Kwa sisi tunaofunga na tunaishi nchi za Kaskazini (Norway, Sweden, Denmark, Finland, Iceland, visiwa vya Faeroe, Greenland) tuko kwenye majira ya Kiangazi na huku majira haya mchana ni mrefu na usiku ni mfupi!
Kuraani Tukufu inasema : Baada ya kuyakinisha jua limetua, waliofunga ni lazima juu yao kufuturu (tafsiri ya Sheikh Said Mussa kwenye kitabu chake cha Kiswahili: Saumu na shuruti zake, uk.16). Hii ina maana tunatakiwa kufunga mpaka tutapoona jua limezama! Kipindi hiki huku, kwa hapa Oslo nilipo jua linazama kwenye saa 3 na nusu hadi nne za usiku saa za ulaya ya kati (Saa 4 na nusu hadi tano za usiku za Afrika Mashariki).
Kwa wale wanaoishi kaskazini ya Norway, ndio usiseme. Jua linazama kwenye saa 5 hadi 6 za usiku za ulaya ya kati (CET = Central European Time) au saa 6 hadi 7 za usiku za Afrika Mashariki (EAT = East African Time). Mwisho wa kula daku huku, ni kwenye saa 9 na dakika 25 za alfajiri au saa 10 na dakika 25 za alfajiri za Afrika Mashariki. Huku Kaskazi ya dunia tumeanza kufunga kwa masaa 18 badala ya masaa 13 ya Makka (kuchwa na kucha kwa jua): Ni masaa mengi.
Kadri siku zinavyoenda, jua taratibu linawahi kuzama na linachelewa kutoka. Lakini mpaka mwezi wa Ramadhani ukiisha, bado mchana utakuwa mrefu ukilinganisha na usiku.
Waislamu tunaofunga huku tumekuwa tunajiuliza maswali kadhaa wa kadhaa juu ya nyakati za majira ya Kiangazi yalivyo huku kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ukilinganisha na nchi Afrika, Asia, Mashariki ya Kati, Marekani ya Kusini na Kaskazini. Wanatheolojia na wanazuoni wa Kiislam huku wameshindwa kutoa majibu ya ufasaha juu ya majira ya Kiangazi huku (mchana mrefu usiku mfupi) na muda wa kufunga na kula daku. Wanahitilafiana sana.
Imam Senaid Kobilica, Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislam Norway (IRN = Islam Råd Norge) amesema juzi kuwa; wataitisha kikao cha Mashehe na Maimam baada ya Ramadhani kwisha ili kujadili utata uliojitokeza wa suala hili. Imam Kobilica anakubaliana na Imam Basim Ghozlan wa msikiti wa Rabita hapa Oslo kuwa watu wanaweza kufuata masaaa 13,5 ya kufunga ya Makka. Wakati Imam Syed Nehmat Shah wa msikiti wa Central Jamaat-e Ahl-e Sunnat na Imam Hafiz Mehboob ur Rehman wa Islamic Cultural Centre hapa Oslo wanasema kuwa lazima waumini wa Kiislam wafuate masaa yaliyoandikwa kwenye Kuraani Tukufu; Kucha na kuchwa kwa jua!
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwakani utaangukia Julai. Na huku hizi nchi za Kaskazini Julai ni katikati ya Kiangazi! Jua linapotea kama saa moja sana sana masaa mawili. Je, itakuwaje kwa wale watakaojaliwa kuufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani?
Manaake itabidi wafunge kama masaa 23 hivi. Kwa wale waishio kuvuka nyuzi za Actic wao itabidi wasifunge, kwani jua huwa halizami kabisa!!!
Watu mpaka tumefikia kusema kuwa: Wakati dini ya Kislamu inaanza watu waliokuwa wanaishi enzi hizo hawakujua kama kuna nchi huku kaskazini zilizo na majira ambayo ni tofauti na yale yaliyoko huko kulikoanzia Uislam na matokeo yake ndo utata huu tulionao kama kwenye mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu. Wangejua kuwa huku wakati wa majira ya theluji kukoje na wakati wa majira kiangazi kukoje, labda utata huu usingekuwepo.
