Mwenyekiti wa timu ya simba aliyevaa tisheti nyekundu Godrefy Nyange Kaburu akiwa amewatembelea mashabiki wa timu ya Yanga waliouthuria Tamasha la Simba uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha na wakibadilishana mawazo
Makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu akiongea na wana Yanga
Mshabiki wa timu ya yanga aliyetambulika kwa jina moja la Rama Yanga akiwa amekwidwa na washabiki wa timu ya Simba kwa kuingia kwenye tamasha la simba na kukaa upande wa wana Msimbazi akiwa na jezi ya Yanga
Mashabiki wa Simba toka Dar es salaam wakiwa wanashangilia mara baada ya timu yao kuingia uwanjani
mashabiki wakishangilia kwa nguvu
Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi akiwa na Makamu Mwenyekiti wa timu ya simba Godfrey Nyange Kaburu wakitambulisha jezi mpya ambayo timu hiyo itaitumia katika msimu wa ligi ujao
Mgeni rasmi wa tamasha hilo ambaye ni mkurugenzi wa Tanapa Bw. Allan Kijazi akiwa anasalimiana na wachezaji wa timu ya Victors wa Uganda wakati akikagua timu. Katika mchezo huo Victors iliifunga Simba bao 1-0 kwa njia ya penati.
Picha zote na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii
Picha zote na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii
kwa kweli unajua kila siku huwa tunasema Simba akili zao kama sisimizi watu wanabisha. Huyu wanayemsukuma na kumpiga walitakiwa wampe hongera na wamsifu kwa kuonyesha kuwa ni mwanamichezo. kalipa kiingilio ili kuwaunga mkono watani zake na kujumuika pamoja kama mwanamichezo. lakini la kushangaza wanampa kichapo. kama sio ujinga na ushamba ni nini?! kwani siku ile walisema/walitoa tamko kuwa ni kwa ajili ya Wanasimba tu?! maana kwa mujibu wa matangazo waliyoyatoa ni kwamba watu wote tulikuwa tumealikwa na tena kwa kiingilio.
ReplyDeleteSIMBA ACHENI USHAMBA!