Ndugu Michuzi, naomba uwaambie watu wa DAWASCO hili shimo liko wazi kwa muda mrefu sasa zaidi ya  mwezi . Picha namba 2 inaonyesha shimo likipungua kidogo maji machafu ya choo. Picha ya pili ni kuonyesha njia ambao watu wanapita , ni kama inchi 20 kutoka kwenye shimo. Likiwa Halina maji shimo ni refu sana karibia futi zaidi ya 12. Je,  DAWASCO wanataka mtu afe ndio wazibe? Shimo liko karibu na kwa Kakobe, karibu na baa inayoitwa cafeletino. 

Tuna wasiwasi mkubwa hili shimo linaweza likaleta kilio kwa aidhaa familia iliyokaribu na hilo shimo au watumiaji wa hiyo baa au wapiti njia. Hivi lazima aje mtaalamu kutuoa ushauri wa kuweka kifuniko? Nasema hivi, kama ukitumbukia kwenye hili shimo, hakuna njia yeyote utakayoweza okolewa ukiwa hai.  DAWASCO ndio waliojenga hili shimo/chamber ambayo inapokea maji machafu kutoka mlimani city na wakazi wengi waliokaribu na Mlimani city. Naomba kupita hii website yako, uwaambia uongozi wa dawasco kuwa kama itatokea tatizo  lolote watawajibika. 

Labda uongozi wa juu utatoa agizo liwekewe kifuniko lakini, watu wanataka washughulikie baada ya matatizo kutokea. Nadhani utaokoa maisha ya wapendwa wetu kwa kufikisha huu ujumbe kwa uongozi wa DAWASCO. Shimo liko wazi kwa zaidi ya mwezi sasa lakini kama litaleta mahafa ninasema kesho yake litafunikwa. Hivi kwanini tukumbushwe kila kitu? Tena ilikuwa hatari zaidi maana ukiangalia vizuri hiyo picha kunamtu aliweka bati eti kuzuia mtu asitumbukie tena bati lililooza. Hivi mbona tunaleta mzaa kila mahali hata kwenye maisha jamani? 

Mungu akubariki
Mkazi Sinza



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huwezi amini hapo mahala pana baa maarufu, wanataka sie tudumbukie humo waseme eti tumelewa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...