TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DAR ES SALAAM AGOSTI 29, 2011.
1. KATIKA KUHAKIKISHA KWAMBA AMANI, USALAMA NA UTULIVU VINADUMISHWA HAPA NCHINI, NA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA SIKUKUU YA IDD EL FITRI INAYOTARAJIWA KUAZIMISHWA TAREHE 30-31/08/2011, JESHI LA POLISI NCHINI LINAPENDA KUTOA TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE KUSHEREKEA SIKUKUU HII PASIPO VITENDO AMA VIASHIRIA VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA SHERIA.
2. WANANCHI WENYE IMANI YA KIISLAM NA HATA MADHEHEBU MENGINE HUTUMIA MUDA HUO KWENDA KUABUDU NA KUFANYA MUENDELEZO WA SHEREHE HIZO KWENYE MAENEO MBALIMBALI YA STAREHE. HATA HIVYO, UZOEFU UNAONYESHA KUWA BAADHI YA WATU HUTUMIA KIPINDI HICHO CHA SIKUKUU KUFANYA MATUKIO YA UHALIFU KUTOKANA NA MIKUSANYIKO HIYO YA WATU.
3. KATIKA KUTEKEREZA KAMPENI YA UTII WA SHERIA BILA KUSHURUTISHWA KWA VITENDO, WANANCHI WOTE WANAOMBWA KUZINGATIA KANUNI, TARATIBU NA SHERIA MBALIMBALI ZA NCHI ILI KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UHALIFU.
4. TUNATOA TAHADHARI KWA WANANCHI, KWAMBA, WATOKAPO KWENYE MAKAZI YAO WASIACHE NYUMBA WAZI AMA WATOE TAARIFA KWA MAJIRANI ZAO PALE ITAKAPOBIDI. NA ENDAPO WATAMTILIA MASHAKA MTU/WATU WASIOWAFAHAMU WASIKAE KIMYA BALI WATOE TAARIFA KWA JESHI LA POLISI ILI HATUA STAHIKI ZIWEZE KUCHUKULIWA HARAKA.
5. AIDHA, TUNAPENDA KUWATAHADHARISHA WALE WOTE AMBAO WATAKUWA WAKITUMIA BARABARA, WAENDESHA PIKIPIKI, WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI, MADEREVA KUEPUKA KWENDA MWENDO KASI, KUJAZA ABIRIA KUPITA KIASI AMA KUTUMIA VILEVI WAWAPO KAZINI.
6. KATIKA KUHAKIKISHA USALAMA KWENYE KUMBI ZA STAREHE, WAMILIKI WA KUMBI HIZO WANATAHADHARISHWA KUZINGATIA UHALALI NA MATUMIZI YA KUMBI ZAO KATIKA UINGIZAJI WA WATU KULINGANA NA UWEZO WA KUMBI HIZO, UZOEFU UNAONYESHA WENGI HUENDEKEZA TAMAA YA FEDHA KWA KUJAZA WATU KUPITA KIASI.
VILEVILE, WAZAZI WAWE MAKINI NA WATOTO WADOGO, WASITEMBEE BILA UANGALIZI WA KUTOSHA, ILI KUEPUKA AJALI NA MATUKIO MENGINE YANAYOWEZA KUSABABISHA MADHARA JUU YAO.
7. KATIKA KUHAKIKISHA KWAMBA WANANCHI KOTE NCHINI WANASHEREKEA SIKUKUU HII KWA AMANI NA UTULIVU, JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA KIKAMILIFU. ULINZI UMEIMARISHWA BARABARA ZOTE, KWENYE MAENEO YOTE YA KUABUDIA, DORIA MAALUM MAENEO YA FUKWE ZA BAHARI, SEHEMU ZA STAREHE NA MAENEO MENGINE YOTE AMBAYO YATAKUWA NA MIKUSANYIKO MIKUBWA YA WATU.
8. JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WADAU WOTE WA USALAMA YAKIWEMO MAKAMPUNI BINAFSI YA ULINZI, VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUHAKIKISHA KWAMBA HAKUNA VITENDO VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA SHERIA VITAKAVYOJITOKEZA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA KUELEKEA SIKUKUU, WAKATI WA SIKUKUU NA HATA BAADA YA SIKUKUU. KWA TAARIFA ZA UHALIFU WANANCHI WATUMIE NAMBA YA SIMU 188.
9. JESHI LA POLISI HALITAWAJIBIKA KUMWONEA HURUMA AMA UPENDELEO MTU YEYOTE ATAKAYEKWENDA KINYUME NA SHERIA, NI VYEMA WATU WOTE WAKAZINGATIA UTII WA SHERIA BILA KUSHURUTISHWA KAMA MSINGI WA MAENDELEO YANAYOZINGATIA USALAMA, AMANI NA UTULIVU.
TUNAWATAKIA WATANZANIA WOTE KHERI YA SIKUKUU YA EID EL FITRI.
Imetolewa na:-
Advera Senso–ASP (0783 260334)
Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini
KNY: INSPEKTA JENERALI WA POLISI
Hii ilitakiwa kuwa "taarifa kwa Umma" na si kwa vyombio vya habari
ReplyDeletena wewe mdau hapo juu umechapia pia badala ya vyombo umeandika (vyombio) sasa nani amkosoe mwenzie ?
ReplyDeletesorry...ni typo error. Ila substance iko pale pale. nashukuru kwa kunirekebisha.
ReplyDelete