Ijumaa kareem!
Mdau Ughaibuni
Mdau pole sana, Uislam ni kufuata Quran na hadith sahihi za Mtume (SAW). Sheria ya kufunga inasema jua kutoka na juma kutua. Masaa kweli ni mengi lakini ndio sheria. Kuna Islam TV ambako sheikh mmoja aliulizwa swala hili kuhusu Alaska, akajibu kuwa utaangalia nchi jirani saa zao za kufutari na kula daku. Lakini mdau logic yako haikubaliki maana kuna watu somali sasa hawali kwa siku tatu, je wao vipi? Maana ya Ramadhani ni kumfundisha binadamu kujua njaa maana kuna watu hawajui njaa ndio nini hususan watu hao wa kaskazini ya dunia. Mawazo yangu ni kuwa watu wa kaskazini wanauwezo wa kufunga masaa 48 mfululizo maana wako fit kinoma.
ReplyDeleteni kweli kabisa maneno yako maana utata huo upo takribani nchi zote za ulaya kwa mfano sisi hapa Holland tunafunga masaa 19 kutokana na juwa kuzama saa tatu na nusu mpaka saa nne, na sasa hatujui mwakani itakuaje maana ramadhan ya mwakani itakuwa katikati ya summer ambapo juwa litategemewa kuzama saa tano za usiku.
ReplyDeletemdau nakubaliana na wewe yaani unafunga for almost 20 hrs na ikifika midsummer wa finland jua linazaa kwa lisaa limmoja je hapo watu wanafungua vipi wale daku vipi waswali taraweh vipi cant wait for this time.
ReplyDeleteallahuyaalam tusubirini tujionee
Yaani wewe mdau inaelekea huijui dini yako. Yaani unaposema hapo awali watu hawakujua kama kuna hali hiyo Kaskazini mwa dunia unamaanisha Mwneyezi Mungu aliposema hivyo alikuwa hajui au, sasa kama alikua hajui nani alieumba sehemu hiyo.
ReplyDeleteulieandika habari hii kumbuka Ramadhani zilizopita nyingi zilikuwa kwenye winter!!Je hukulalamika???mbona muda ulikuwa ni mdogo mno sawa na masaa matatu tu.....au ulifuata time za Tanzania? fuata jua linapozama ok.
ReplyDeleteTakk.. Norway
Jamani hii kitu sio utani ni kuhabarishana na kufumbuana macho.Kwa sisi tuliopo North ya Norway wakati wa summer usiku inakuwa hakuna yaani kuanzia june mpaka sept hii ramadhan tu ni kiboko.ya mwakani ndo itakuwa moto kwani ni kipindi ambacho jua ni masaa 24,sasa hapo ni Quran gani ifuatwe.kwa kuwa kutakuwa hakuna kutoka kwa jua wala kuzama kwa jua basi haina haja ya kufunga,na kama kuna fufunga basi tunafunga ili tufe kwa njaa.Ni bora itambulike kwa waisilamu wote kuwa kufunga ramadhan ni siku 30 na kufunga ni masaa 13 kuto jali ni nchi gani unaishi.kama vile waislam wanapofunga bila kujali ni nchi gani wanaishi.Twende na mabadiliko kidogo zamani koran tulijifunza madrasa na sasa tunajifunza ktk internet na mambo yanakuwa mswanu tu.Ramadhan kareem wadau
ReplyDeletewewe kama hujui usemacho hebu nyamaza ..alieleta SWAUM ndio alieumba dunia kwa hio acha ujinga.kwa kujiona unajua masaa .. wewe ni mgeni tu hapo ulipo.sio kwenu hapo na hio sio nchi ya kiislam ikifika wakati unaona ngumu rudi kwenu ukafunge.
ReplyDeletepole ndugu yangu inaonekana wewe ni muislam jina tu.....
