Treni iendayo kasi barani Afrika, imeanza safari yake mpya kuelekea mji mkuu, Pretoria, kutoka Johannesburg katika jitahada za kurahisisha usafiri baina ya miji hiyo mikubwa ya Afrika Kusini. Na Maganga One
Kwa gari mwendo wa safari hiyo huchukua hadi saa mbili wakati watu wengi wakiwa wanatumia usafiri kwenda ama kurejea kazini.
Treni hiyo ijulikanayo kwa Gautrain inachukua chini ya dakika thelathini kwa safari ya umbali huo wa kilometa 54, wakati kwa gari inachukua takriban masaa mawili na ushee.
Safari ya treni hiyo ya Gautrain kwa njia ya kueleka uwanja wa ndege ilizinduliwa wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010, ambapo maelfu ya mashabiki wa soka waliitumia kusafiria.
Lakini kwa kufika Pretoria, inaonekana itatumia zaidi na wasafiri wa kawaida nchini Afrika Kusini ili kukabiliana na foleni katika barabara yenye magari mengi nchini humo.
Mamia ya watu walimiminika katika kituo cha treni cha Rosebank mjini Johannedburg tangu mapema saa kumi na moja na nusu alfajiri kuwahi treni ya kwanza iliyoelekea Pretoria.
Kulikuwa na matatizo kidogo yalijitokeza, ikiwemo matatizo ya kiufundi katika behewa moja, lakini wahandisi wamesharekebisha tatizo hilo, kwa mujibu wa maafisa wa Gautrain.
Serikali imesema lengo lake ni kuufanya usafiri wa treni ndio uti wa mgongo wa mfumo wa usafiri wa umma, kwa mujibu wa Waziri wa Usafiri, Sbu Ndebele.
Treni hiyo ya Gautrain imegharimu randi bilioni 24 sawa na dola bilioni 3 kuijenga.
Kasi ya treni hiyo ni kilometa 160 kwa saa.
Gautrain inatarajiwa kupunguza idadi ya magari katika barabara ya N1 Ben Schoeman inayounganisha Pretoria na mji wa kibiashara wa Afrika Kusini wa Johannesburg kwa asilimia 20.
Hiyo ndiyo raha ya kuwa na hao jamaa waliojaliwa miakili, japo wengine ni wabaguzi. angeachiwa rangi nyeusi peke yake hapo kusingefanyika kitu. Ujanja ungefanyika pesa zihamishiwe Uswis halafu repoti nzuuuuri kabisa inaandikwa.
ReplyDeleteKWELI AFRICA BADO TUNATAMBAA. YAANI GARI ZINATUMIA MASAA MAWILI NA USHEE KUSAFIRI UMBALI WA KILOMETA 54? HII NI KARIBU MAILI 30. WAKATI MAREKANI MWENDO MDUNDO MAIL 65 KWA SAA. YAANI HUO MWENDO WA TRENI NDIYO WENZETU WANAENDESHA MAGARI HALAFU SISI TUNAITA ETI NI MWENDO KASI.
ReplyDeleteSisi viongozi wetu(wanasiasa)sijui hela za wanachi wanazipeleka wapi..Inasikitisha kweli.."Muda wa kutanguliza Vyama mbele umekwisha"(Barack Obama)
ReplyDeleteDavid V
JAMANI KAMA HEKO TUWAPE TU WENZETU WAMEJITAHIDI KWA UPANDE FULANI KWA KWELI,SIO KAMA KULE MATAKONI KWETU MWISHO WA ULIMWENGU TANZANIA.WATU HAWANA AKILI KABISA HATA BABA YANGU HANA AKILI SHENZI KABISA.WATU WANAKAZI YA KUIBA TU.
ReplyDeleteHaya maendeleo ni kuigwa tena ni Africa na karibu na Tz,wananchi tunateseka jamani tuleteeni haya mambo
ReplyDeleteUnafikiri hiyo treni imejengewa gozi gozi? Gozi gozi watabaki kwenye vile vile vibanda vyao.
ReplyDeleteBongo ni ufisadi tu kwa kwenda mbele. Halafu tukilalamika ufisadi kwenye blog yetu hii, mheshimiwa Michuzi anazibana.
ReplyDeleteLakini hata hao South ni kwa sababu wanaishi na wadhungu. Kama ingekuwa ndio wenyewe, mwafrika ni yuleyule. Tunatanguliza ubinafsi zaidi.
siwezi kufananisha hiyo train ya south africa na haya ma train machafu ya america. hongera south africa kwa maendeleo yenu. rafiki zangu waliokwenda south africa karibuni wameniambia hiyo nchi ni nzuri sana. when it comes to infrastructure america haina lolote japokuwa ina pesa nyingi. mji kama boston na miji mingi tu barabara za downtown zimejaa pot holes na chafu. south africa is beautiful and new.
ReplyDeletehuwa nakerwa na wale wanaodai pesa za wananchi zinakwenda wapi wakati watanzania hatuna utaratibu wa kulipa hata Kodi ya nyumba, tunalilia maendeleo yatatoka wapi ikiwa tunakwepa kulipa Kodi, Afisa mzima wa serikali ana deni shirika la nyumba la mil 3 na ushei sasa shirika hilo litajiendesha vp? anatolewa vitu nje anadai hujuma jamani tuache kuitupia lawama serikali na tuwajibike. Hityo treni kwetu ni ndoto wahindi wa TRC wako wapi???
ReplyDeleteNji hii wajinga ni wengi ndio maana wako tayari wakombe pesa zote za nchi wapeleke kwenye majumba yao huku taifa likiendelea kudidimia. Wakitoka hapo wanjiona wajaaaaanja. Nyambaf zenu. Treni mtazisikia kwenye nchi za wengine. Lakini ngozi hii sijui ina laana manake hata wa nchi zingine ujinga ni ule ule. Naijeria wana mapesa meeengi toka kwenye mafuta lakini hawana usafiri kama huo na wananchi ni maskini. Wanachojivunia ni kutapeli watu kwenye internet. Mmmmmmh ngozi hii jamani.......!!?
ReplyDelete