Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe, akizungumza na Balozi wa Libya nchini, Prof. Ahmed El Ash'hab baada ya Balozi huyo kuitwa Wizarani,Dar es Salaam leo . kufuatia Ubalozi huo kubadilisha Bendera ya nchi hiyo bila kufuata taratibu. PICHA NA MDAU TAGIE MWAKAWAGO WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. We surely don't wanna get ourselves immersed into this mess at this juncture like Zimbabwe. Lets just be observers and select our course wisely! Currently, the situation is very fragile there, though its all said and done that 'The King of Kings' is no more the King of Tripoli, or even Sirte for that matter. Am jus sayin!

    ReplyDelete
  2. Wizara inatakiwa kukubaliana na matakwa ya wananchi wa Libya; siyo kushikilia msimamo wa kutotambua TNC, kwani Libya kwa sasa serikali iliyokuwa madarakani imeshakubali matokeo; hivyo mataifa mengi yanayotambua Haki za binadamu yameshaitambua TNC; sielewi Tanzania wanashikilia msimamo gani. Tunakumbuka miaka ile wakati ule Mercedes Benz kibao zilipomwagwa ikulu; kipindi cha Mzee; kwa hiyo wanataka 'Wasimwangushe' Brother leader. He is GONE; mwisho. Bendera ya TNC inatakiwa ikubaliwe kote duniani; watu wa Libya wameteseka vya kutosha.

    ReplyDelete
  3. Tanzania acheni kujifanya mnajua sana!Walibya hawamtaki Ghadafi na nyie mnamtaka awe rais wa wapi?

    ReplyDelete
  4. kwani walibya washafanya uchaguzi na kusema hawamtaki Gadafi? kama wao wababe wafanye uchaguzi in the next 6 months halafu wamruhusu na Gadafi asimame waone matokeo

    ReplyDelete
  5. Wewe Any wa 02.42 kwani serikali mpya inapatikana tuu kwa kufanya uchaguzi? Yeye Gaddafi aliingia madarakani kwa kuchaguliwa? Duh! Wakati mwingine tunailamu serikali lakini kama kuna Watanzania wenye vichwa vibovu kama chako,ni balaa tupu.

    ReplyDelete
  6. Walibya hawajafanya maamuzi bado. maamuzi yamefanywa na NATO. Ukoloni uyooo unarudi Africa.

    ReplyDelete
  7. Asanta sana ndugu Membe hata kwa kiasi hicho umeonyesha msimamo na ujasili mkubwa.
    Nyie anony wa kwanza, pili na tatu hamjui dunia inavyokwenda. Kama anony wa nne hapo juu alivyosema. Walibya hawakumkataa bwana wa pamba. BwP amekataliwa na wakoloni mambo leo. Hao walibya munaowaona kwenye picha wameshika mitutu ni watoto wadogo kwa fikra kama nyinyi anony wa kwanza, pili na tatu. Bwp aliwatunza sana watu wake. Subili mutawasikia hao walibya wenu watakavyolia baada ya Bwp kuondoka. Eti Oh! miaka 45 amekuwa raisi! huu ni unafiki mkubwa!? Fikilini sana bila sisi kudai uhuru wetu hao wakoloni wasingeondoka, wangetutawala mpaka leo hii. Na hiyo ingekuwa miaka mingapi vile? Hata hivyo nchi nyingine hawakutaka kutoa uhuru mpaka kwa mtutu! Na leo hii bado wananyemelea ili warudi. Fikilini msifanye makosa yasiyoweza kulekebishika. Ni kweli tuna matatizo yetu ya ndani kama wakoloni. Lakini tukumbuke AFRIKA NI MOJA!

    ReplyDelete
  8. Tanzania tuna matatizo mengi ya kushughulikia kabla ya kuingilia mambo ya wanaume wa shoka wa Libya. Nchi iko kwenye giza, elimu duni, sekta ya afya imekufa, ajira usiseme, inflation through the roof halafu mnahangaika kumhoji balozi wa Libya! Kweli priority zenu ziko backward. Mdau

    ReplyDelete
  9. huyu naye anachekesha...badala ya kuhoji ni kwa nini TZ inagawa ardhi ya wananchi kwa wazungu anaishia kuuliza hayo ya bendera! Looooooo!

