HAYA NDIO YALIYOJIRI UK NA FUJO BADO LINAENDELEA LIMEHAMIA MANCHESTER KUTOKA LONDON BIRMINGHAM BRISTOL NA HUENDA LIKAFIKA HADI LEEDS. maduka na magari kuchomwa moto na kuporwa utafikiri mageuzi ya nchi za kiarabu.
 Mwanamama akiruka toka katika nyumba inayoungua
 Maduka yamechomwa moto
Vijana wakivunja maduka
Moto kila mahali katikati ya jiji la Manchester. Ndugu zetu Watanzania mko Salama huko? Tunawaombea manusura

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Wana bima hau walipwa!

    ReplyDelete
  2. TUKO SALAMA
    Inatisha kidogo, tupo hapa si mbali sana na Manchester.
    Leo tupo nyumbani,tumemaliza swaumu saa mbili na dakika hamsini
    Tunaangalia vurugu hizo kwenye TV
    Hapa nilipo naona hata magari njiani yamepungua
    Hatuna khofu
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  3. michuzi hali bado tete huku uk ukitoka umekwisha

    ReplyDelete
  4. Tuko salama wandugu, ila mambo magumu sana. sasa hivi wengi wetu tupo ndani muda mrefu. Mtuombee wapendwa.

    ReplyDelete
  5. acha mambo yako wewe haya mambo ya kawaida sana kwetu sisi wabongo tumeyazoea sindio mtayo kutana nayo kila siku so hakuna kipya wacha wachome nchi si yao na nifaida kwetu next month kazi za constraction zitakua nyingi kinoma so wamatumbi tutaendelea kumake moniooooooo

    ReplyDelete
  6. acha zako wewe unayetaka kupunguza ukali wa hayo mambo yanayo tokea uingereza hivi sasa kwa kusema eti ni mambo ya kawaida. hayo si mambo ya kawaida hata kidogo na acha kufananisha bongo na uk. waingereza hasa media zao waache kucheka nchi za watu wakiwa na fujo. sasa angalia mambo yame wageukia.

    ReplyDelete
  7. tupo salama ila kutembea usiku ni kasheshe. Kama leo nimepata shida kweli mitaa ya birmingham

    ReplyDelete
  8. Si waombe Tz iwapeleke FFU wetu huko? Hawakuona jinsi wanvyowadhibiti CHADEMA?

    ReplyDelete
  9. wafanye wafanyavyo ila wasifike north london kwa washika bunduki the gunners kitongoji sha ashbaton grove! emarates!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. Litasambaa mpaka bongo hili kama limetokea kwenye nchi ya waungwana duniani, basi ujue lipo njiani likielekea bongo ukiangalia kama bunge lilivyo na wendawazimu, hakuna umeme hakuna mafuta, ni kiza kinene tanzania, viongozi wanashindwa kutoa maamuzi magumu! Umebakia usanii tu. Inatisha wananchi wanaelekea kuchoka zaidi na uzalendo utawatoka! Tanzania inahitaji turning point tunakoelekea sio kuzuri!

    ReplyDelete
  11. haya wabeba boxi wakuu kazi kwenu kimenuka londoni mtakimbilia wapi maana huwa mnaponda kwenu

    ReplyDelete
  12. Mimi naona hiyo ni njema, inawafundisha viongozi kuwa cyo tu kuvagaa mambo ya watu wa nchi zingine wakati na wao wana matatizo yao, wanamuonea Gaddaffi sasa wananchi wao wawafundishe adabu..japo nasikitika kuwa watu wa kawaida ndiyo wanaathirika zaidi..!

    ReplyDelete
  13. Michuzi hakuna picha nyingine za wazungu wakibomoa maduka? au ndo kusema wamatumbi ndo shughuli zao huko? Na hapa nakubaliana na media kwamba ni wahamihaji ndo wanaosabasha fujo na uhuni. Je salama yao ni vipi baada ya kuisha kwa vurugu hizi au ndo wenzetu watarudishwa home? Jamani karibuni sana home kwani picha inaonnyesha kwamba wamatumbi bado kabisa ama la Michuzi tuwekee nyingine za wazungu basi.

    ReplyDelete
  14. Waingereza ni wabaya zaidi kuliko hata TZ ndio maana watu wao hawakusubiri sheria ichukue mkondo wake. Watu hawa kwanza wana kitu kinaitwa umoja, pili wana kitu kinaitwa "back stabbing" maana yake wanakufanyishia wakati wewe mwenyewe atakapokuwa huoni au huna habari. Ili mambo yako hapa UK yawe mazuri siku zote useme kile anatotaka kusikia mzungu. Mfano black yeyote ambaye mambo yake ni mazuri atasema wanaoandamana na kufanya fujo ni wahuni, hatosema hata siku moja kama polisi ni wabaguzi na serikali ichukue hatua. Huyo atakayesubutu kusema kuwa polisi ni wabaguzi basi kama anakazi nzuri watamfatilia mpaka wamfukuze, kama kulikuwa na jambo lolote lile zuri wanamharibia, polisi pia watakuwa wanamfuatilia watafute jambo lolote lile hata kama kumuwekea ushahidi wa uongo watafanya ili wamfunge, kwa hiyo UK watu wake hawana demokrasia yoyote na huo uongo wanaousema kuhusu sheria zao ikitaka kuzitumia tu basi uwe muangalifu.

    ReplyDelete
  15. Tofauti kati ya UK na Arabuni, ni kuwa hakutakuwa na maazimio ya UN kulaani tabia ya polisi wa UK kuua watu weusi wasio na hatia..

    ReplyDelete
  16. Hali ni shwari huku hakuna shida kwa sisi waTZ, kwanza kila fujo zinapoongezeka sisi watoto wa mbwa ndo tunapata pa kutokea, wache wapigane thereafta tupige mzigo wa deiwaka. haina mbway mgosi

    ReplyDelete
  17. Naombeni watanzania msije mkajaribu fujo kama za UK. Hatuna pesa ya kulipa hasara itakayopatikana. Kama serikali inakosea, tuendelee tu kuishinikiza hadi hapo itakapofunguka masikio. Uzuri ni kwamba serikali zetu zinatawala miaka mitano uchaguzi unafanyika. So, poeni kidogo neema itakuja. CCM tumejipanga kuwaletea maisha mazuri.

    ReplyDelete
  18. Nyie wamatumbi mliopo huko uk msijifanye hayo mambo yanawahusu msijihusishe kiuongo hayo mambo yana wenyewe nyie subirini mpewe hela za mwezi bila kufanya kazi hela za kikimbizi au wengine mkabebe maboks msijifanye na nyinyi kama hao wajamaica au warabu wa ulaya hao wenzenu wapo huko miaka mingi kabla hata nyerere hajaacha kutulisha mahindi ya njano

    msiige tembo kukamua kilo 10 kwa njia ya....

    ReplyDelete
  19. Nimeona picha kwenye interenet zinaonesha watu weusi tu. Ina maana hizo fujo ni watu weusi peke yao au wapo na wenye nchi yao? Hatima yake itakuwa nini? Wabongo jitahidini kujiepusha na hilo janga kwani mkirudi home hali hata huku sio nzuri. Tunategemea mtupige tafu kwa senti mnazopata huko. Tunawaombea msije mkarudishwa bongo kwa kisingizio cha fujo.

    ReplyDelete
  20. Anzisheni blogu zenu za kuweka picha za watu weupe wakifanya fujo.. acheni kuwalaumu wazungu wakiweka picha za weusi wakati ninyi hamfanyi za oppsite!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...