ReplyDeleteMDAU NORWAY
Asalaam aleykum
ReplyDeletesisi London alfajr inaingia saa 8 na nusu usiku na tunafungua saa 9 usiku ndio jua lazama (kadri siku zinavyozidi kwend time zinabadilika)
majibu ya maswali yako ni simple sana kwani linajibika ukizingatia maeneo kama Alaska Jua sasa hivi lawaka kwa masaa 23!
1. Mnaruhusiwa kutuata nchi ya jirani ambayo mnatumia same time zones
2. Mnaruhusiwa kutumia time ya Makkah kufunga na kuftari
to be honest sina majibu marefu zaidi ila swali hili liliulizwa hapa na kuna jamaa walijaribu kulia address
http://www.wazalendoforums.com/forumdisplay.php?f=18
Msikufuru mkataka kuibadilisha Qurán.
ReplyDeleteQurán inasema tufunge jua linapochomoza mpaka linapozama.Nyie mnaopiga kelele kuhusu mchana mrefu mbona hamlalamiki wakati wa winter mnapofunga kwa masaa machache tu?, kwani winter mchana ni mfupi sana na usiku ni mrefu na humsikii mtu kulalamika.
Kumbukeni ni dhambi kubwa sana kuibadilisha Qurán.
Hao mashekhe wa norway wanaotaka kubadilisha sheria ya Qurán ni makafiri wakubwa wanaopotoa watu wakufuru.
Ramadhan Kareem.
Mdau Helsinki.
Mtalalamika sana mwisho mtasema oo basi ramadhani iwe kama world cup kila baada ya miaka minne katika nchi moja tu, si ndio?, manake mnapenda kila kitu ubwete.
ReplyDeleteHii ni kuonyesha jinsi gani huyu mtu si mpenda dini maana kama yangekua masaa machache kwake yeye ni poa ila sasa kibao kimegeuka anatafuta njia ya mkato. Acha hizo huu uislamu haujaletwa na watu wa maka kwa taarifa yako Uislamu umeletwa na Allah(SW). Na ramadhani ni yake yeye sasa ni juu yako kumtii Allah(SW) au kumtii huyo shehe wenu huko mi nipo uk baadhi ya siku huku najikuta mara ya mwisho kula kwangu ni saa nne 4 naenda zangu kulala kutokana na uchovu wa boksi naamka asubuhi nafunga mpaka hiyo saa tatu usiku bila shaka yoyote. Achaeni uroho wa kupenda kula.
ReplyDeleteYaani inaonyesha jinsi gani ndugu zangu waislamu walivyokosa elimu ya ufikiri.Hili ni swala linahitaji kufikiri,kutumia logic na ndio maana huyo mdau ameamua kuchangia nasi utata alionao ili kwa pamoja tujaribu kutafuta ufumbuzi lakini wengi mnaonekana wasomi wa madrasa tu elimu Dunia hakuna.Kama mnahisi majibu yenu ni mazuri ukweli ni kwamba Uislamu haukuletwa kwa ajili ya hao watu huko kaskazini kuna vitu haviwezekani.Joto liko zaidi ya minus 20 unafikiri unaweza kunawa vipande vipande (kutawadha)? au unaisikia baridi ukiwa Tanzania? kila kitu kinaganda. Fanyeni utafiti kwanza kabla ya kuropoka.Mengi yanayofanywa katika uislamu yanakwendana na mazingira ya jangwa huo ndio ukweli.ukikataa hainiumi kwani najua IMANI ikoje.
