Waziri Mkuu,Mizengo Pinda (katikati) akielekea kuzindua rasmi ujenzi wa nyumba za makazi za Medeli,zilizopo mjini Dodoma leo.kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC),Nehemia Mchechu,akifuatiwa na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Prof. Anna Tibaijuka na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHC,Eng. Kesogukewele akifuatiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania,Anne Makinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikata utepe kwaajili ya uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za makazi za MEDALI,mjini Dodoma leo. (kushoto) Ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. AnnaTibaijuka
Baadhi ya Wazee wa mji wa Dodoma wakifurahia hotuba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani) aliyoitoa wakati akizindua rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ziliopo MEDALI Dodoma leo.
Wasanii wa kikindi cha Mjomba Band wakitumbuiza katiak sherehe hiyo ya Uzinduzi rasmi wa ujenzi wa nyumba za makazi za MEDALI Dodoma leo.
Baadhi ya watoto waliohudhuria katika uzinduzi rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba,za makazi ziliopo eneo la MEDANI Dodoma, Mradi wa ujenzi utagharamiwa na shirika kutokana na mikopo ya kutoka taasisi za fedha za hapa nchini, Mradi huu umebuniwa na shirika la nyumba na lengo lake nii kupunguza tatizo la makazi kwenye mji huu mkuu wa nchi yetu, (Picha na Mwankombo Jumaa-MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hakuna tunachoshindwa Tanzania yani nyumba izi zinawezekana kuwepo nchi nzima sema tu, siasa za matumbo ndo zinatykwamisha. ila tukiamua tunaweza. Mungu ibariki Tanzania Mungu wabariki watanzania

    ReplyDelete
  2. Ankal hapa kwenye blog ya jamii kuna articles ambazo wakati mwingine hazieleweki kutokana na 'typo' na hivyo maneno mengine kutoeleweka. Watu wajitahidi kabla ya 'kuposti' wapitie yale waliyoyaandika ili yawe sahihi.

    ReplyDelete
  3. Nisikizie baadae magorofa yatakavyochafuka - maji na umeme wa mgao. Tuombe Mungu migao itokomee kabisa.

    ReplyDelete
  4. Naona tunakoelekea ni kwenye utamaduni wa kuwa na estates kama kwa watani wa jadi. NHC 'YES YOU CAN! Achaneni na historia mbofu mliyorithi, pigeni mzigo hata mkila vizuri mle hela yenu isiyo na majotroo! Imagine NHC yenye estates kila mji/jiji/manispaa nchini, kuanzia low income, mid income, na wenye vijisenti plus investments za highrise office/residential blocks...! Haya mambo yanawezekana, tatizo tunakimbilia kula kwanza kabla ya kazi. Mi hakyanani mtu akiniibia na kazi akafanya nikaiona, namsamehe!

    ReplyDelete
  5. Yaani, Rais wetu mpendwa ungekuwa umeitendea haki Tanzania ungekuwa umeanzisha shule za Kata kila kata, na kujenga nyumba za walimu pia, ili waalimu wapate motisha ya kuwa na uhakika wa mahali pa kukaa. Siyo unampeleka mwalimu kijiji kisicho hata na nyumba moja. Mbona nyumba za wabunge Dodoma zinajengwa? Na wabunge wenyewe hawakai mule kwenye zile nyumba, kwa nini msingejenga nyumba kama hizo kwa ajili ya waalimu, kila penye shule???

    Jiji la DSM linatakiwa zijengwe nyumba kama hizi, bomoeni slums humu DSM, magomeni, mikumi, Mhurahati, manzese...jengeni nyumba kama estates watu wapangishe wakae mule...nyumba ndogondogo na zisizo na mpangilio zinazojengwa jijini zinazidi kuharibu sura ya jiji. Hivi hamwendi Uingereza na nchi nyingine mkaona mifano? Badilisheni mfumo na sura ya miji yetu. Msile fedha, fanyeni kazi kwa ajili ya kizazi hiki na kijacho!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...