NA NAFISA MADAI -MAELEZO,ZANZIBAR
WIZARA ya kilimo mali asili zanzibar imepiga marufuku uingizaji wa bidhaa ya ndizi,miche ya migomba,majani ya migomba pamoja vigogo vya mgomba kutoka tanzania bara.
WIZARA ya kilimo mali asili zanzibar imepiga marufuku uingizaji wa bidhaa ya ndizi,miche ya migomba,majani ya migomba pamoja vigogo vya mgomba kutoka tanzania bara.
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari huko ofisini kwake mwanakwerekwe wilaya ya magharibi, mkuu wa kitengo cha uhifadhi na utibabu wa mazao, Bi. Zainab Saliim Abdallah amesema taarifa hiyo imefuatia na kuibuka maradhi mnyauko ambayo yanasababishwa na bakteria katika migomba huko tanzania bara.
Aidha amesema maradhi hayo tanzania bara yameingia tokea mwaka 2007 lakini kama idara inajukumu la kuwakumbusha wananchi wa zanzibar kwa vile kipindi hiki cha ramadhani walaji huwa wengi zaidi kuliko siku za kawaida.
Hata hivyo alisema maradhi hayo hayana athari kwa mlaji bali athari kubwa anaweza akaipata mkulima wa zanzibar endapo bidhaa hiyo ikizidi kuingia chini kwani alisema huwenda ikamsababishia hasara kubwa mkulima huyo kwa asilimia mia moja.
Bi Zainabu aliwaomba wanzanzibar kutoa mashirikiano makubwa na kuwatafuta wale ambao bado watakwenda kinyume na agizo hilo ili kuweza kudhibiti uingizaji wa bidhaa hiyo.
Sambamba na hayo Bi Zainabu alisema mtu yoyote ataekamatwa anahusika na uingizaji wa bidhaa hiyo kutoka bara atafikishwa katika vyombo vya sheria na sheria itashika mkono wake kwa muingizaji huyo.
Amesema kitengo chake tayari kimeshakamata ndizi ambazo zimebainika na maradhi hayo kutoka bara na mipango inaandaliwa kuangamiza ndizi hizo ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanampango wa kuingiza ndizi zanzibar.
Akizungumzia nzi wa matunda,Bi Zainabu amesema nzi hao hivi sasa wameshamiri sana zanzibar na wanashambulia embe kwa kiasi kikubwa jambo ambalo limekua likiwavunja moyo wakulima wa zao hilo visiwani zanzibar.
Aidha alisema nzi hao ambao chimbulo lake ni nchini indonesia wamekua wakileta hasara kubwa kwa wakulima kwani soko limekua dogo sana ukilinganisha na hapo awali.
Hata hivyo alisema juhudi zinafanywa za kuangamizwa nzi hao za kuwawekea mitego maalum na kwasasa tayari wameanza katika wilaya ya kusini na wamefanikiwa kwa asilimia hamsini ambapo zoezi hilo linategemewa kufanya katika mikoa yote ya zanzibar.
Bi Zainabu pia alizungumzia mende wadogo ambao nao wameshamiri kwa wingi katika visiwa vya unguja amesema mende hao wanaathiri sana katika makaazi ya watu kwani hushambulia nguo na vitu vyengine majumbani.
Amesema kuwa mende hao wametokea ulaya na wamekuja kutokana na vifaa vya umeme ambavyo vimezagaa katika manispaa ya mji wa zanzibar.
Aidha alisema juhudi za makusudi zinachukulia za kutokomeza mende hao maarufu mende wa ulaya, na kuwaasa wale wote wanaofanya biashara hiyo ya vifaa vilivyokwisha tumika kuangalia kwa makini vifaa hiyo kwani athari yake baadae inaweza kuwa kubwa zaidi.
UTAFITI WA KISAYANSI UNASEMAJE KUHUSU MAGONJWA YA NDIZI? JE NI TZ BARA TU AU KUTOKA MAENEO MENGINE PIA? TOA NA EVIDENCE BASI ILI UZUIAJI WAKO UONEKANE NA USHAHIDI WA KISAYANSI. AU UNA YAKO TU WEWE!
ReplyDeleteChuki binafsi hizo. Magonjwa ya ndizi hayapo bara tu hata Malawi, Kenya, Uganda, Msumbiji n.k. Hata zanzibar kwenyewe huo ugonjwa upo.
ReplyDeletekama hazina mazara kwa mlaji wacha ziingie kwa kuwa zinaliwa ila kama ni miche basi isiingie Huyu mama hana akili sasa kwani mgomba unaoteshwa na kinyesi? yaani mtu akila ndizi na kwenda haja ndio anapanda? sasa si aseme miche tu izuiliwe na sio ndizi kama alivosema kuwa hazina madhara?
ReplyDeleteHao mende kila summer tuwanakuwepo na mbona wanakuwepo stone town tu Wafanye uchunguzi mwengine sio waropokwe tu
Bado Pwani kukataza ndizi kutoka Morogoro na Dodoma kukataza kuingiza mbuzi kutoka Singida!!!!!!!!!
ReplyDeleteWewe mdau unayezungumzia mtaalamu wa utibabu wa mimea kuwa hana akili, ni weewe ndiye mjinga kabisa kwa vile siyo mtaalamu wa fani hiyo.
ReplyDeleteMaganda ya ndizi na hata ule mkungu unakuwa na bakteria hao na ndiyo wanaweza kusambaza pindi vikiwekwa karibu na miche ya migomba.
Aina hiyo ya uzuiaji mimea ili magonjwa fulani yasiingie nchini (quarantine) huwa inatumika sana kwa mimea duniani kote na ina ufanisi mkubwa. Mfano ni ugonjwa wa minazi (lethal yellows) ambao huko bara umeshamiri lakini kwa sababu ya karantini wameweza kuzuia ugonjwa huo usiingie Zanzibar.
Hapo hakuna chuki wala wivu ila ni kufuata procedures za quarantine. Na hata kwenye mifugo huwa quarantine inatumika.
Tusitukane ila kweli Tz ndizi zile za asili hakuna, hata ukienda moshi vile vindizi vidogo vitamu vinaitwa ndizi kisukari hakuna kuna vingine vinaitwa kisukari ulaya mabaya sikuyapendi na zimefanyiwa research na wanasayansi hawa (wanaotumia mabinti zetu ulaya kama mtumwa)na kuziona si ni nzuri wakati hata sokoni haziuziki. Pia ndizi mshare wachaga mnazijua maana sijui kama mikoa mingine inaita the same name zote zimebadilishwa na kuwepo za ulaya. Na mimi huku Ulaya sijawahi kuona wakilima ndizi wanakuja kufanya jaribio tu huko na kuwaachia uchafu vile bongo tambarareeeeeee. If so why Zanzibar ikubali huo uchafu???? Maana naona wenzetu wanatunza vitu vyao vya zamani ila Tz honestly you do sometimes take rubbish. Come on wakulima Open u r eyes tunataka kujifunza kwenu please. Hongera kwa Zanzibar kama wanakataa ndizi za ulaya but if is ukorofi tu chonde chonde.
ReplyDelete