FFU Ughaibuni jijini Frankfurt
 Mdau hana hamu kwa uzito wa gwaride
Mashabiki wavamia jukwaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. FFU aka watoto wa mbwa,ngoma africa kazi mnaiweza tena mnatisha,lakini habari nyeti tunasikia kwamba kamanda umewekewa kali na washabiki kuwa
    siku utakayosema heti muziki basi..ndio mwisho wa kuishi..pole sana kwa
    kali hiyo

    ReplyDelete
  2. hole wako kamanda kama usingetokea pale ,kama ulivyokua unadai oh! nafunga swaumu kaburini ungekwenda na watoto wa mbwa nao wangekufuata

    ReplyDelete
  3. Hongera wanaNgoma Africa band,juhudi zenu zinaonekana na nyinyi ndiyo mabalozi wetu huko ugaibuni kimuziki,ni vizuri na heshima kuu kuona wsanii wetu walio nje wakiwajibika na kujitahidi kutuletea habari mara kwa mara,za muziki na maendeleo yao.Wasanii wetu wengine pia mjitahidi kuwa mnatupa habari kama hawa "FFU"msijisahau sana huko majuu.
    Juma Mdoe,Korogwe.

    ReplyDelete
  4. Mbona watazamaji wanaingia bure? Kuna pesa wanazolipwa lakini hawa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...