ReplyDeletemdau unaongea vizuri wengine ndohuo umbumbu sasa kamajua halizami afanyeje? mpe ufafanuzi hata hapa tz hapa dsm tunafuturu saa12 na dk25 bukoba wanafuturu saa moja na nusu usiku wakati ni tanzania ni moja kwahiyo wakati huo watu walikuwa hawajaijua dunia ilivyo hata kama mungu ndiye aliumba hiyo dunia kwahiyo mdau hesabu masaa hayo 13 futuru hatakama bado jua liko mbinguni au kabla jua halijazama
ReplyDeletemdau uliyehoji kwa kweli huji usemalo. kama huko mnasema ni masaa mengi jee hapa uarabuni ambapo masaa ni ya kawaida lakini jua ni kali hadi above 50 degrees centigrade. jee na sisi tufanyeje? Allah sw ameumba kila pahala pana ugumu wake na raha zake. wewe umepewa masaa mengi lakn hali ya hewa ni nzuri. pamoja na kuwa huko sasa ni summer lakni hali yake ya hewa ni nzuri sana kuliko hata afrika. hapa uarabuni summer hiyohiyo tunafunga na jua kali sana.
ReplyDeletejee nasisi tuseme tulalamike? dini ndugu yangu ni kufuata mafundisho kama unaweza fuata kama hutaki wacha ukaone kazi yake baada ya kufa kwako. lkn dini haibvadilishi kama nguo hivyo unavyotaka wewe.
kufunga na kufungua ramadhan kunafuata kuchomoza na kuzama kwa jua iwe masaa 12 iwe 20 iwe 24 nk. ndivyo dini klivyosema.
wenzetu mayahudi wakati wao Allah alipowapa funga hakuwapa daku. hiyo inasemwa wazi katika hadithi za mtume saw. sisi tumepewa daku bado unalamika!!!!
tafadhali fuata sheria....
Ramadhani inazunguka na itakapo fika majira ya baridi......uuulize pia sio uulize sammer tu.kwani mtakuwa mnafunga masaa saba hadi nane.......Mnapenda dini tu.bila kujifundisha,Eti walioanzisha kufunga.....pole sana bro...
ReplyDeleteHilo pia la majira ya theluji limezungumzwa na hao maimam na mashehe kuwa itakuwaje? Anayesema tuangalie saa za nchi za jirani sijui kama ameshafika hizi nchi za kaskazini. Nchi za jirani majira ni sawa na Norway. Utafuata wapi? Alyeandika hatujui Uislam....tunaujua sana uislam. Kuna utata ndio maana hata hao maimam na mashehe nao wameshindwa kujibu maswali ya waislam wa huku Norway.
ReplyDeleteNadhani kuna wengi hawajasoma na kuelewa maudhui ya mwandishi wa makala.
ReplyDeleteKichwa cha habari kinasema:
"Muda wa kufunga mrefu - wanatheolojia na wanazuoni wa Kiislam hapa Norway wanashindwa kutoa majibu ya uhakika!"
Mwandishi akaendelea:
"Imam Senaid Kobilica, Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislam Norway (IRN = Islam Råd Norge) amesema juzi kuwa; wataitisha kikao cha Mashehe na Maimam baada ya Ramadhani kwisha ili kujadili utata uliojitokeza wa suala hili. Imam Kobilica anakubaliana na Imam Basim Ghozlan wa msikiti wa Rabita hapa Oslo kuwa watu wanaweza kufuata masaaa 13,5 ya kufunga ya Makka. Wakati Imam Syed Nehmat Shah wa msikiti wa Central Jamaat-e Ahl-e Sunnat na Imam Hafiz Mehboob ur Rehman wa Islamic Cultural Centre hapa Oslo wanasema kuwa lazima waumini wa Kiislam wafuate masaa yaliyoandikwa kwenye Kuraani Tukufu; Kucha na kuchwa kwa jua!"
Aliyeandika na kusema kuwa mwandishi hajui Uislam - hapa nimecheka.
Huyo aliyeandika hivyo ana maana basi hata hao maimam na mashehe wa NOrway hawajui Uislam!
Imam Senaid Kobilica.. ana asili ya Bosnia na ana Ph.D the theolojia ya dini ya Kiislam. Unaposema kuwa mwandishi hajui uislam - mhhhh! nimeshiwa na nguvu. Ni sawa pia na kusema hata Imam Kobilica hajui Uislam...
Mwandishi anajua uislam sana. Ni rafiki yangu.
