Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profes Ibrahim Lipumba (kulia),akimwinua mkono kumnadi mgombea wa ubunge wa chama hicho katika jimbo la Igunga, Lucas Mahona, wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho, kwenye Uwanja wa Sokoine leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akihutubia katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Igunga,uliofamyika kwenye Uwanja wa Sokoine leo.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwa na mgombea Ubunge wa chama hicho Leopold Mahona kwenye mkokoteni wa punda na katika maandamano ya wanachama kwenda katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho.
Profesa Lipumba akizungumza jambo na mgombea ubunge wa chama cheke katika jimbo la Igunga, Leopold Mahona.
Moja ya malori ya Chama cha Wananchi (CUF), likiwa limebeba watu kutoka vijiji mbali mbali kuwapeleka katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za jimbo la Igunga, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoineleo.
Moja ya malori ya Chama cha Wananchi (CUF), likiwa limebeba watu kutoka vijiji mbali mbali kuwapeleka katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za jimbo la Igunga, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sokoineleo.
" HATUMWAGII TINDIKALI KAMA WAO" moja wa wafuasi wa CUF akiwa na bango linalosomeka hivyo, wakati wa maandamano ya kumpokea Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye baadaye alizindua kampeni za chama hicho katika viwanja vya kumbukumbu ya Samora mjini Igunga mkoani Tabora. Wiki iliyopita mfuasi mmoja wa CCM alimwagiwa tindikali na watu wanaodaiwa kuwa wa CHADEMA.
Mlinzi wa CUF (kulia) akiwa kazini wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho .
huyo mlinzi vipi tena, yaani CHADEMA vazi lao la kawaida ni la kijeshi kuliko la huyo hapo? job true true.. kazi kweli kweli
ReplyDelete= = =
buffalo,
new york
Duh aisee CUF wamechoka vibaya... hawaeleweki wako upande gani.
ReplyDeletekumwagia watu tindikali ni uchanga wa kisiasa,tunashukuru kama CUF mmeliona hilo.
ReplyDeleteHili suala la haki za wanyama linapigiwa kelele kila siku ulimwenguni CUF haliko kwenye sera zao? au ndo kupagawa na uchaguzi
ReplyDeletehongera CUF kwa siasa safi na za kistarabu
ReplyDeletewaacheni hao wamwagie watu tindi kali nyie ombeni kura tu
HAWA CUF WAPO WAPO TU,KWANI HAWA SI WAMESHAFUNGA NDOA NA CCM,NANI ASIYELIJUA HILI.CUF SI CHAMA PINZANI KM TUNAVYOJUA WAO NI HEWALA TU KWA CCM,WAMEKWISHAUMBUKA SASA kdddk.
ReplyDelete