Asalaam Aleykum Warahmatullah.

Kwa niaba ya uongozi na marafiki wa Kisiwa cha Mafia (Friends of Mafia Island) tungependa kutoa salaam za Rambi Rambi wa wenzetu toka visiwa vya Unguja na Pemba ambao wamepatwa na mtihani mkubwa wa kupotezewa ndugu, jamaa na marafiki zao.

Tungependa kuwafahamisha wana Unguja na Pemba kuwa sisi wana Kisiwa cha Mafia tuko nanyi kwenye kipindi hiki cha huzuni kubwa kwani tunajua fika adha ya usafiri wa Baharini.

Wenzetu wametangulia mbele ya Haki nasi tuko njiani

Inna Lillahi wa Inna Illahi Rajuun

Imetolewa na idara ya habari ya Friends of Mafia Island.

http://www.friendsofmafiaisland.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kaka, kwa moyo mkunjufu tunapokea rambi rambi zenu.Tunaelewa hisia mlizonazo katika msiba huu, hasa ikizingatiwa kua nanyi ni wana visiwani hivyo mnaelewa adha za usafiri wa bahari pamoja na maumivu ya ajali za namna hii.Jazak -Allah- fiq.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...