Mkuu wa Mfuko wa kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania
"Vodacom Foundation"Yessaya Mwakifulefule
 Katika kuendeleza utamaduni wa kujali makundi mbalimbali ya kijamii nchini mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni ya mawasiliano Vodacom Tanzania" Vodacom Foundation" unazindua rasmi kampeni yake ya share and care kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramdhani.

Kampeni hiyo ambayo ni utamaduni wa kila mwaka wa kampuni hiyo kupitia kitengo chake caha"Vodacom Foundation" hufanywa nyakati za siku kuu kubwa za kidini ikiwemo Ramadhani na Krisimasi ambapo makundi mbalimbali ya kijamii yasiyojiweza hupatiwa chakula na vitu vingine mbalimbali ili kuwafanya kuwa wenye furaha na kuwapunguzia upweke.



"Mwaka huu Ramadhani share and care  inazinduliwa Mafia Jumamosi Agosti 6, 2011 ambapo kama ilivyo desturi itakuwa na fursa ya kupata futari pamoja na watoto yatima na wazee wasio na uwezo hususan wajane na baada ya hapo tutaendelea na kampeni hii katika mikoa mbalimbali nchini"Alisema Mkuu wa Mfuko huo Bw.Yessaya Mwakifulefule.


Vodacom Foundation itatumia kiasi cha shilingi milioni hamsini kuwafikia waislamu kwenye maeneo mbalimbali kwa lengo la kuwafuturisha na kuwapatia sadaka ya vyakula.Azma ya Vodacom Foundation kufuturisha makundi yenye uhitaji maalum ni kuwafanya kuwa na furaha wakati huu wa mwezi mtukufu na kufurahia ibada ya swaumu na pia hulenga kuwaweka pamoja wanajamii wa makundi hayo na kuwafanya kuwa kitu kimoja huku ikiwapa fursa ya kujenga undugu miongoni mwao.


"Tumekuwa tukifanya hivi tangu mwaka 2007 na tunafurahia kuwa na kampeni ya aina hii ambayo ni ya kipekee kwa makampuni hapa nchini ni sehemu ya kuonesha utu na kujali kwetu kwa vitendo kila mmoja tunamjali kwa wakati wake hii ikimaanisha wakristo wakati wa Krismasi na waislamu kwa Ramadhani, tunadhani ni jambo jema na tunajivunia"Aliongeza Mwakifulefule.


 Mbali na kupata futari kwa pamoja  Vodacom Foundation hutumia wakati  wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kutoa sadaka ya vyakula na vitu mbalimbali kwa vituo vya watoto yatima na kwa makundi mengine ya wasiojiweza wakiwemo wajane na wazee.


Baada ya uzinduzi wa Mafia kampeni hiyo itagusa mikoa ya Arusha,Mwanza na Pemba na inatarajiwa kutoa faraja kubwa kwa waumini wa kiislamu wasiojiweza katika maeneo yatakayoguswa na kampeni hiyo ambao kwa sasa wanatekeleza ibada ya swaumu.Waumini wa kiislamu nchini wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Agosti Mosi mwaka huu.Uongozi na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania unawatakia kheri na fanaka tele katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...