Kwa Mwiislam kuuliza swali (maswali) si ujinga wa kutojua uislam ni kutaka kuujua uislam kwa undani zaidi. Kuna ubaya gani kutaka kuujua usialm kwa undani zaidi.
Sisi Waislam tuna tatizo moja: mtu akiuuliza swali gumu...wanaojibu ama wanakuwa wakali ama wanamwona anayeuliza swali mjinga.
Assallaam alleykum!
ReplyDeleteAllah anasema "hakika hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake na ni muongozo kwa wamchao mwenyezi mungu" kitabu hicho ni qur'ani.
Mdau amekuja na swali au utata na anahitaji kusaidiwa,basically hoja au utata wake una "logic" kwa sababu anachokiongea kuhusu hayo masaa ni kwel.
Lakini kimsingi,kuna magumu au utata ambao kila mtu akipewa nafasi ya kusema,basi yataibuliwa magumu mengi sana,wengine ndo kama hawa wanaodai tofauti ya masaa,wengine watadai sisi nchi yetu ina joto sana na mambo kama hayo ambayo kwa binadamu ni kama "demerits" kwa sababu yangelikuwa ni "merits" kwake wala asingelalamika,kama vile kipindi cha winter kufunga huwa ni masaa machache.
Sasa kimsingi,tukikaa na kuanza kujadili magumu haya maana yake tutakuwa tunaenda kinyume na kitabu kile Allah alichosema kuwa "ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake na ni muongozo kwa wamchao mwenyezi mungu"
Tukianza kujadili vitu kama hivi maana yake tunadhamiria kukibadilisha kitabu chetu kitakatifu,Uislamu haukuja kwa kundi fulani la watu,uislamu ni dunia nzima,hata kama uko kwenye nchi mwaka mzima ni barafu,joto au siku nzima jua linawaka masaa yote 24,Mungu mwenyewe anajua jinsi ya kuwafanyia wepesi katika swaumu zenu maana hata malipo ya funga hakuna anaejua ila yeye pekee.
Kwa hiyo inshaallah tusiwe wepesi wa kuhoji vitu ambavyo viko wazi,tukumbuke Qur'an siyo katiba,tukasema tujadili kwa nini hapa kuko hivi na pale kuko vile.Maana yake tutakuwa tunafanya dhambi kubwa!!
Wabillah Tawfiq
Hussein-Mwanza Tanzania
The tougher the conditions the greater the reward. Many non-Muslim health lifestyle gurus now recommend 18 hour-fasting for up to 18 hours a day! Kwa hivyo basi faida inaanza hapa hapa duniani. Lakini faida kubwa zaidi ni kiroho/kidini. Yaani, kupiga vita matamanio yako ya kimwili na kihisia. Kina Nabii Issa (AS) walikuwa wanafunga siku 40 mfululizo, lakini sisi hatuko katika daraja lao.
ReplyDeleteOK. Naomba wadau wote waliotumia muda wao bila kufikiri vizuri juu ya mantiki ya swala hili kumshambulia huyo aliyeleta hii mada hapa watupe majibu ya nini waislamu wanaoishi huko wafanye ktk zile siku ambazo jua halizami kabisa. Tumeambiwa tule linapozama na kama kuna kipindi halizami kabisa wafanyeje? Mimi naamini mwenyezi mungu alipotuletea dini hakuwa na maana ya kutukomesha bali kutufundisha njia muafaka za kumtii yeye. Na naamini kuwa huyu mdau anataka kujua na bila shaka jambo hili linaweza kupatiwa ufumbuzi ikiwa wasomi watachimba zaidi ktk qoran na hadithi za mtume (SAW). Ramadhan kareem.
