BEATRICE MLYANSI NA ESTHER MUZE - MAELEZO

Watanzania wamehamasishwa kujitokeza kupigia kura Mlima Kilimanjaro ili uweze kushinda katika maajabu saba mapya ya dunia yatakayofanyika tarehe 11 Novemba 2011 Lisbon Ureno .

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dare es salaam Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Save Mt.Kilimanjaro Bw.Ernest Olotu amesema mlima Kilimanjaro ulipendekezwa kuingia kwenye mashindano ya maajabu saba mapya ya duniani . tarehe 7/7/2007.

Akielezea kuhusu mashindano hayo Bw. Olotu amesema shindano la Maajabu saba mapya ya duniani yalizinduliwa na shirika la New Open World Cooperation (NOWC) tarehe saba mwezi wa saba Lisbon Ureno ambapo kura zaidi ya milioni 100 zilipigwa kutafuta maajabu 28 mapya ya dunia.

Mwenyekiti huyo ameelezea kuwa vivutio 77 vilipendekezwa mwanzoni ambapo 28 vilipigiwa kura kuingia kwenye shindano hilo”,Afrika ikitoa nchi mbili Tanzania inayoshindanisha mlima Kilimanjaro pamoja na Afrika kusini inayoshindanisha Table Mountains.

Aidha Bw Olotu amesema Mlima Kilimanjaro una nafasi nzuri yakushinda kuingia katika maajabu hayo kama utapigiwa kura nyingi kutoka kwa watanzania.

“waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari mlioko hapa na wasiokuwepo hapa ni jukumu letu kuwahabarisha na kuwahamasisha Watanzania wote popote waliko bila kujali itikadi,dini ,rangi wala kabila kuonyesha uzalendo tushirikiane pamoja katika kupiga kura ili kuhakikisha Mlima Wetu unashinda”.alisema Bw.Olotu.

Amesema watu watakaotaka kupiga kura waingie kwenye tovuti ya www.smk.or.tz kupata maelezo ya kupiga kura au wanaweza kuingia moja kwa moja kwenye tovuti ya www.new7wonders.com.

Sambamba na mtandao namba za simu zitakazotumika kupiga kura kimataifa kutokea nchini ni +2392201055,+18697605990,+16493398080 na +447589001290.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. TUAMASISHWE KUPINGA UFISADI NAONA ITATUSAIDIA ZAIDI,KWA MAHANDAMANO.

    ReplyDelete
  2. Pamoja na kwamba mimi ni mtanzania sioni cha ajabu chochote kuhusu mlima kilimanjao. Kwa vigezo vipi?

    ReplyDelete
  3. Tujifunze lugha yetu. tuhamasishwe, maandamano.
    mdau naona unaendelea kubofoa yaelekea kiswahili kinakusumbua mno, jaribu kujipiga msasa.

    ReplyDelete
  4. Ni takribani miezi mitatu imepita tangu nitume habari kama hii kwenye blogu hii ya heshima ya jamii, nilifanya hivyo kwa kuwa naiheshimu sana blogu hii, kwa masikitiko makubwa habari ile haikupostiwa wala sijatumiwa email ya maulizo, ila kwa vile ni swala la kuomba hivyo nilikaa kimya tu. Leo ninafuraha sana kuiona imewekwa mbele ya jamii na blogu hii hii iliyopiga teke habari kama hii, sitaki kusema kuwa walipendelea 'no' sababu sijui kwa nini haikutila maanani labda ilionekana si ya kweli, au lugha haikuwa fasaha, aama ilipotea mtandaooni, au aliyeituma hajulikani. zaidi ya yote nimefurahi leo kuiona, ila pengine ingewekwa kipindi kile watanzania wengi wangepata nafasi ya kupiga kura maana kwa sasa muda nao umezidi kwisha kwani washindani wetu wakuu amabao ni South Africa wamepiga hatua kampeni ni kubwa hata wamefungila tovuti maalumu. Watanzania tupige kura kwa wingi, Idumu blogu ya jamii.

    wenu Mtanzania!

    ReplyDelete
  5. Sielewi kwa nini comments zangu hamzipost! sijatumia lugha ya matusi wala nini, ni kwa vile nimejaribu kuhoji ni kwa vipi habari niliyowaomba kuitoa(miezi 3 imepita) kwa umma wa Watanzania hamkuitoa? habari ya kuupigia kura mlima Kilimjaro, nilitoa details zote hata website ya 77 wonders nilitoa, ila mliitupa kapuni, au kwa vile hatujuani?? hiyo habari ni kwa manufaa ya Taifa letu sote, wenzetu Afrika kusini wameanzisha hadi tovuti yake kwa kivutio chao (Table mountain) Mungi awabariki! hata msipopost hii comment najua ujumbe mmepata.

    Mtanzania halisi!

    ReplyDelete
  6. How pleased I am to see Tanzania as one of the only two countries in Africa to be selected for 7 wonders. Pride, Pride...is the source of power, confidence, money.. almost everything!

    It is sad to see my fellow Tanzanians do no see the benefit of it. Yes, we have so many problems but that doesn't forbid us from exploiting our strengths, and Kilimanjaro has been spotted as one of them. Please, vote for Kilimanjaro!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...