Profesa Msambichaka
Na Lukwangule

Bodi ya Magavana ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii imewafukuza wahadhiri 21 wa chuo hicho kutokana na kuendesha mgomo unadaiwa sio halali. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana Profesa Lucian Msambichaka, amesema uamuzi huo ulifikiwa Agosti 17, mwaka huu baada ya kufanyika kwa kikao cha Bodi.

Kwa mujibu wa taarifa wahadhiri hao wamefukuzwa kwa kukaidi maagizo ya mamlaka za juu. 

Agizo la kutaka Taasisi hiyo ifunguliwe mara moja lilitolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye aliigiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inayoisimamia Taasisi hiyo kushughulikia suala hilo mapema iwezekavyo. 

Wahadhiri waliofukuzwa kazi ni Faustine Nzigu, Rindstone Ezekiel, Mariana Makuu, Aziel Elinipenda, Deodatus Mkumbe, Daud Chanila, Viscal Kihongo, Elizabeth Bitegela, Joseph Sunguya, na Constantine Njalambaya.

Wengine ni Mwajuma Hussein, Rita Minga, Caroline Mutagwaba, Elia Kasalile, Marwa Phanuel, Adrophina Salvatory, Kinswemi Malingo, Suzana Nyanda, Machumbana Michereli, Warioba Nyamoni na Yassin Mwita. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Safi sana Serikali,baadhi ya walimu hawa walikosa sifa za kufundisha muda mrefu na kuwa wakaidi kwa kiasi cha kutisha sana,Serikali inatakiwa iwe inachukuwa hatua stahiki pale mambo ya namna hii yanapotokea,kuna wengi ambao wana taaluma nzuri na wamefaulu masomo yao ya degree ya kwanza na pili vyema na wangependa kufundisha wapewe nafasi.

    ReplyDelete
  2. We mtoa maani wa kwanza, hebu acha kulolonga, maana hujui usemalo-umejaza hadithi tu zisizokuwa na kichwa wala mkia. Next time andika facts na siyo majungu. Labda kama una agenda za siri

    Kusema kweli Serikali kupitia hiyo bodi ya chuo haijawatendea haki hawa wahadhiri. Kama kuna watu wenye upeo katika hili suala (which i doubt) they have to rethink this decision. It's a dangerous path!

    ReplyDelete
  3. THOSE IN POWER WHO HAVE DECIDED TO OVERLOOK REALITY BY KEEPING THEIR FRIENDS IN PLACE AT THE COST OF AN OPPORTUNITY FOR EDUCATION FOR OUR SONS AND DAUGHTERS, WILL BURN IN HELL. THEY KNOW WHO THEY ARE AND THIS MOVEMENT HAS JUST STARTED. AT WORST WAACHENI HAO RAFIKI ZENU KWENYE MADARAKA LAKINI WABADILIKE BASI. VINGINEVYO, NEXT YEAR MTAFUKUZA ANOTHER BATCH OF 21. HAO WAALIMU TUNAWAELEWA MALALAMIKO YAO AND HONESTLY THEY HAVE A POINT, BE IT HAWAKUFUATA UTARATIBU. IN REALITY 1945, HAKUKUKUWA NA JINSI YA KUFUATA UTARATIBU KUMUONDOA HITLER.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...