ReplyDeleteNenda hii website wana software nzuri tu itakupa nyakati zote za sala na kufutari ana kula daku. http://www.islamicfinder.org
ReplyDeleteAcheni mambo ya UROHO hayo siku hizi hata wasiokuwa waislam wanafunga. Kuna jamaa hapo mkiristo ni mtu wa tizi nae anasema anafunga tena anasema anakula tende siku nzima. Yeye matamanio anayo isipokua amengundua akifunga afya yake inakuwa nzuri. Msipende sana kusikiliza waislamu wa ki-Ughaibuni hususan hawa wazungu maana wengi wao wana agenda za kubadilisha uislam na kuwa ukubalike na wenzao wa magharibi. Nchi kama Uturuki wamebadili mambo mengi ya kiislamu ili yaendane na siasa zao. Wabosnia nao pia wapo katika kundi la Waturuki. Haina maana mtu ana PhD ndio umsikilize inawezekana ni MUONGO na MNAFIKI. Uzuri wa Uislamu ni kuwa unatakiwa ufuate vitu viwili tu Quran na Hadith SAHIHI za Mtume.
ReplyDeleteHussein wa Mwanza umeandika tusiwe wepesi kuhoji vitu. Sawa na mimi naongezea tusiwe wepesi kujibu maswali magumu kwa majibu mepsi ya haraka haraka.
ReplyDeleteWaislam hawako wa tamaduni moja na asili moja. Tuko wengi na wenyewe itikadi tofauti za madhehebu ya Uislam.
Mwandishi ameleta mada ambayo inazungumzwa na wanatheolojia na wanazuoni wa hapa Norway. Si mada ya mwandishi.
Na ndio maana wanatheolojia, wanazuoni, maimam na mashehe na waislamu wengine hapa Norway wakiongozwa na Baraza la Waislam Norway (IRN) wameamua kulivalia njuga suala zima la majira ya kufunga wakati wa majira ya theluji, kipindi ambacho wakati mwingine jua halitoki na wakati wa majira ya Kiangazi, wakati ambao sehemu zingine hapa Norway jua halizami kabisa.
Wanaotoa majibu ya haraka haraka tu kuwa ahha - mtu anaweza kufunga masaa arobaini na nane...wanapoteza lengo zima.
Quraani inasema: Jua kucha na kuchwa. Hakuna ubishi hapa.
Je, wakati wa kiangazi hapa Norway sehemu ambazo jua halichwi kabisa wasifunge?
Je, wakati wa majira ya theluji sehemu ambazo jua halichi (halitoki kabisa) wasifunge?
Hilo hata wataalamu wa dini hapa Norway wana utata nalo.
Hakuna sehemu inayozuia mtu kuuliza swali linalohusu dini ya Kiislam.
Narudia: Ndio maana wanatheolojia, wanazuoni na waislam wengi hapa Norway wakishirikiana na Baraza Kuu la Waislam Norway (IRN) watakaa na kulizungumza hili baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Suala hili si la mwandishi wa makala peke yake.
Kuna mmoja aliyechangia ameandika kuwa mbona Alaska wanafunga? Hali na mazingira ya Alaska huwezi kuyaweka kwenye hali na mazingira ya Norway.
Hao Waislam na wataalam wa dini hapa Norway wnaijua Quraani fika si wajinga kusema watakaa na kulizungumzia suala hili baada ya Ramadhani.
Hilo suala halihusu majira ya Kiangazi pekee, linahusu pia na mjira ya theluji.
Na halina uroho, kukashifu dini ya Uislam au vitu vinavyofanana na hivyo ni swlai la muhimu. Yanatakiwa majibu ya kufikiri kwa mapana na marefu na si ya haraka haraka tu....
http://www.islamicfinder.org
Haiwezi kunipa muda wa kula daku wala kufuturu wakati wa majira ya theluji au wakati wa majira ya kiangazi hapa Norway. Nimeshaipitia.
Tamati
Ndugu zangu waislamu,jazba za nini, tena mwezi mtukufu wa Ramadhani? Mtu kauliza anapaswa kuelekezwa kwa uzuri. Kama ni mjadala wa Winter,kama wewe ni mjuzi, basi eleza ujuzi wako ili watu waupate. Saumu si kwa ajili ya binadamu bali ni kati yamja na mwenyezi Mungu. Achaeni kuhukumu (statement kama hujui utendalo, wewe ni muislamu jina, winter hamlalamiki nk). Kejeli za nini? Siku ya hesabu ni Mja na Mwenyezi Mungu hivyo chunga kauli yako ndugu Muislamu!