    ReplyDelete
  10. Membe kwa ubabe ndio mwenyewe!

    Yeye ni vitisho na onyo kali, kila kukicha.

    Mabalozi wa nje anawaona kama watoto wa shule wa kufundisha nidhamu. Diplomasia ni kama ameweka pembeni kabisa.

    After-all, who else in the world cares about what Tanzania thinks of Libya? Jee tutawapa msaada?

    Kwanza tusipoangalia hata mafuta tutanyimwa na serikali mpya halali ya watu wa Libya.

    ReplyDelete
  11. Walibya walifanya lini uchaguzi kumchagua Ghadaffi?

    ReplyDelete
  12. ni kitu gani watu wasichoelewa kuwa Gadafi kaondolewa na Nato na hao wapinzani mnaosema wengi wao sio raia wa Libya wengi wamepandikizwa toka Afghanistani na Tunisia na nchi jirani zinazoizunguka Libya ni wazi kuwa bado kuna majority ya waLibya wanaomuunga mkono Gadafi, watu hawajiulizi hao wapinzani wangekuwa kweli na uchungu na nchi yao wangekua wanaua raia wasiokuwa na hatia, unakumbuka majeshi ya NATO yalipotupa mabomu na kuua maelfu ya raia na baadae kuomba radhi kuwa walitupa mabomu hayo kwa makosa, huyo aliyedai maembe aulize maswala ya ardhi basi hiyo sio kazi yake yuko Anna Tibaijuka ni waziri wa Ardhi mengi ni waziri w mambo ya nje na hiyo ndio idara yake haswa kama kitu hamjui msiropoke. huyo balozi hakuletwa nchini na wapinzani na kama mnavyojua waarabu ni wanafiki, kwanza hao rebles hawataki kabisa kuitwa waafrika wao ni waarabu ndani ya bara la afrika sasa kwa nini sisi tuwasupoort? tangu mapigano yaanze wanaoteseka ni waLibya weusi amabao walitetewa sana na utawala wa Gadafi.

    ReplyDelete
  13. Ghadafi keshakimbia! Tanzania kila kukicha siasa. Wenzetu wa Nchi zinginge za afrika wanawahi kuwatambua wapinzani na wanajiwekea nafasi nzuri ya madili ya biashara. Tanzania viongozi wetu ni kama Ghadafi

    ReplyDelete
  14. mgogoro wa libya ni tatizo lililosababishwa na sarkozy,kisa anataka mafuta kwa kuwekewa pipe ambapo Gaddafi aligoma na sarkozy kusema tutakutoa na kweli yanatokea,unajua kama Gabdo alitolewa na sarkozy pia?kisa makampuni ya kifaransa yalitakiwa kulipa kodi paris na sio Ivory cost?Na Bagbo alivyokuwa mbisha akaambiw autatoka na kweli ametoka.Unafahamu kuwa Boss wa IFM alikuwa anapinga nchi za west kujihita matajiri wakati wanategemea nchi masikini kama India,Brazil,China na nyingine kibao,na alikuwa mpizani wa Urais wa sarkozy na akaletewa kesi ya kubaka na sasa hayupo kwenye short list ya wagombea tena.Africa tusipokuwa makini tutatawaliwa tena na Hili la Libya ni Umoja wa waafrica ndio unatarajiwa kuwa kikwazo na sio Tanzania peke yake,kamaLibya iko africa basi tungeweza kusolve matatizo yetu ila west ni viburi wa kutupa especialy sarkozy,a short man.Kama wanapenda amani basi walitakiwa kwenda somalia kwanza kabla ya kwenda libya.Wanafiki watu wa west na Nato yao.

