Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetoa fursa kwa Watanzania kuweza kupiga kura na kuchagua mrembo anaevutia zaidi kati ya warembo 30 wanaoshiriki katika shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania 2011.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Bw. George Rwehumbiza alisema ili kupiga kura Watanzania watatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na namba ya mshiriki kwenda 15550 ambapo gharama kwa kila ujumbe ni shilingi 150 tu .

Aidha Bw, Rwehumbiza aliongeza kuwa kila ujumbe mfupi utakaotumwa utampatia Mtanzania pointi 10 ambapo wateja 20 watakaobahatika kuwa na pointi nyingi zaidi kila mmoja atajipatia TIKETI mbili za VIP zitakazomwezesha kwenda kushuhudia fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011 itakayofanyika tarehe 10 mwezi septemba katika ukumbi wa  Mlimani city jijini Dares salaam.

Pia kwa wale watakaohitaji kutoa maoni au mitazamo yao mbalimbali kuhusu Vodacom Miss Tanzania watapata fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na maoni kwenda namba 15550.

Akisisitiza hili Bw. Rwehumbiza alisema ili kuwafahamu warembo wanaoshindania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 Watanzania wote wanaweza kuangalia kituo cha STAR TV leo kuanzia muda wa saa moja jioni pamoja na CLOUDS TV muda wa saa tatu usiku kila siku pia soma magazeti ya Mtanzania, The African,Dimba,Rai na Bingwa.

Vodacom
kazi ni kwako

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Haya bwana mambo haya mwezi huu mtukufu wa ramadhani hayanivutii kabisa. Ngoja nikafuturishe watoto wa mtaani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...