Baadhi ya Wananchi wa Mjini Morogoro wakimsaidia  kumpeleka  kwenye gari derava wa bodaboda  aliyerushwa kutoka  kwenye Pikipiki yake namba  T 818 BFY  baada ya kuiparamia Daladala T 962 BDY iliyokuwa ikitokea Mjini kwenda Kihonda, wakat alipoingia barabara kuu bila kuwa mwangalifu , siku ya septemba 8, mwaka huu, akiwa na abiria wake wakike na wote kujeruhiwa vibaya ,hata hivyo walikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kupatiwa matibabu
 Wananchi wa Mjini Morogoro wakimwangalia mwanamke aliyerushwa kutoka kwenye Pikipiki yenye namba za usajili T 818 BFY aliyokuwa akisafiria baada ya mwendesha pikipiki hiyo kuiparamia Daladala yenye namba T 962 BDY iliyokuwa ikitokea Mjini kwenda Kihonda, wakati Bodaboda hiyo alipoingia barabara kuu bila kuwa mwangalifu , siku ya Septemba 8, mwaka huu ,wote wawili waliumia vibaya na walikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kupatiwa matibabu.
 Baadhi ya Wananchi wa Mjini Morogoro wakiangalia ajali iliyotokea siku ya Septemba 8, mwaka huu eneo la Msamvu , kati ya bodaboda  yenye  namba  T 818 BFY  baada ya  mwendeshaji wake kuiparamia Daladala  T 962 BDY iliyokuwa ikitokea Mjini kwenda Kihonda, wakat i Bodaboda huyo alipoingia barabara kuu bila kuwa mwangalifu , akiwa na abiria wake wakike na wote kujeruhiwa vibaya ,hata hivyo walikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kupatiwa matibabu.
Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Sheria ya Kuvaa Helmet ipo wapi??
    Ni lazima dereva wa pikipiki na abiria wake, wote wavae kinga za kichwa.
    Tatizo la bongo kila mtu hajui wajibu wake kwenye usalama wake na wa wenzake... TUAMKE JAMANI.

    ReplyDelete
  2. wakati mwingine tunaweza kumuongezea matatizo majeruhi kwa nia njema ya kumsaidia,huo ubebaji hapo juu sidhani kama ni sawa.Inabidi tuelekezwe jinsi ya kumsaidia majeruhi.

    mdau Likwilu-Mbamba bay

    ReplyDelete
  3. Huyo anayebebwa hata kama alikuwa hakuumia sana kwenye ajali ataumia zaidi kwa jinsi walivyombeba

    ReplyDelete
  4. tanzania tunatoka mbele tunarudi nyuma! tunaiga upumbavu toka lini pikipiki ikapewa leseni ya kuchukua abiria au hiace huu ni mfumo mbovu kwani ajali za kipumbavu hazitokwisha. mfumo mzuri wa kubeba abiria ni ule wa mabasi ya uda na tax peke yake siyo bajaji kama india pikipiki kama nigeria

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...