Meneja Biashara wa Mafuta ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati(EWURA),Mhandisi Godwin Samwel, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli, dizeli na taa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta hao katika soko la dunia pamoja na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania kulinganisha na dola za Kimarekani.Kulia ni Titus Kaguo ambaye ni Ofisa Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa EWURA. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA.
Kupata bei hizo kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Bongo kwa usanii si mchezo. Wiki hii iliokwisha mlituambia kuna stock ya siku 38, hata wiki haikufika mnaleta stori za kupanda bei ya mafuta sasa hio stock iliokuwa ishanunuliwa imeishia wapi? Yaani mazungumzo yenu na wafanya biashara yamewashinda ndio mmewakubalia kurudisha bei ya zamani sio??Sasa nyinyi muwafungie au msiwafungie mimi nitanunua mafuta kwa wale walioniuzia mafuta wakati wa mgomo tu na nawaasa watanzania wenzangu wafanye hivyo hivyo. BP hutaniona tenaa hata kama mtaani watachakachua mafuta.

    ReplyDelete
  2. MDAU WA KWANZA NI KWELI KABISA UNACHOSEMA, WALE WA KWANZA NDIO WENYE UPENDO WA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  3. UKISIKIA KUPELEKWA PUTA NDIO HUKU. UKISIKIA SERIKALI ISIYOKUWA NA MENO NDIO KAMA HII. TABU TULIZOZIPATA KWA HUU USANII HAINA MAANA KABISA. IMESAIDIA NINI HII KUSHUSHA BEI WIKI MOJA NA KUPANDISHA TENA. TUMECHOKA. HII MAMLAKA HAINA KAZI BADALA YAKE INAIVURUGA NCHI. TENA NI HATARAI SANA MAANA KIDOGO TU NCHI INGEWEZA KUINGIA KWENYE VURUGU AU MGOGORO MKUBWA SANA KWA SABABU YA MAMLAKA INAYOONGOZWA NA WATU AMBAO HAWANA VISION. NINGESHAURI MANAGEMENT YOTE IPIGWE CHINI, KWANZA NAWASIWASI WAMSHAJIKITA KWENYE RUSHWA. KWA UFANISI MANAGEMENT KAMA HII INATAKIWA IBADILISHWE MARA KWA MARA MAANA NI RAHISI KUTWEKWA NA WAFANYA BIASHARA.

    ReplyDelete
  4. TATIZO SIO EWURA BALI NI VIONGOZI WA JUU AMBAO WANA PERCENT ZAO KWENYE MAKAMPUNI YA MAFUTA WAMEPIGWA MKWALA HAKUNA TENA 10% WAMENYWEA LAZIMA WARUDISHE BEI YA ZAMANI MAMBO YAENDELEE HAWA WATU WANAMUANGUSHA SANA MHESHIMIWA SANA MR JK MWISHO WAO UTAFIKA TU WATALIA NA KUSAGA MENO MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  5. EWURAAAAAAA, Habari zenyu bwana. Usanii mtupu. Si mseme tu mlichemka. But no problem. Tutafika tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...