Baadhi ya Washiriki wa semina ya wabunge kuhusu madawa ya kulevya wakitazama baadhi ya madawa hayo wakati wa semina hiyo, kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kama wanagombe dawa vile? Mkuu wanagawiwa au?

    ReplyDelete
  2. Tatizo la dawa za kulevya ni tatizo la ulimwengu mzima na ni tatizo la kijamii ambalo linasababiswa na elimu,kukosa kazi,malezp yasio mazuri nk.Nchi kama Saudi Arabia,Malaysia n.k ni siku nyingi sana wananyonga wahalifu wa madawa ya kulevya lakini mpaka leo tatizo hili ni kubwa na linazidi.Tukikimbilia adhabu ya kifo bila kujua tatizo la chanzo ni bure.Tuna matatizo makubwa sana ya wizi wa mali za umma,watu wanakufa kwenye mahospitali kwa vile hawana pesa za kuhonga madaktari,wananchi wanakamatwa na polisi ili walipe rushwa,mahakama zinafunga watu ambao hawana uwezo kifedha n.k.Je Ditopile alikuwa anatumia dawa za kulevya?Wezi wa EPA wanatumia dawa za kulevya.Tatizo hili ni rahisi kama tutatafuta sababu zake kwani hata ikiwa ni adhabu ya kifo mwendesha mashataka na mahakama zitahongwa na watu wataaciwa

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu unaelewa fika tatizo linalotukumba. Kuwa na irresponsible governments ndo kunasababisha biashara haramu kama hizi zinashamiri. Kwani wauza madawa ya kulevya watamuuzia nani kama hakun soko. Ni suala la Demand firs then supply...!! Demand ikuwa low na supply itashuka tu. Sasa demand inasababishwa na matumizi mabaya ya fedha na mali za umma kinachopelekea watu kukosa cha kufanya. Kwani muuza madawa ya kulevya na mwizi wa mali za umma wana tofauti gani? Hao hao wabunge wanaojifanya kushangaa madawa ndo wakwanza kuomba waongezewe kipato bungeni wakati wananchi wao wanateketea. Just focus on the real issues....corruption...!!

    ReplyDelete
  4. Mimi naona wote anony wa kwanza na wa pili wote mko sawa. Hamjatofautiana sana. Nchi yetu mnaijua fika kwa hiyo hata wakiwanyonga itakuwa kazi bure.

    Chukulia mfano mzuri tu. Ni ufisadi kiasi gani umefanywa na wakubwa wetu? Lakini ni wangapi mapaka sasa hivi wamefungwa kwa makosa ya ufisadi? mbinu wanazozitumia kukwepa kufungwa pindi wanapofanya ufisadi ndio hizohizo watakazotumia pindi watu wao wanaposhikwa na madawa ya kulevya.

    Jela zetu zimejaa vibaka, walionajisi au kubaka. Waliofanya uharibifu wa mali za umma kama mali asili, waliofisadi nchi na waliongia mikataba mibovu wako huru barabarani wanaendelea kula kiulaini walivyoiba. Hii ndiyo danganyika bwana!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...