Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi, Zanzibar
Polisi Visiwani Zanzibar wamekamata Shehena kubwa ya Pembe za ndovu katika Bandari ya Malindi Visiwani hapa.
Hii ni Shehena kubwa ya kwanza kukamatwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba ambapo Polisi walifanikiwa kuigundua baada ya taarifa za Kiintelijensia zilizofanyiwa kazi kitaalam.
Shehena hiyo ya Vipusa ilikuwa imepakiwa katika makontena mawili huku kukiwa na shehena ya samaki aina ya dagaa wa maji baridi.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na Mamlaka husika, zinadai kuwa Shehena hiyo ya Pembe za Ndovu ilikuwa ikipelekwa nchini Malaysia.Hadi saa 1:00 usiku Polisi walikuwa wakiendelea na kazi ya upakuaji na upekuzi zaidi katika eneo la Bandari ambapo kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi Bandarini, Martin Lissu watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi.
Watu waliokamatwa ni pamoja na Wakala wa mizigo ambaye Polisi wamesema ni mapema mno kumtaja kwa sababu za kiupelelezi



Itakuwa ni za nanahii
ReplyDelete