Marehemu Selemani Kasaloo Kyanga
Na John Kitime
Mwanamuziki Selemani Kasaloo Kyanga ambaye alifariki dunia juzi amezikwa jana Ijumaa katika makaburi ya Sinza, jijini Dar es salaam.
Marehemu, ambaye alikuwa pacha wa Kyanga Songa walizaliwa Kongo mwaka 1957. Mapacha hao walikuwa ni nyota katika bendi zote walizopitia nchini zikiwamo, Matimila, Makassy, Maquis, Sambulumaa, Ngorongoro Heroes, Tancut Almasi, Sandton Sound, Kalunde Band na bendi nyingine nyingi .

Kasaloo aliyetangulia kuingia nchini akifuatana na Skassy Kasambula mwaka wa 1980, aliweza kutingisha anga za muziki kuanzia pale aliposikika kwenye nyimbo zilizorekodiwa na Super Matimila. Kyanga nae akisindikizana na Issa Nundu walifuatia na sauti zao kuanza kusikika katika recording ya Orchestra Makassy na zile nyimbo Olenge,Bembeya,na pia kuimba na Masiya Radi katika nyimbo Tunagombana Bure.
Kyanga alifia Kenya na Kasaloo amefariki jijini Dar es Salaam kutokana na mapafu yake kujaa maji. Alikuwa Sandton Sound Band aliyojiunga nayo akitokea Kalunde Band.
Kamati ya msiba wa Kasaloo ikiongozwa na King Kiki yenye wajumbe Mzee Mapili, Mzee Manyema, Mbombo wa Mbomboka, Deo Mwanambilimbi, Mzee Jerome, Matunda, Mzee Peter George na John Kitime. Marehemu ameacha wake wawili na watoto 6.
Seleman Kasaloo alibadili dini na kuwa Muislamu katika miaka yake ya mwisho ya maisha, na kutoa wosia kuwa azikwe kwa taratibu za dini yake ya Kiislam.
Kasaloo Kyanga(RIP)
ReplyDeleteAsante JFK kwa taarifa hii, swali hivi aliyekuwa mume wa Jane Butinini ni huyu au ndugu yake? Tena alimtungia na wimbo akiwa Tancut Almasi kule Iringa hii ni sehemu ya maneno "... sitakuwacha mamaaa Butinini hata waseme vipi..".
ReplyDeletePili, bado nasumbuka sana na Kiswahili kinavyochakachuliwa hasa hili neno "NYIMBO" zikiwa nyingi ukiwa ni mmoja unaitwa "WIMBO". Jamani tusiharibu lugha yetu