UONGOZI WA GLOBU YA JAMII UNAPENDA KUOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE ULIOPATIKANA BAADA YA KUCHAPISHA PICHA HIYO HAPO JUU MARA TU BAADA YA HABARI ZA KUZAMA KWA MELI YA MV SPICE ISLANDER ILIPOTUFIKIA. BAADA YA UCHUNGUZI WA KINA NA KWA MSAADA WA WADAU KADHAA WANAOITAKIA MEMA GLOBU YA JAMII, IMETHIBITIKA KWAMBA PICHA HIYO ILIYOLETWA NA MDAU SIKU HIYO NI YA MELI YA TRANS-ASIA SHIPPING LINES YA MALAYSIA ILIYOZAMA MNAMO JULY 31, 2011 NA SIO MV SPICE ISLANDERS.


GLOBU YA JAMII HAINA JADI YA KUJITETEA AMA KUTAFUTA VISINGIZIO. ENDAPO IMETOKEA KWIKWI INAKIRI MOJA KWA MOJA KUWA IMEKOSA BILA KUTAFUTA MCHAWI AMA KUMTAJA NANI KAFANYA KOSA HILO ILI KUPUNGUZA SOO, KWANI UONGOZI NA TIMU NZIMA PAMOJA NA WADAU NI KITU KIMOJA. TUKIPATIA TUNAKUWA TUMEPATIA WOTE NA TUKICHEMSHA NDIO HIVYO TENA..


HIVYO KWA HESHIMA NA TAADHIMA TUNAOMBA RADHI SANA KWA KOSA HILO LA KIBINADAMU. TUNAKIRI UDHAIFU KWANI HAKUNA ALIYE KAMILI ILA MOLA TU.


NA ILI KUTHIBITISHA KUWA HII MELI HAPO JUU PICHANI SI MV SPICE ISLANDER
BOFYA HAPA


-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Vyombo vya vimewapeleka markiti wasanii wa Zanzibar walioimba wimbo wa kuwaenzi waliopoteza maisha katika meli husika kama inavyoonekana katika blogu yetu hii. Wametumia hii picha. Kwa mtazamo wangu, vyombo vya habari ni kama mabenki tu, vinapaswa kuwa makini sana katika kazi zao maana athari za makosa yao zinaweza kuwa kubwa sana.

    Mhariri asiye rasmi.

    ReplyDelete
  2. Hapo kweli Bwana Michuzi, michuzi uliikoroga kweli.

    ReplyDelete
  3. Umesamehewa kaka ila siku nyingine uwe makini.

    ReplyDelete
  4. mh, pole kaka michuzi, but am just suprised na namna ambavyo picha hii ilikua imesambaa kila mahali, in facebook kuna taarifa nyingi watu walikua wakibadilishana kuhusu hii ajali wakirefer picha hii, its very suprising!pengine kama unaweza kufanya jitihada kama inawezekana kupata image halisi ya io meli yetu iliozama, not important though, na may be ni changamoto juu ya source yako ulipopata hii pic, this incident is not damaging, but in the future, you might find our self in trouble kwa kosa kama hili, ni ushauri tu

    ReplyDelete
  5. Bongo tambarare!

    ReplyDelete
  6. Nimeona hii picha imewekwa mpaka kwenye video ya kuwaenzi wale walioadhirika na kuzama kwa meli ya Spice Islander. Yaani huu ni mchemsho wa hali ya juu. Ina maana hata wale wanao regulate the music industry hawajaona hii hiyo video? Kwa staili hii tutazama wengi.

