Mhesimiwa Rais,
Nakupa pole kwa majukumu mengi na mazito ya kuendesha nchi yetu yenye matatizo mengi na kila mahali hatuonekani kufanikiwa ila matatizo na umasikini kwa watanzania vinaonekana kuongezeka kwa kasi kubwa, huku uzalishaji ukipungua kwa kasi kubwa na wakati huo huo wawekezaji ama wakiamua kuondoa mitaji yao au wale wengine ambao hii ni nchi yao hawana pa kukimbilia wakiwa wanafilisika kutokana na matatizo ya nishati ya umeme na hata mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo na mashine mbalimbali za uzalishaji.
Pamoja na hayo yote naomba leo uchukue muda wako kidogo japo uweze kusoma maoni yangu kwani naamini kuwa yanaweza yakawa ni mchango katika kusaidia katika kukuza uchumi wetu kama yatachukuliwa maanani na kufanyiwa kazi, Pamoja na ukweli kuwa ninajua unavyo vyombo vingi sana na watu wengi sana ambao wanakushauri kwenye mambo mbalimbali si vibaya ukasoma maoni yangu pia .
Mheshimiwa Rais , kwa ruhusa yako naomba leo niweze kuchukua muda huu kukueleza kwa kina juu ya matatizo yaliyopo kwenye biashara ya uwindaji wa Kitalii na haswa kutokana na wasaidizi wako ambao umewateua kutokutaka kupokea ushauri ama kupuuzia ushauri ambao wamekuwa wakipewa na watu mbalimbali na hata ushauri uliotolewa na wabunge wakati wakijadili bajeti ya wizara ya Maliasili na utalii kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Mheshimiwa Rais nimeamua kufanya hivyo kwa kutumia njia hii kwani naamini kabisa kuwa wasaidizi wako na haswa waziri na watendaji wa wizara hiyo wamekuwa hawakuelezi ukweli juu ya biashara hii ya uwindaji wa kitalii au hawana ufahamu wa kutosha kuhusiana na biashara hii na ndio maana wanashindwa kukushauri vizuri kuhusiana na jambo hili .
Hii ni kutokana na ukweli kuwa Matumizi ya raslimali ya wanyamapori hayajapewa thamani na hivyo sekta hii inachangia kidogo sana kitaifa kuliko ilivyotegemewa. Licha ya kuwepo uwezo wa kuzidisha mapato kutokana na wanyamapori kupitia misingi ya ushindani wa kiuchumi, hili halifanyiki. Hii inatoa fursa kwa ufisadi. Kawaida iliyopo katika usimamizi wa wanyamapori kwa sasa hairuhusu kukuza manufaa ya uchumi kitaifa kutokana na raslimali ya wanyamapori.


Kwa nini barua isiwe addressed kwa waziri husika? Yaani kila kitu ni Rais tuu? Kwa sababu hata kama rais akitumiwa hiyo barua ataiforward tuu kwa wazara husika.
ReplyDeletehii ni habari ya kina kweli kama ulivyoandika???
ReplyDeleteNafikiri ametuma kwa Rais labda alishamwambia waziri kwani ukisoma utaona kuwa ni kama mtu ambaye anamlalamikia waziri so angeipeleka kwake asingepatiwa majibu.
ReplyDeleteNaona kuwa kuna tatizo kubwa hapo, kama sheria kweli iko hivyo kwani mimi sijawahi kuiona wala kuisoma basi itakuwa inaenda kinyume na sheria ya uwekezaji ambayo inatoa mwanya kwa wawekezaji kuingia ubia na pia sheria ya makampuni inasema ni vigezo gani vinatumika ktk kusema kuwa hili ni la nje na hili ni kampuni la ndani.
Nakubaliana na huyu bwana kuwa basi sheria irekebishwe na watanzania wawe wanamiliki hisa asilimia hasini kwa hamsini, na
Sijasoma barua yako iliyofichwa lakini kwa huo muhtasari nimeelewa kuwa kuna tatizo kwenye sekta ya utalii hasa wa uwindaji. Napenda nikujulishe kuwa udanganyifu upo sehemu zote za utalii hasa kwenye mbuga za kule kaskazini. Idadi ya watalii wanaokuja nchini hawaripotiwi wote na haiendani na mapatao yanayoripotiwa. Ukitaka kujua kuthibitisha hili, nenda kwenye mbuga yoyote omba data za utalii na mapato yake kama uatapewa. Wanaficha nini kama hakuna uongo unaotakiwa kuingizwa humo?
ReplyDelete