Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omari Nundu (kushoto) akikata utepe kuzindua boti 4 leo katika bandari ya Dar es Salaam akiwa na Naibu Wake Mhandisi Athmani Mfutakamba (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara yake Mhandisi Omari Chambo (kulia)Uzinduzi huo ni katika maadhimisho ya miaka50 ya Uhuru kwa Wizara ya Uchukuzi
Sehemu ya wafanyakazi wa TPA wakiwa katika hafla hiyo
Hizi ndizo boti zilizozinduliwa leo katika Bandari ya Dar es Saalam. Boti kubwa mbili ni za kuongoza meli na ndogo ni kwa ajili ya kuwapeleka mapailot na kufanya doria. Shughuli zote hizi zimefanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika maadhimisho ya miaka ya uhuru kwa sekta hiyo ya Uchukuzi
Kweli Wanawake wakiwezeshwa Wanaweza! Hii ni leo Sept,16,2011 katika Bandari ya Dar es Salaam wakati Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omari Nundu (hayupo pichani ) alipozindua Boti za doria. Juu pichani ni mwanamke pekee Mhandisi katika Tagi la Nyangumi, Bi. Maisara Rumani ( katikati) akiwa na Mhandisi Sifuel Felix (kushoto) pamoja na Mhandisi Nicholus Mfumgomara
Meneja mawasiliano wa TPA Frakline Mziray (kulia) akiwa na msanii mkongwe wa muziki nchini Mzee Muhidini Maalim Gurumo zalikuwepo kutoa burudani na bendi yake ya Msondo Ngoma Jazz Band
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Athmani Mfutakamba (kushoto) akizindua eneo la ujenzi ,wa kutunzia makontena( GEREZANI CREEK CONTAINER YARD) ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo katika eneo la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania jijini Dar es Salaam. Mwenye suti nyeusi Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omari Chambo ambapo kulia ni Meneja wa Mawasiliano wa TPA Bw. Franklin Mziray
Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omari Nyundo (katikati) akizindua huduma kwa mteja kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandar Tanzania leo. Mkurugenzi Mkuu wawa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Ephraim Mgawe,(kushoto), kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Athumani Mfutakamba akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omari Chambo,Ni katika shamrashamra za Maadhimisho ya ,miaka 50 ya Uhuru katika sekta ya Wizara ya Uchukuzi. Picha zote na Mwanakombo Jumaa wa Maelezo
hizi boti zimeingia lini maana wakuu wabongo wakishaona ajali ndowanaanza sera zao kama zingikuwepo tangu zamani mbona ajali isingetokea huko pemba yani inatia uchungu kwakweli hajali ishu za wananchi mpaka litoke janga kubwa ndo wanaanza kujishauwa yani bongo kazi kweli2 haya ngoja tuone hizo boti zinazofanya patro
ReplyDelete