Waagizaji wa mafuta kutoka makampuni mbali mbali yanaoagiza na kuuza mafuta hapa nchini, wakiwa katika mkutano wao  Wizara ya Nishati na Madini, kujadili kuhusu mgomo wa makampuni ya kuuza mafuta wanayoyamiliki uliotokana na serikali kupitia EWURA, kushusha bei za mafuta.Katika mkutano huo ulioongozwa na Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na viongozi wa EWURA, waagizaji na wauzaji hao  wa mafuta wamekubali kusitisha mgomo wao na kuendelea kuuza mafuta kwa bei mpya iliyotangazwa na EWURA.
Picha na mdau Victor Makinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. hawa jamaa ni watanzania kweli.naona sura za kipakistani pakistani hapo!LOL

    ReplyDelete
  2. Serikali inabidi iangalie hili. Kuna watu wako humu nchini kwa sababu za kibiashara na ki-maslahi tu, hawajui wajibu wao kwa jamii na taifa. Wanataka 'haki' tu lakini kuwajibika hawataki. Ndugu zetu wengi kama hawa wanaoonekana kwenye picha hii (waliozunguka meza)wana uraia wa nchi zingine ingawa huwa wanajifanya ni watanzania. Hawana uzalendo wa kujali maslahi ya wadau. Kama serikali imepunguza bei kutokana na kuondoa au kupunguza tozo na kodi zeke yenyewe, tatizo la hawa ni nini!? Hiyo hasara wanayoisema inatoka wapi? Au walikuwa hawawakilishi makato ya serikali? Hoja ya uzawa na uzalendo inanukia hapa! Sekta nyeti kama hizi inabidi zishikwe na wazalendo.

    ReplyDelete
  3. Kweli nimeamini aslimia kubwa ya watz ni wabaguzi kichizi. Hakuna sheria inayomzuia mtu kufanya bishara halali hapa nchini. Na hakuna mfanyabishara atakayekubali kupata hasara hata siku moja. Kwa hiyo awe muhindi ama mchaga swala la uzalendo hakuna mbele ya pesa.

    ReplyDelete
  4. mimi nadhani wanasahau kuwa serikali hiyo hiyo ikitangaza kupanda kwa bei ya mafuta saa 3 asubuhi,wao wanapandisha saa 3:05 asubuhi hiyo hiyo tena bila mgomo wala vikao kama hivi! sasa wasiwe wagumu na kuhitaji vikao vikao wakati wa kushuka bei! muosha huoshwa!!

    ReplyDelete
  5. Kuvaa suicide jacket sio ngumu kama kugoma kuuza mafuta ala..hutuoni vp!!
    Sisi ni wenye nchi yenu Bwana..Kohoeni muwone kama mtakaa muone wese..alaaaaaaaaaahh...

    ReplyDelete
  6. Kwenye sura hizo hapo zinazooneka ni yupi mwenye kuitakia Tanzania mema. Hamna watanzania halisi wanaohitaji vibali vya kuagiza mafuta. Mbona biashara zenye manufaa zinatawaliwa na hawa wa asia. Kuna siri gani hapo. Tutaendelea kukamuliwa hadi tone la mwisho kama hali yenyewe ndio hii. Faida wanayoipata hawa kwa asilimia kubwa, haina manufaa kwa taifa letu. Na nina shaka kama kweli serikali inapata kodi inayostahili kutoka kwa hawa watu. Maana inajulikana wazi hamna wakwepaji kodi kama hawa. Ndio wale tulio wazoe wanasema je unataka bei ya risiti au isiyo na risiti.

    ReplyDelete
  7. NYINYI WALALAHOI HAPO JUU KWANI HAMJUI KAMA KUNA WAARABU WATANZANIA NA WAHINDI WATANZANIA?ACHENI USHAMBA NA UBAGUZI WENU MTAKUFA NA KIJIBA CHA ROHO.
    HAWA WALIGOMA KUTOKANA NA KUPUNGUZWA KWA BEI KWA KUSTUKIZWA ANGALAU WANGESUBIRI MAFUTA WALIONUNUA KWA BEI JUU WAYAMALIZE ILI NA WAO WAPATE KUNUNUA KAMA WATAPUNGUZIWA.HALAFU SERIKALI INAPO WAAMURU KUUZA KWA BEI YA CHINI WAKATI WAO HAWATAKI KUPUNGUZA KODI SASA HAMUONI KAMA NI BIASHARA KICHAA?HAWAJAKURUPUKA TU NA KUGOMA KUUZA MAFUTA KWANI NA WAO PIA WATAFURAHI KUPUNGUZWA KWA MAFUTA MAANA KUPANDA KWA MAFUTA HUSABABISHA BIDHAA NYINGI KUPANDA BEI KWASABABU YA USAFIRISHAJI WA BIDHAA.
    HALAFU NYINYI WASHAMBA ACHENI KUCHAFUA HALI YA HEWA HAPA.

    ReplyDelete
  8. Mbona mafuta yakishuka bei huko kwenye soko la dunia wao hawashushi? Mwalim aliposema njia kuu za uchumi tuzimiliki wenyewe mkamuona mjinga. Mafuta ni bidhaa muhimu na lazima ununue ili uwezi kuendesha gari. Pia mafuta hayaharibiki kwa kukaa muda mrefu. Lazima serikali imlinde mtumiaji. Mfanyabiashara kila siku anataka faida kubwa. Serikali lazima ithibiti uuzaji wa bidhaa muhimu kwa maisha ya raia. Mbona Kenya mafuta rahisi?

    ReplyDelete
  9. Kuna watu wengine ni ndumilakwili. Ni nani mfanyabiashara gani ambaye hataki kufanya biashara yenye manufaa na faida kubwa? Mwalim amepinga kwa nguvu zake zote mifumo ya ubaguzi ikiwemo ukabila. Mimi sioni shida ya kufanya hiyo biashara mtu mwingine yeyote. Aingie na afanye sio kulalamika ovyo. Kwanza hiyo ni sign ya uvivu wa kufikiri na ujinga. Tubadilikeni!! Yes Change we can Believe in!!

    ReplyDelete
  10. Duuuh wahindi wamekamata uchumi wa tanzania....Ona hapo, meza kuu yote wamejaa wahindi...Wabongo waliotumwa na mabosi wao wamekaa viti vya nyuma...Confidence Zero!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. Piga chini wanyonyaji hao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...