    ReplyDelete
  15. anon wa tue aug 30, 03;36;00 am 2011 Gadafi hakukubaliwa na wananchi wa Libya kabla ya mapinduzi yaliyomuweka madarakani. Gadafi, Arafat, Mohamed Boudia (Carlos m-Algeria), illich ramirez sanchez( Carlos m-Venezuela),madam Cellech (mpoland) Anwar sadat, kuwataja wachache hawa walisomeshwa na urusi siasa za ujamaa wa kirusi na mafunzo ya kijasusi katika chuo cha Patrice Rumumba urusi ili wakaueneze duniani kote hata kwa mtutu wa bunduki, kuisaidia urusi kuwa na nguvu duniani (ukoloni mambo leo). Hivyo basi Gadafi alisaidiwa na wakoloni wa mashariki kuingia madarakani, na sasa 'amesaidiwa' na wakoloni wa magharibi kuondoka madarakani. na kama ni kweli wa libya watateseka hawata hudumiwa vizuri, basi Gadafi nae alikuwa mkoloni kwanza hakutaka kuachia madaraka na pili hakuwarithisha wa libya utamaduni wa kuhudumiana vizuri kama alivyowahudumia kama kweli aliwahudumia vizuri, kwani mkoloni hawezi kufundisha watu anaowatawala kuthaminiani. viongozi wengi waafrika ni watawala (wakoloni), hawataki kuachia madaraka, wanachukua sehemu kubwa ya rasilmali za nchi kwa manufaa yao na familia zao huku wananchi wakiteseka, na kupitisha maamuzi kibabe bila kujali maslahi ya mataifa yao ili mradi wao na familia zao wanafaidika, lakini kwa sababu wanawafanyia wananchi wenzao basi wanaonekana kuwa si wakoloni.

    ReplyDelete
  16. Kweli Tanzania tumeishiwa na Uzalendo wetu

    Mwl. Nyerere alitufundhisha mengi kuhusu Haki za Wananchi

    Gadaffi aliwanyima haki wananchi wake akajenga utumwa kwa kutoa pesa kwa Nchi zetu za Africa... Tumesahau kweli MONEY IS EVIL

    * SINDIO HUYU ALIJIUNGA NA IDD AMINI KUTUVURUGA?
    UN WANAITAMBUA HAWA WAPINZANI KWANINI SIO TANZANIA?

    KWELI TUMEISHA, SIO TANZANIA YA KIZALENDO

    Mswahili - New York

    ReplyDelete
  17. Kweli Tanzania tumeishiwa na Uzalendo wetu

    Mwl. Nyerere alitufundhisha mengi kuhusu Haki za Wananchi

    Gadaffi aliwanyima haki wananchi wake akajenga utumwa kwa kutoa pesa kwa Nchi zetu za Africa... Tumesahau kweli MONEY IS EVIL

    * SINDIO HUYU ALIJIUNGA NA IDD AMINI KUTUVURUGA?
    UN WANAITAMBUA HAWA WAPINZANI KWANINI SIO TANZANIA?

    KWELI TUMEISHA, SIO TANZANIA YA KIZALENDO

    * sipendwi? niambie niache kutuma maoni yangu - nngu007@hotmail.com

    ReplyDelete
  18. Hata kama BwP alimsaidia Amini bado tunaweza kuwa jasili kwa kumsamehe. Kisasi hakiwezi kutufikisha popote, ila umoja ni nguvu. Hata wewe anony wa Tue. aug. 30,02:50 ugombanapo na ndugu yako au mfanyakazi mwenzako ni vema kusamehe ili maisha yaendelee. Maana unaweza kumnunia mtu maisha yako yote harafu siku moja ukakumbwa na gonjwa, harafu ukaambiwa huyo huyo unaemnunia ndiye ana dawa ya kukutibu. Je,utafanyaje? Unasema uko Newyork, right? Kuwa baba kuwa. Hao wababe wa hapo unapoishi hawapatani na waingereza kwa kuwa waingereza waliwatawala na kuwatoza kodi kichizi, lakini yote wamesamehe na hata wakaungana kumteketeza mwana wa Useni. Inashangaza sana kuona kuwa mimi na wewe na unyonge wote huu bado tunamchukia Bwp. Kama sikosei kuna maajabu saba ya dunia, na hili ni la nane.

    ReplyDelete
  19. yaani eti TZ inajitutumua hatimae!! hao ni vibaraka wa US nyie TZ mna ubavu wa kuwatisha?! Tishia nyau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...