ReplyDeleteUjinga ni mzigo. Hivi kwanini sisi waislam huwa waoga sana mtu anapohoji mambo ya dini yetu? Kuuliza si kosa na ni njia ya kujifunza. Kama kuna mtu anajua atoe majibu ya uhakika. Ktk miaka ijayo kuna maeneo hayo aliyoyataja huyu mdau, jua litakuwa halizami wiki nzima ndani ya mwezi wa Ramadhan. Je, waislam wa huko wasile wiki nzima? Huo ni ukweli kwamba Ramadhan zijazo zitakuwa ndani ya kipindi ambacho jua sio linachelewa kuzama bali halizami kabisa. Wenye elimu ya kutosha watupe ufafanuzi wa jambo hili.
ReplyDeleteWEWE NI MNAFIKI NA MNAFIKI MKUBWA AU NSIO MARA YAKO YA KWANZA HAPA ULAYA
ReplyDeletePILI.MUOMBE MWENYEZI MUNGU MSAMAHA KWA UNAYOSEMA.1 HAWAKUJUA KAMA SCUNDANAVIA WAKATI HUU MAGHRIB NI SAA TATU NA ALFAJR SAA TISA!HALI MDA UNAZIDI KUPUNGUA KWA MAGHRIB.2 KIPINDI CHA WINTER MAGHRIBI INAWAI NA ALFAJIR INACHELEWA SWALI KWA NINI USIFUATE TANZANIA KWA BABA NA MAMA?JIBU MMMMHHH KIMYAA WEWE FUNGA NA KAMA UTAKI NENDA KASOME UIJUE DINI YAKO VZR.
NDIO NYINYI MNAOLETA ,IGONGANIO KWENYE DINI YA MWENYEZI MUNGU KWA UJINGA WENU HALI MNAJUA QUR ANI INA KILA KITU
lETE MADA KUHUSU POSHO ZENU ZA UKIMBIZI SAHIHI KUCHUKUA AU MZIACHE?
WADAU TUPUNGUZE JAZBA NA HUYU MTU AJIBIWE KUTOKANA NA UPEO WA ELIMU SASA KAMA WATU HAMNA ELIMU YA JAMBO HILI NI VYEMA KUMTAFUTA ULAMAA MWENYE ELIMU NA HILI AFAFANUE...KUMBUKENI QUR-AN INAUFAFANUZI WAKE NA NI HADITHI NA SUNNA BASI TUWE WAPOLE TUZUNGUMZE JAMBO AMBALO TUNA UPEO NALO...USHAURI WANGU HUYU BWANA TUMSAIDIE KITAALAMU LI AJUE VYEMA NINI SWAUMU NA SHARTI ZAKE!
ReplyDeleteNITAMUULIZE ULAMAA HAPA KISHA NITATOA MAONI YA KITAALUM JUU YA SUALA HILI NA WENGINE MTAFUTE MAULAMAA HUKO MLIPO TUPATE MAJIBU SAHIHI...M/MUNGU ANASEMA "LA IKRAA FFI DDIN" HAKUNA KULAZIMISHANA KATIKA DINI ILA NI KUFAHAMISHANA...INSHAALLAH SHIME AALLAYKUM!
Mnamkumbuka yule Phd Amina (Islamic Feminist Imam) aliyesalisha jamaa kwa mkanganyiko wa watu na vituko kadhaa kule marekani, je na yeye afuatwe kwa matamanio yake,
ReplyDeleteHakika quran ni kitabu kisicho na shaka na hadith za bw. Mtune (S.A.W) ndio jibu.
Ila poleni sana kwa kulilia muda, wataalamu wa fiqih toeni fatwa suali ni gumu.
