Na Audax Mutiganzi,Bukoba

JUMLA ya wananchi 1,076,260 mkoani Kagera wamenufaika na mradi wa unyunyiziaji ya  dawa ya ukoko majumbani unaofadhiliwa mfuko wa rais wa marekani wa kupambana na malaria  unaoratibiwa na  shirika la maendeleo la nchi hiyo (USAID).

Hayo ilidhihirishwa jana na Dr Woiufoo Munisi ambaye ni msimamizi wa mradi wa unyunyiziaji wa dawa ya ukoko majumbani (RTI) wa mkoani Kagera alipoongea na waandishi wa vyombo vya habari jana.

Munisi aliwaambia waandishi wa habari kuwa wananchi hao walinufauka na unyunyiziaji wa dawa ya ukoko majumbani toka mwaka 2007 hadi mwezi april mwaka 2011.

Msimamizi huyo alisema walionufaika na mradi huo ni wananchi wa wilaya za Ngara, Karagwe, Biharamulo,Chato, Bukoba vijijini, Muleba na Misenyi, alisema wananchi ambao dawa ya ukoko haikunyunyiziwa majumbani mwao ni wananchi wa manispaa ya Bukoba.

Alisema unyunyiziaji wa dawa ya ukoko majumbani imeweza kushusha maambukizi ya ugonjwa wa malaria mkoani Kagera toka asilimia 41.1 mpaka asilimia 5, Munisi alisema kabla ya serikali kuanza kunyinyizia dawa hiyo majumbani mwaka 2007 milipuko ya malaria ilikuwa mikubwa.

Aliendelea kuwaambia waandishi wa habari kuwa milipuko ya ugonjwa wa malaria ilikuwa mikubwa katika wilaya za Karagwe na Muleba, alisema idadi ya wagonjwa wa maralia ilikuwa kubwa sana kiasi cha kutisha.

Munisi alisema wakati wa mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa malaria wilayani Muleba wagonjwa walikuwa wakilazwa katika hospitali ya Rubya na wilayani Karagwe wagonjwa walikuwa wakilazwa katika hospitali ya Nyakahanga.

Alisema mahospitali hayo yalikuwa yakifurika wagonjwa wa Malaria, kipindi hicho wagonjwa wanne wa  malaria walikuwa wanalazwa  kitanda kimoja, kutokana na hatua ya kufurika kwa wagonjwa hospitali zililazimika kujenga wodi za dharura za mahema.

Msimamizi huyo aliwaambia waandishi wa habari alisema unyunyiziaji wa dawa ya ukoko majumbani imekuwa faraja kubwa kwa wananchi mkoani Kagera kwa kuwa maambukizi ya ugonjwa wa malaria yanakaribua asilimia sifuri.

Munisi alisema dawa hiyo imeonyesha mafanikio makubwa ya kuthibiti ugonjwa wa malaria, alisema kinachodhirisha hali hiyo ni idadi ndogo sana ya watu wanaokwenda kutibiwa ugonjwa wa malaria mahospitalini.

Alisema wodi za kulaza  wagonjwa wa malaria katika mahospitali mkoani Kagera ni tupi hazina wagonjwa, alimalizia kwa kusema watu kwa sasa hawaugui malaria kwa kuwa vimelea vya ugonjwa huo vimeharibiwa na dawa ya ukoko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Asilimia 40 hadi 5 ni kubwa sana. Wafanye utaratibu dawa hii isambazwe Tanzania nzima. Natumaini wauza dawa wa kimataifa (ambao wanapenda tuendelee kuugua Malaria) watatuchunia

    ReplyDelete
  2. Dawa ya ukoko, hiki kiswahili cha wapi? cha wapi?

    ReplyDelete
  3. Hao USAID waaendelee na mikoa mingine ikiwemo DSM. Mbu ni wengi sana licha ya huduma nyingi kuwepo za hospitali. Yaani toka mwaka 2007 bado mko mkoa mmoja tu, kweli tutafika? Serikali pamoja na kugawa net za Bure za Rais Bush, sasa umefika muda wa kunyunyizia mbu wenye malaria wafe. The government has to take serious initiatives now!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...