Ankal akila konozzz na Mamou, bintiye anayepiga kitabu kidatu cha tano katika shule ya sekondari ya wasichana ya Babro Johansson iliyoko maeneo ya Luguruni nje kidogo ya Dar es salaam. Shule hii, ambayo hupokea waliohitimu vyema katika mtihani wa kidatu cha nne kwa kupata Division One, imepewa jina la Mama Barbo kutoka Sweden ambaye aliipenda mno Tanzania kiasi cha kuchua uraia. Na mfuko wake wa Joha Trust ndio unaofadhili shule hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti Mwanzilishi Profesa Anna Tibaijuka wakati Mzee Paul Rupia Ndiye mlezi wake pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mh Solomon Odunga. Mama Halima Kamote ndiye Mwalimu Mkuu na Mkuu wa Utawala. Tembelea tovuti yao BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Tehe teh tee tee!

    Kaka nakuonea huruma wewe kwani umejitafutia balaa mwenyewe!
    Subiri sasa wakishaamka wale jamaa zetu wale, maana saa hizi kwao ni usiku bado wamelala. Tehe teh tee te!

    Ila ana MGUU MZURI!

    ReplyDelete
  2. Michuzi ubaya unautangaza mwenyewe..
    Sasa usije "ukatu-Babu Seya" ..wakware sisi tukimtembelea binti kumsalimia hapo shuleni.
    Tunashukuru sana kwa taarifa.. Tutaifanyia kazi soon!

    ReplyDelete
  3. HONGERA SANA ANKAL UMENIKOSHA SANA HII NI KUONYESHA KUWA UNAIJALI FAMILIA MPE BIG UP MWANA NA APIGE KITABU CHA NGUVU ZAIDI TUNA MTEGEMEA AJE KUWA KAMA MAMA DR ASHA ROSE MIGILO NI KUMPA MOYO TU HAKUNA KINACHOSHINDIKANA AKIKAZA BOOT LA KUSOMA ALSO HONGERA MMEFANANA SANA - mdau Richie wa ughaibuni

    ReplyDelete
  4. naona ankal binti yetu anachekelea kibahasha hicho mkononi utakachomwachia!!!!!hehe
    Mdau wa IT

    ReplyDelete
  5. Ankal naona ulikuwa mpenzi sana wa TP OK JAZZ ndio maaana umemwita bintiyo jina la MAMOU. Namtakia kila la kheri Mamou katika harakati za Elimu.

    KALLEY.

    ReplyDelete
  6. Kuna haja ya kuanza kujua ratiba za visiting za babro.....teh teh teh....

    Hongera ankal kwa kurithisha wanao kile chenye kheri na manufaa kwao - elimu bora.......

    ReplyDelete
  7. Michuzi mnunulie viatu binti yetu manake naona mguu wa kulia kamba za viatu zimekatika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...