    ReplyDelete
  7. Mimi nasema hivi michuzi wala wadau hatuja koroga, kwasababu lengo nikuonyesha Meli inavyozama na siyo lazima iwe exactly Meli husika hapana katika uandishi wa habari hayo yanafanyika sana na mimi sioni tatizo, je ujumbe wa meli kuzama haukufika? ulifika tena vizuri tu, hamna kilicho haribika kabisa,ila tu mmoja angeweza kusema huu ni mfano wa meli iliyozama ya spice au la hakusema si vibaya hivyo kama mnavyotaka kusema, mara nyingi tu, waandishi tunafanya hayo, mfano rais kikwete ametoa salamu za rambirambi kwa fulani, tunaenda tu maktabu na kuchukua picha ya rais yenyekuonyesha huzuni tunaweka katika gazeti, au soko la mbeya lina ungua (sisemi ile nayo ilikuwa picha tofauti hapana), tunaenda tu maktaba tunachukua picha ya lilipoungua soko la songea tunaweka, kitu muhimu ni ujumbe ambao picha hiyo inawakilisha sawa jamani msio waandishiwa habari, mimi nawapa siri hiyo, kwa hiyo hii siyo issue kabisa, na mara nyingi inatokea hivyo kama picha ya kitu husika haiwezikupatikana haraka.Ok!

    ReplyDelete
  8. wadau mbona ile meli ilizama usiku! hapa mchana

    ReplyDelete
  9. halafu watu kibao wakaja kunyofoa hii picha humu na kuhamishia kwenye blog zao, yani ingekuwa ni mtihani watu wangefeli kwa kukopi makosa ya mtu wa kwanza.

    ReplyDelete
  10. We mdau 040:4:00 acha siasa. Meli imezama Inaitwa X, unaweka picha ya Meli Y inayozama, tena nchi nyingine si sawa na unavyosema. Mfano Kikwete anaenda kutoa rambirambi, unaweza kuweka picha ya Mandela anasikitika? Niliweka comment siku ya pili kuwa hii picha siyo, sijui ikawaje..
    cha msingi ameomba radhi. Libeneke linaendelea

    ReplyDelete
  11. Kuomba radhi kwa kuapa au kudhamilia kutokufanya makosa tena ni uungwana ambao unakubalika katika jamii pindi unapogundua umefanya makosa ambayo hukutegemea kuyafanya. Kuomba radhi kunakuwa na maana kamili itayokubalika katika jamii pale unapokuwa hujarudia kosa kama hilo. Tatizo nchini, tuna vyombo vya habari ambavyo vingi havijui madhara yatokanayo na habari zisizo hakikiwa vizuri, na kama vinafahamu, basi vinatumia mapungufu yaliyopo katika muundo wa sheria ya vyombo vya habari ili kujinufaisha.
    Demokrasia bila uhuru chanya wa vyombo vya habari siyo demokrasia huru, vile vile uhuru wa vyombo vya habari visivyo na mipaka ni kichocheo cha mitafaruku katika jamii ambayo mwisho wake ni miparanganyiko katika hiyo jamii.
    Hatuwezi kujua na kupima habari hii imefanya uharibifu gani katika jamii hasa kwa wale ambao wameguswa hasa na taarifa hii, lakini tunalolijua ni kuwa imefanya uharibifu kwa kutoa taarifa ambayo ndani yake imeongezwa ''chumvi''.
    Demokrasia ya kweli katika habari inajengeka katika jamii yenye soko huria katika vyombo vya habari ambavyo misingi yake inakuwa imejengwa na serikari na wananchi wake.
    Hatuwezi kukaa hapa na kuvilaumi tu vyombo vya habari. Vyombo vya habari katika jamii yenye demokrasia ya kweli kama tujuavyo vipo siyo tu kwa ajiri ya kupasha habari na kuielimisha jamii bali pia kwa ajiri ya kuwa na uwezo wa kujiendesha kibiashara. Serikari ni taa ambapo pia ni mwongozaji na msimamizi wa vyombo vya habari kwa mujibu wa sheria.
    Mwalimu nyerere alisema katika kitabu chake cha Uongozi wetu na hatima ya Tanzania kuwa Chama legelege huzaa serikari legelege. Mimi ninasema, Wananchi legelege huzaa vyama vya siasa legelege ambavyo huzaa serikari legelege, kinyume chake pia ni kweli.
    Mpaka hapo wananchi watakapojua wajibu wao na nafasi yao katika vyombo vya habari, tutabakia na kuendelea kupata habari ambazo hazina uchunguzi fasaha.
    Hata hivyo, kesi kama ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye dhidi ya magazeti ya Mtanzania na Rai imeonyesha kuwa kule tunakoelekea barabara imeanza kuwa na mwanga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...