Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Mrisho Shaban (kushoto) akimkabidhi msaada wa vyakula Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Juma Lukinga kwa ajili ya sikukuu ys Eid El Fitr wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika shule hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.

Na Francis Dande
KAMPUNI ya simu Tanzania (TTCL) leo imetoa msaada wa vyakula kwa watoto walemavu wa shule ya Uhuru mchanganyiko pamoja na wasiojiweza katika kituo cha SOS kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi misaada hiyo vyenye thamani ya shilingi mil 3.5. ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Mrisho Shaaban alissema msaada huo unalenga kusherehekea sikukuu ya Idd Elfitr pamoja na watoto ambao kwa namna moja ama nyingine ni kundi linalohitaji kusaidiwa na jamii inayoizunguka.

“Sisi TTCL kama kampuni ya umma na ya kizalendo tunajali sana jamii inayotuzunguka pamoja na matatizo yake ndio maana leo tunatoa msaada wa vyakula kwa makundi haya ya watoto wahitaji kwa kuwa in jukumu letu kama kammpuni ya kitanzania kusaidia,”alisema Shaaban.

Alisema mbali na kutoa misaada kwa Uhuru na SOS lakini pia tayari wametoa misaada kama hiyo kwa vikundi vya wazee , yatima na walemavu wa viungo vya mwili mjini Moshi ambapo vikundi vitatu kila kimoja kilipatiwa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.

“Tunaahidi kuendelea kuhudumia jamii yetu pale kampuni inapofanya vizuri na mapato kuongezeka kwani ndio njia mojawapo ya kurudisha baadhi ya mapato tuliyokusanya kwa wateja wetu ,”alisema Shaaban.

Aidha aliwaomba watanzania kuendeleza ushirikiano na kampuni hiyo katika kupinga hujuma zozote dhidi ya mtandao na kampuni ya TTCL kwa ujumla.

Naye mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Juma Lukinga alisema sio mara ya kwanza kupokea misaada mbalimbali kutoka kwa TTCL na kwamba anamshukuru mungu kwa kuwa misaada hiyo inawasaidia sana kutokana na hali ngumu ya maisha iliyopo.

Alisema misaada hiyo itawasiaida kula na watoto katika sikukuu ya Idd na kwamba watajiona wanafuraha sawa na watoto wengine .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Heee wazee wa kutwanga kumbe bado muko hai! Tunawamiso kweli kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...