Gari ya abiria aina ya Hiace yenye nambari za usajili T219 ASW ambayo ilikuwa ikitokea mji mdogo wa Tunduma ikielekea Jijini Mbeya iligongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Prado yenye nambari za usajili T155 ACQ, majira ya saa mbili unusu usiku jana.
Watu wakiangalia gari aina ya TOYOTA Prado Hiace yenye nambari ya usajili  T155 ACQ ambayo iligongana uso kwa uso na gari ya abiria aina ya     Hiace yenye nambari ya usajili T219 ASW ambayo ilikuwa ikitokea mji mdogo wa Tunduma ikielekea Jijini Mbeya jana saa mbili unusu usiku.
Watu wakiangalia gari aina ya TOYOTA Prado Hiace yenye nambari ya usajili  T155 ACQ ambayo iligongana uso kwa uso na gari ya abiria aina ya     Hiace yenye nambari ya usajili T219 ASW ambayo ilikuwa ikitokea mji mdogo wa Tunduma ikielekea Jijini Mbeya jana saa mbili unusu usiku. Picha Na Mbeya Yetu 



Na Francis Godwin

MATUKIO ya ajali za barabarani yameendelea kukatiza maisha ya watu, hususan katika wiki hii ya Usalama Barabarani. 


Jumla ya watu  tisa  wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali iliyohusisha basi dogo la abiri (Hiace) kugongana uso kwa uso na gari aina ya Landcruiser(Prado) katika barabara ya Mbeya- Tunduma.


Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimoro, akizungumzia ajali hiyo amesema ajali hiyo imetokea Septemba 28 mwaka huu saa 1;30 katika kijiji cha Chimbuya wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.Kimoro alisema ajali hiyo ilihusisha basi hilo aina ya Hiace lenye namba za usajili T 219 ASQ ambayo iligongana uso kwa uso na Prado lenye namba za usajili T 155 ACQ. 


Alisema dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo alishindwa kumudu mwendo hivyo alikuwa akiyumba kutoka upande wake hadi upande wapili ambako aligongana uso kwa uso na gari hilo lililo kuwa likielekea Tunduma kutokea Mbeya .


Kimolo aliwataja waliokufa na ambao tayari wametambuliwa na ndugu zao kuwa ni Anna Mbembela na mwanaye Mariam Mrema, na Rahabu Mwaijumba na mwanaye Leah Said.


Aliwataja wengine waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Binaisa Mwashiuya, Baraka Mwansite na dereva wa Hiace ambaye hajafahamika jina lake, na mwingine Agness Mpoli alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.


Alisema majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya Vwawa ni Frank Simbeye (25) mkazi wa Chimbuya,Emanuel Sanga (16) mkazi wa Mlowo,Agness Anthony (28) mkazi wa Mbeya na wanaye wawili Jackiline Christopher na Victor Christopher.


Majeruhi wengine ni Anastazia Mtumbo (19) mkazi wa Tunduma na Richard Ezekiel ambaye ni mtoto wa miezi 10 na Chenny Mwembe (25) mkazi wa Chimbuya. 


Watu walioshuhudia ajali hiyo wamedai kuwa basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Charles Kumbi wakati Prado lilikuwa likiendeshwa na mmiliki wake Emanuel Kaila ambaye amelazwa katika Hosptali ya Sifika mjini Vwawa akipata matibabu kutokana na kujeruhiwa vibaya. 


Wamesema pia kuwa katika eneo hilo kulikuwa na trekta ambalo lilikuwa limebeba tanki la maji na ambalo halikuwa na taa na kwamba dereva wa Basi dogo alitaka kulipita.Imeandikwa na Moses Ng'wat na Esther Macha kutoka Mbeya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...