Mdau mMlaysia
Ikifika muda huo turudi nymbani tukafunge kwa masaa tuliyoyazoea
ReplyDeleteMkuu alieandika:
ReplyDeleteUmeanza kwanza kumsema mwandishi wa makala kuwa ni mnafiki....halafu ukamalizia na:
LETE MADA KUHUSU POSHO ZENU ZA UKIMBIZI SAHIHI KUCHUKUA AU MZIACHE:
Mkuu, si wote tulio huku Norway ni wakimbizi. Wachache sana waliotoka Tanzania wamejilipua huku.
Wengi tulio huku tumekuja kwa uhalali na tuna shughuli zetu za kila siku zinazotulisha na familia zetu na tunalipa kodi kama watu wengine huku.
Hiyo peke kudhani kila mtu huku ni mkimbizi ni kejeli kwa upande wako.
Hiyo mada aliyoleta mwandishi wa makala si ya kwake peke yake ni ya Waislam wengi huku tumejiuliza na wanatheolojia, maimam, mashehe na wanazuoni wa hapa Norway wameshindwa kutoa majibu ya uhakika na ndio maana wameamua kukutana na kulijadili hili baada ya Ramadhani.
Hakuna Mwiislam huku anayetaka Quraan ibadilishwe na hakuna anayetaka mgogoro.
Swali gumu limeulizwa na halitaki majibu mepesi na ndio maana litajadiliwa na Baraza Kuu la Waislam Norway (IRN = Islamsk Råd Norge).
Sasa hata IRN nao ni manafiki? IRN kuna Waislamkutoka pembe zote za dunia. Nao ni Waislam pia.
Mada hii imekuwa ikija kila wakati huku Skandinavia: Kiungo hapo chini ilikuwa ni Denmark. Mwulizaji alijibiwa na sheikh kuwa mfungaji anafunga kufuatia masaa ya Denmark ni sio kwingine kokote. Je, huyo shehe aliyejibu hivyo mnafiki?
http://www.haya.dk/Fasten/er-det-muligt-at-faste-i-forhold-til-mekkas-tider.html
Hii kwenye kiungo hiki hapo chini ilitoka mwaka 2006 na aliyeuliza hakujibiwa kwa kejeli wala majivuno. Alijibiwa Kiistaarabu kabisa. Bahati mbaya iko kwa Kinorwejiani
http://www.islam.no/forum/forum_posts.asp?TID=3718
Hii mada aliyoandika mwandishi ilianzia kwa Waislam wa Norway (si mwandishi wa makala). Ilitoka kwenye gazeti la Aftenposten la jioni Jumatano 3. Agosti 2011 ukurasa wa 4.
Ikiwa na kichwa cha habari kwa Kinorwejiani: "Vil følge Mekkas fastetid" yaani "nitafuata masaa ya kufunga ya Makka" Yaani masaa 13,5 vyovyote vile.
Ikaendelea kwenye Aftenposten la jioni Jumatano 10 Agosti 2011 ukurasa wa 12. Ikiwa na kichwa cha habari "Uenige om kortere faste" yaani "hawakubaliani muda mfupi wa kufunga"
Kwenye hili Aftenposten la tarehe 10 Agosti ndipo wanatheolojia, maimam, mashehe na wanazuoni wakawa wamesema kuwa wameshindwa kuafikiana kuhusu muda wa kufunga na kufungua kwenye kipindi cha Kianagzi na pale Ramadhani itakapoangukia majira ya theluji.
Imam Senaid Kobilica, shehe mkuu wa Baraza la Waislam Norway (IRN = Islamsk Råd Norge) akawa amasema kuwa watakutana kulijadili baada ya Ramadhani hii.
Kwa hiyo watakaochangia kutoa majibu wayaelekeze kwa Waislamu wote wa Norway na si kwa mwandishi pekee na badala ya kutoa majibu ya kejeli na kebehi; tunaomba majibu ya kitaalamu ya kidini.
Tamati.