TAARIFA KWA UMMA
MAELEZO KUHUSU MAKALA ILIYOTOLEWA NA GAZETI LA MWANANCHI KUHUSU UBOVU WA MAJENGO UDOM TAREHE 12 AGOSTI 2011

Gazeti la Mwananchi la tarehe 12 Agosti 2011 ukurasa wa 8 liliandika makala kuhusu Chuo Kikuu cha Dodoma yenye kichwa cha habari:Ubovu wa Majengo UDOM; tatizo linalohitaji kumulikwa haraka na mwandishi Habel Chidawali.

Katika makala hii kuna mambo ambayo hayakuwekwa sawa na mwandishi.Chuo kinapenda kuyaweka sawa ifuatavyo;

1.Mwandishi ameeleza kuwa uongozi wa Chuo unaficha habari na hasa zile zinazoonekana kukosoa.Jambo hili tunalikanusha kwa dhati kwani Makamu Mkuu wa Chuo amekuwa mstari wa mbele katika kuwapa habari waandishi na pia amekuwa akiwasisitiza kuwasiliana nae muda wowote wanapotaka kujua jambo lolote.Sio hivyo tu bali amewapatia waandishi fursa ya kutembelea majengo ya Chuo wakati wowote ili kujiridhisha.

2.Suala la ubovu wa majengo ambalo mwandishi alieleza kwamba majengo yanavuja.Chuo Kikuu cha Dodoma kina vyuo sita na tayari vyuo vinne vina majengo yake.Mwandishi hakuweka bayana ni majengo yapi aliyoyaelezea kwamba yanavuja.Tunapenda kuuhakikishia umma wa watanzania kuwa sio kweli kwamba majengo ya UDOM yanavuja.Mwandishi alichokiita kuvuja kwa majengo ni mtiririko wa maji yaliyopo kwenye matenki juu yanapojaa.

3.Jambo lililozungumziwa na mwandishi kwamba Makamu Mkuu wa Chuo aliwaeleza viongozi wa serikali waliokitembelea Chuo tarehe 16 Aprili 2011 kuwa Uongozi unatumia muda ambao wanafunzi wanakuwa likizo kufanya ukarabati mdogo mdogo ni jambo la kawaida kwa majengo mapya kwani majengo mengi bado yapo kwenye “defect liability period” hivyo basi kufanyiwa ukarabati mdogo mdogo mara tu yanapoonekana kuwa na tatizo. Naomba kuweka bayana zaidi hili kwamba ni ukarabati mdogo mdogo ambao uko ndani ya “defect liability period”.

4.Makala pia ilielezea kwamba Mifuko ya hifadhi ya jamii iliyojenga Chuo haina mkataba maalum waliyowekeana na Chuo na akatupa lawama kwa uongozi wa Chuo kwa kutofanya hivyo.Ukweli ni kwamba Serikali kupitia wizara ya fedha ndio wenye mamlaka ya kuingia mikataba na Mifuko husika .
5.Kuhusu kudhulumiwa kwa fedha za wafanyakazi kama ilivyoeleza makala ni kwamba kama mwandishi alikuwa anafuatilia vizuri suala hilo, serikali kupitia mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali alifanya ukaguzi wa hesabu za Chuo na hakukuwa na taarifa za mfanyakazi yoyote aliyedhulumiwa fedha yake na uongozi wa Chuo.

6.Mwanchishi pia alihitimisha makala yake kwa kueleza kuwa Chuo kimekuwa uwanja wa mazoezi kwa polisi.Ukweli ni kwamba Uongozi wa Chuo hauwezi kukaa kimya wanapoona hali ya amani na usalama wa mali za umma unatetereka.Hali hii inapotokea kunakuwa na ulazima wa kuwasiliana na vyombo husika ili kurudisha amani.

Tafadhali naomba kupitia gazet lako uweke sawa taarifa hii kwa ajili ya maslahi ya jamii
Nakala kwa:Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo

IMETOLEWA NA BEATRICE BALTAZARY
AFISA MAHUSIANO
CHUO KIKUU CHA DODOMA
14 AGOSTI, 2011
Simu ya mezani: 26 2310171
Simu ya mkononi:0767 694999

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Msijitetee pale penye mapungufu ni lazima yasemwe. Mwandishi hawezi akaandika tu jambo kwa kufikiria toka kichwani mwake ni lazima kuna walioona mapungufu hayo. Tatizo la viongozi wetu hasa ambao bado wapo kwenye mfumo wa ki-ccm-ccm bado wana fikra kwamba hawakosei na hivyo wanpokosolewa huanza kujitetea na kuweka chuki dhidi ya waliowakosoa.

    Napenda kuwaomba viongozi wetu kuwa hii ni zama nyingine ya utawala. Usipokubali kukosolewa hutawajibika hata siku moja na ndio maana nchi inazidi kudidimia kila kukicha.

    Namba mbili hapo juu umejitetea kuwa kuna maji yanatiririka toka kwenye matanki pindi yakijaa. Je huoni kwamba kuruhusu maji kumwagika ovyo ni kupoteza rasilimali adimu hapo Dom? Hamuwezi mkafunga kitu cha kukata maji pindi matanki yanapojaa?

    ReplyDelete
  2. HOJA YA CHUO KUHUSIANA NA MFANYAKAZI AU WAFANYAKAZI KUDHULUMIWA HAIJAJIBIWA KIKAMILIFU KWANI KUWEPO AU KUTOKUWEPO TUHUMA KAMA HIYO HAKUWEZI KUWA REVEALED NA AUDTOR WA AINA YOYOTE , HATA MR UTTOH Mwenyewe. Hizo ni taarifa zinazotolewa na wafanyakazi wenyewe, na wanayo haki ya kuzidai kwa uongozi wa chuo au wizara mama wakati wowote. Kma Uongozi una hakika haudaiwi then nikusema hivyo tuu bila kuihusisha Audit report.

    Retired Accountant/UDITOR

    ReplyDelete
  3. Ndio maana nalipenda gazeti hili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...