Wajumbe wa bodi ya taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo SAVE MT. KILIMANJARO , bwana Ernest Olotu na Godlisten Mamba wakiwa nje ya viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Tanzania mara baada ya kumalizika kikao cha bajeti ya Wizara ya mali asili na utalii pindi walipotembelea Bungeni hapo. Wadau hawa walipoulizwa juu ya ujuo wao Bungeni hapo, walisema ni katika harakati za kuelimisha umma wa watanzania ndani na nje ya nchi juu ya shindano la kusaka maajabu mapya saba ya asili ya dunia linaloendelea duniani kote na kushirikisha mlima kilimanjaro(Tanzania) na table mountains (South Africa) kwa upande wa Africa.Taasisi ya SAVE MT. KILIMANJARO ndio imeteuliwa na NEW 7WONDERS ,Kamati ya dunia ya kusaka maajabu hayo kusimamia elimu kwa umma na uhamasishaji wa kupiga kura kwa upande wa Tanzania.
Kwa kupiga kura tembelea; www.new7wonders.com au www.smk.or.tz



Bongo hivi sasa watu wameshajua jinsi ya kula kiungwana!!
ReplyDelete